Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ana uoga fulani kwa mke wake. Maybe suala la kazi anaona kama atamfanyia mke awe na mawazo. Anavyozidi kukaa kimya ndio unavyozidi kupalilia tatizoBishop asante
Sijapenda Sammy anavyomficha mkewe kufukuzwa kazi wanaume sijui mpoje jamani mwambie ukweli mkeo hata kama unaumiza jamani
Hawajui hawa viumbe jamaniAna uoga fulani kwa mke wake. Maybe suala la kazi anaona kama atamfanyia mke awe na mawazo. Anavyozidi kukaa kimya ndio unavyozidi kupalilia tatizo
Ajikaange??Bishop asante
Sijapenda Sammy anavyomficha mkewe kufukuzwa kazi wanaume sijui mpoje jamani mwambie ukweli mkeo hata kama unaumiza jamani
Kumwambia ukweli mkeo ndio kujikaanga mpoje nyieAjikaange??
kuanzia sasa nimekukakidhi rasmi ndugu yangu wa damu kabisa shunie umchukue jumla jumla,baraka zetu unazo toka kwangu,tumosa na sakayo!hivyo baba jilie vyako sasa bureeeeeNimekuja mama, nilikusikia kwa mbaaali, sema nilidhani naota...
kuna mafile yamechanganywa hapaTaxi - (52)
Sammy alikwenda kuketi kwenye sofa sebuleni, mara akawaona Pendo na Winifrida wakimfuata pale kwenye sofa huku wakionesha wasiwasi mkubwa. Sammy alimkumbatia Pendo na wakati huo Winifrida aliketi kimya kwenye sofa huku akimtazama Sammy kwa makini.
“Joyce hajawahi kunidharau kama alivyofanya leo. Nlijua tu mambo kama haya lazima yatatokea ndiyo maana nilikuwa nasita kumweleza ukweli. Cha msingi hapa ni kukabiliana na chochote kitakachojitokeza,” Sammy aliwaza huku akiwa amefura kwa hasira.
Aliendelea kuketi pale akiwa amemkumbatia Pendo aliyekuwa akimtazama kwa makini pasipo kusema chochote. Sammy alikuwa bado ameduwaa, hakujua afanye nini.
Mara walimuona Joyce akitoka chumbani akiwa amevaa gauni na mkononi alikuwa anaburuza begi kubwa la magurudumu. Wote walimtazama kwa mshangao.
“Nashukuru kwa kunionesha kuwa mimi ni mtu nisiye na maana, narudi kwa wazazi wangu Tanga,” Joyce alisema na kuanza kupiga hatua zake taratibu kuelekea kwenye mlango mkubwa ili aondoke.
Sammy alionekana kuchanganyikiwa, aliinuka haraka na kujaribu kumshika Joyce katika hali ya kutaka kumzuia lakini Joyce alimsukuma kisha akamzaba kibao kikali cha shavuni. Alikuwa amekasirika sana na macho yake yalikuwa yanawaka kwa hasira.
“Niache niondoke. Siwezi kukuamini tena!” Joyce alisema kwa hasira.
“Ungenisikiliza kwanza basi…” Sammy alisema huku akimkodolea macho yaliyokuwa yakibembeleza.
“Muda huo sina, wapo watu wa muhimu kwako watakaokusikiliza siyo mimi!”
Pendo alianza kulia kwa uchungu huku akimshika mama yake miguuni kumzuia asiondoke. Winifrida alikuwa amesimama akiwaangalia wote kwa zamu, hakujua afanye nini. Alimshika Pendo aliyekuwa analia kwa uchungu na kumtoa eneo lile akitaka kumpeleka chumbani, japo Pendo alikuwa akirusharusha miguu akitaka aachwe.
“Mwache!” Joyce alisema kwa hasira na kumshika Pendo mkono huku akiwatazama Sammy na Winifrida kwa uchungu.
“Naondoka na mwanangu, siwezi kumwacha kwa mwanaume mwongo na laghai kama wewe,” Joyce alisema na kuanza kupiga hatua huku kamshika Pendo aliyekuwa bado analia. Walitoka nje wakimwacha Sammy amepigwa butwaa.
Sammy alitaka kusema neno lakini sauti haikutoka. Winifrida alisimama akimtazama Sammy kwa huzuni na kushusha pumzi, kisha alitingisha kichwa chake kwa huzuni na kuelekea chumbani kwake…
“Baba Pendo, mbona umenikodolea macho tu na husemi ulichotaka kunimbia, kwani kuna nini!” sauti ya Joyce ilimgutusha Sammy kutoka kwenye mawazo yake.
Sammy alimtazama Joyce na kushusha pumzi za ndani kwa ndani, alishukuru Mungu kuwa yalikuwa ni mawazo tu yaliyompeleka mbali sana kiasi cha kumwogopesha hata kumweleza Joyce alichokusudia kusema. Uso wake ulikuwa umefifia na alionekana kusita sana.
Joyce alimtazama kwa udadisi zaidi, akajiinua kutoka pale kitandani na kujiegemeza kwenye ukuta huku akiendelea kuyatuliza macho yake kwenye uso wa Sammy.
“Una nini, Baba Pendo, mbona unanitisha!” Joyce alisema huku akimeza mate kutowesha koo lake lililoanza kukauka.
Sammy alimtazama Joyce kwa makini na kushusha pumzi huku akilazimisha tabasamu, alionekana kusita sana. Picha aliyoiona mawazoni kwake iliendelea kumtisha, alihisi kuwa endapo angemweleza ukweli Joyce basi hali ingekuwa kama ambavyo picha ile ilionekana mawazoni mwake.
“Amm… amm… hakuna kitu!” Sammy alimudu kusema na kumfanya Joyce ashangae zaidi. Alimkodolea macho Sammy kama vile alikuwa ameona kiumbe cha ajabu kutoka sayari ya mbali.
“Hakuna kitu! Mbona sikuelewi? Ni nini kinachoendelea ambacho hutaki nikijue?” Joyce aliuliza huku akimtazama Sammy kwa udadisi.
Sammy alionekana kupata kigugumizi, aliangalia chini kwa kitambo kifupi akiwa hana cha kusema, aliogopa kumpoteza Joyce. Wakati huo Joyce aliendelea kumkazia macho Sammy kwa udadisi.
“Mimi ni mkeo, kama unanificha jambo unadhani ni nani wa muhimu kwako wa kumweleza? Halafu hadi sasa hujanieleza kuhusu hili gari ulilokuja nalo!” Joyce aliuliza na kumfanya Sammy ahisi kijasho chembamba kikimtoka, hata hivyo aliamua kuuvaa ujasiri. Aliachia tabasamu, akakohoa kusafisha koo lake.
“Nimeamini kweli unanijali mumeo, nilitaka kukupima nione… ukweli ni kwamba niliamua kukufanyia sapraizi…” Sammy alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.
“Sapraizi ya nini?” Joyce aliuliza huku akiendelea kuyatuliza macho yake kwenye uso wa Sammy akijaribu kuyapima yale maneno.
“Nimepandishwa cheo kuwa Naibu Meneja Mkuu, na hilo gari nimepewa, ni la kwangu. Ni la kwetu, Mama Pendo!” Sammy alisema huku akiachia tabasamu pana na kumfanya Joyce amtazame kwa kitambo bila kusema neno akiwa haamini alichokisikia.
Sammy alimtazama Joyce kwa wasiwasi hadi pale alipoliona tabasamu pana likichanua usoni kwake.
“Ooh… hongera sana mume wangu!” Joyce alisema kwa furaha huku akimkumbatia Sammy kwa nguvu
“Ni wewe unayestahili pongezi, mafanikio yangu yote yamechangiwa na wewe,” Sammy alisema huku akishusha pumzi za ahueni, hata hivyo, dhamiri yake ilikuwa inamsuta.
* * * * *
Saa tatu na nusu za usiku Mr. Oduya alitoka kwenye jengo lake la ghorofa kumi na mbili katika barabara ya Bagamoyo, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, baada ya kuwa na kikao kifupi na Balozi Aldolf Mageuzi.
Balozi Mageuzi alikuwa amefika ofisini kwa Mr. Oduya kwa mazungumzo mafupi ili kumpa mrejesho wa kile walichokubaliana walipokutana mara ya kwanza. Hakutaka kumweleza kwenye simu kwa kuogopa mawasiliano yao yangeweza kudukuliwa.
“Enhe, nipe mrejesho mheshimiwa Balozi,” Mr. Oduya alisema kwa shauku baada ya Balozi Mageuzi kuketi.
“Mambo siyo mabaya, mzee Fabian Magulu ameonesha kukuunga mkono katika harakati zako kutokana na jinsi unavyojitoa kukisaidia chama na jamii, hii ni habari njema na kama ujuavyo, huyu mzee ni mtu mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama na serikalini…” Balozi Mageuzi alisema na kumfanya Mr. Oduya aachie tabasamu pana.
Inaendelea...
Bishop asante
Sijapenda Sammy anavyomficha mkewe kufukuzwa kazi wanaume sijui mpoje jamani mwambie ukweli mkeo hata kama unaumiza jamani
Laptop yangu imezingua, imekufa motherboard, hivyo tangu juzi nilikuwa nahangaika kutafuta namna ya kuitengeneza na kuitoa stori hii ili tuendelee na uhondo...Mkuu Bishop Hiluka ndo umetokemea jumla na story yako asee kimya sanaaa
Hakuna kilichochanganywa, hapo kuna picha ambayo Sammy alikuwa akiiona akilini mwake (akidhani kuwa hivyo ndivyo ingekuwa endapo angemweleza Joyce ukweli), ndiyo maana akaghairi na kumwongopea. Soma vizuri utaelewa...kuna mafile yamechanganywa hapa