Stori ya kusisimua - Taxi

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Aug 12, 2011
7,140
14,678
Taxi.jpg

Na Bishop Hiluka
(Mwandishi wa stori za kusisimua zilizowahi kuchapishwa hapa JF za Kizungumkuti!; Laiti Ningejua!; Hekaheka!; Hadi Lini! na nyinginezo)

0685 666964

SAA 1:35 asubuhi, Samuel Kambona alishuka kutoka ndani ya gari aina ya Toyota Alphard la rangi ya bluu katika viunga vya maegesho ya magari vya majengo ya hoteli ya Udzungwa Beach Resort, iliyopo katika ufukwe wa Oystebay, jijini Dar es Salaam.

Gari lile lilikuwa na nembo ubavuni iliyokuwa na maandishi ya Udzungwa Beach Resort.

Samuel maarufu kama Sammy, alikuwa kijana mtanashati mwenye umri wa miaka 35 na msomi wa Shahada ya Umahili ya Biashara za Kimataifa na Lugha (M.A in International Business with Languages), aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Warwick nchini Uingereza,

Alikuwa mrefu na mweupe mithili ya chotara wa kizungu, mwenye sura ya tabasamu muda wote. Urefu, mwili wake wa kimazoezi, utanashati na asili ya ngozi yake nyeupe ni vitu vilivyowavutia wasichana wengi aliokutana nao.

Ukiongezea na ndevu nyingi alizopenda kuzinyoa katika mtindo wa circle beard au kama wengi walivyozoea kuita “O”, vilimfanya azidi kuwa mvuto mkubwa kwa walimbende pindi walipomtia machoni.

Siku ile ilikuwa Ijumaa, kama kawaida yake, Sammy alikuwa katika mwonekano maridadi kabisa, akiwa amevalia shati zuri la rangi ya samawati la kitambaa brandi ya Barba ndani ya suti nyeusi ya aina ya Dunhill, tai ya rangi ya bluu shingoni na viatu ghali vya ngozi halisi kutoka nchini Switzerland.

Pia alikuwa amevaa saa ya mkononi aina ya Cartier iliyokuwa na nakshi ya madini ya dhahabu na kujipulizia manukato ghali aina ya Dolce & Gabbana. Mkononi alikuwa amebeba mkoba wake mdogo wa kiofisi aina ya Pad & Quill wa rangi ya hudhurungi.

Wakati akishuka kutoka kwenye gari manyunyu mepesi ya mvua yalikuwa yakianguka ardhini, lakini bado hayakumzuia Sammy kutembea taratibu akikatisha kwenye viunga vya maegesho ya magari na kuelekea mbele ya jengo la mbele la ile hoteli ya kitalii yenye hadhi ya nyota tano.

Wakati akitembea macho yake yaliangaza huku na kule kana kwamba alikuwa akitafuta kitu. Alipishana na askari mmoja wa ulinzi kutoka kampuni ya ulinzi ya Spark K7 aliyekuwa akilinda eneo lile la viunga vya maegesho ya magari.

Eneo lile lilikuwa pana likiwa na uwezo wa kuruhusu magari madogo hadi 100 kuegeshwa kwa wakati mmoja, na lilikuwa limepandwa miti mirefu ya kivuli aina ya ‘Quercus virginiana’ na ‘Arecaceae’ iliyojulikana pia kama ‘coconut palms’.

Pia eneo lile lilipandwa nyasi nzuri laini aina ya ‘Citronella’ na kulikuwa na bustani ya maua ya kupendeza yaliyotoa hewa safi ya upepo wa asili baina ya sehemu moja ya maegesho ya magari na sehemu nyingine, ndani ya uzio wa yale majengo ya hoteli.

Kwa yeyote aliyefika Udzungwa Beach Resort angeweza kubaini mara moja kuwa majengo ya hoteli hiyo yalijengwa kwa ufanisi wa hali ya juu.

Kulikuwa na majengo makuu mawili, moja lilikuwa mbele na la pili lilikuwa nyuma na kila moja lilikuwa na ghorofa saba za juu na mbili za chini, zilizotumika kwa ajili ya kumbi za burudani, kumbi za mikutano na migahawa ya kisasa ya chakula cha kitanzania na cha kimataifa. Pia kulikuwa na maduka na ofisi za utawala kwenye orofa ya chini nay a kwanza ya jengo la mbele.

Katika eneo lile kulikuwa na duka kubwa la bidhaa mbalimbali maarufu kama “supermarket”, duka kubwa la vipodozi na nguo za kisasa (boutique), na duka la kubadilishia fedha za kigeni maarufu kama “Bureau de Change” na vyumba viwili vidogo vyenye Mashine za ATM

Pia kulikuwa na jengo maalumu la klabu iliyojulikana kama Paradise Club, ambayo ilikuwa kwenye jengo la nyuma iliyowakutanisha mabilionea na baadhi ya vigogo serikalini na ilikuwa na ulinzi mkubwa sana, nje na ndani ya klabu.

Walioruhusiwa kuingia ndani ya klabu hiyo ni wanachama tu waliokidhi vigezo na kusajiliwa, ambao walilipa kiasi kikubwa cha ada ya uanachama kila mwaka.

Ndani ya majengo yote ya hoteli hiyo kulikuwa na kamera za usalama (CCTV) kila kona, viyoyozi vilivyosambaa kila mahali, na kutoka ghorofa moja kwenda nyingine kulikuwa na ngazi za kawaida na vyumba maalumu vya lifti za kisasa. Pia kulikuwa na ngazi iliyoendeshwa kwa umeme.

Yale majengo yalijengwa katika eneo tulivu mno lisilo na bughudha la ufukwe wa Oysterbay, jirani kabisa na ofisi za kibalozi na makazi ya watu wenye ukwasi, takriban kilomita tatu tu kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Kwa watu wengi wenye ukwasi, Udzungwa Beach Resort ilikuwa ndiyo sehemu nzuri na tulivu zaidi ya kwenda kujipumzisha na kufurahia maisha, kwani ilikuwa imezungushiwa uzio madhubuti wenye ulinzi na kamera za usalama ulioifanya kuwa mahali patulivu zaidi na pa usalama wa uhakika.

Asubuhi ile kulikuwa na magari machache madogo na mabasi mawili ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Cape Town cha nchini Afrika Kusini na Chinhoyi cha nchini Zimbabwe yaliyokuwa yameegeshwa katika viunga vya maegesho ya magari.

Pia kulikuwa na malori mawili makubwa ya kubebea watalii wa masafa marefu aina ya Mercedes Benz, yaliyokuwa yameegeshwa mwisho kabisa wa yale majengo.

Mbele ya ile hoteli katika jengo la mbele Sammy aliipita milingoti saba iliyokuwa na bendera za Afrika Mashariki, Marekani, Uingereza, India, China, Afrika Kusini na bendera yenye nembo ya Udzungwa Beach Resort, zilizokuwa zinapepea taratibu.

Kulikuwa na mlango mkubwa wa vioo mbele ya jengo na varanda pana yenye ngazi iliyofunikwa kwa kofia nzuri ya zege ikiwa na sakafu nzuri yenye marumaru iliyonakshiwa kwa maandishi ya “Udzungwa Beach Resort”.

Kijana mmoja askari wa kampuni ya ulinzi ya Spark K7 alikuwa amesimama kikakamavu kwenye ile varanda pana akiwa kando ya ule mlango mkubwa wa vioo wa kuingilia ndani. Yule askari wa ulinzi aliyeitwa Fred Luvanda alimuona Sammy na kumpokea kwa tabasamu la kirafiki lililokuwa na bashasha zote kwenye uso wake.

Endelea kufuatilia...

SEHEMU 2
Taxi - (2)

“Habari za asubuhi, Boss!” Fred alimsalimia Sammy wakati alipokuwa akizikwea zile ngazi za ile varanda.

“Salama tu, Fred,” Sammy alijibu huku naye akiachia tabasamu na kuusogelea ule mlamgo mkubwa wa kioo ambao ulijifungua wenyewe kwa vioo vyake kujisogeza pembeni ili kumruhusu aweze kuingia ndani.

“Vipi, kesho utaenda Uwanja wa Taifa?” Fred alimtupia swali Sammy kabla hajaingia ndani ya lile jengo na kumfanya asimame na kugeuza shingo yake kumtazama.

“Kesho lazima niende, safari hii tumejipanga kweli kweli, nyie Simba msubiri kipigo tu,” alisema Sammy kwa msisitizo huku akiangua kicheko hafifu.

“Aa wapi, kwa timu ipi mtufunge sisi?” alisema Fred aliyeonekana kuwa shabiki kindakindaki wa timu ya Simba na aliiamini mno timu yake.

“Basi kesho usizime simu, mpira ukiisha tu nitakutafuta… safari hii hamtoki salama pale kwa Mchina. Tunawapiga hizi!” Sammy alisema kwa kujiamini huku akimuonesha Fred ishara ya vidole vitatu.

“Thubutuu… mumpige nani tatu, labda kama unaongea kinyume chake!” Fred alisema huku akiachia kicheko hafifu, na kuongeza, “Nyie ni vibonde wetu tu.”

“Ningekwambia tuwekeane dau lakini najua utaliwa tu, sisi ndio mabingwa wa kihistoria bwana!” Sammy alisema huku akiingia ndani, na kumwacha Fred akiwa anatabasamu.

Ndani ya lile jengo Sammy alipokewa na mhudumu mmoja wa kiume aliyekuwa amevaa shati jeupe lenye kola ya rangi ya samawati, suruali ya rangi ya samawati, koti la suti la rangi ya bluu, tai ndogo ya rangi ya bluu na kofia ya bluu kichwani.

Yule mhudumu alimsalimia Sammy kwa bashasha zote huku akionesha tabasamu la kirafiki kwenye uso wake. Sammy aliitikia salamu yake na kumpita huku akitembea taratibu kupita juu ya zulia nene la rangi nyekundu, akatokea katika eneo la mapokezi.

Eneo lile la mapokezi lilikuwa pana lenye mazingira yaliyoashiria ustaarabu, yakiwa masafi na yenye mandhari yenye kuvutia kiasi cha kutoa liwazo kwa mgeni yeyote aliyeingia, huku likizungukwa na meza nzuri ya kaunta yenye umbo la nusu duara iliyotengenezwa kwa mbao za mninga, na ilikuwa ikitazamana na makochi mawili makubwa ya ngozi laini ya sofa.

Pembeni ya kidogo pia kulikuwa na makochi mengine manne madogo ya ngozi laini ya sofa yaliyopangwa kwa ustadi mkubwa na mbele yake kulikuwa na meza fupi za vioo zilizokuwa katika mpangilio uliovutia.

Ukutani kulikuwa na madirisha makubwa ya vioo yaliyoruhusu mwanga kutoka nje kuingia mle ndani na yalikuwa na mapazia marefu yenye rangi nzuri za kupendeza yaliyobanwa vizuri pembeni yake. Ukutani kulikuwa na runinga kubwa ya bapa iliyokuwa ikionesha kipindi cha mitindo kilichorushwa na kituo cha runinga cha Nuru.

Pia kulikuwa na kitufe kikubwa chekundu cha kengele ya hatari pembeni ya mitungi miwili mikubwa ya gesi ya kuzimia moto wa dharura.

Sammy alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akilakiwa na hewa safi ya ubaridi iliyokuwa ikisambazwa na viyoyozi vikubwa vilivyokuwa kwenye kona mbili za eneo lile, kutokea juu dari ya gypsum iliyonakshiwa vyema.

Sammy aliwatupia macho watu wachache waliokuwa wameketi kwenye yale makochi ya sofa katika eneo lile la mapokezi: miongoni mwao kulikuwa na Wazungu wawili walioonekana kuwa wapenzi kutokana na mkao wao.

Mwanamume alikuwa mrefu na mwembamba akiwa amevaa fulana nyeupe, suruali nyeusi ya jeans na raba miguuni, na mwanamke alikuwa mrefu kiasi na alivaa gauni fupi jeusi la kukata mikono lililolichora vyema umbo lake na kuyaacha mapaja yake wazi.

Mbali na wale Wazungu, kulikuwa na Waafrika watatu, mwanamume mmoja wa makamo, mrefu na alikuwa na ndevu nyingi zilizokizunguka kidevu chake, alivaa suti maridadi nyeusi na miwani ya macho, pia kulikuwa na vijana wawili walioonekana ni wapenzi au mume na mke waliotoka kufunga ndoa na sasa walikuja kwa ajili ya fungate.

Yule kijana wa kiume alikuwa mrefu na maji ya kunde, alivaa shati la bluu lenye mistari myeupe na suruali nyeusi, na muda wote alikuwa anatabasamu. Mwenzi wake alikuwa msichana mrembo mrefu kiasi, alikuwa amevaa gauni la kitambaa cha bazee lililoshonwa na kudariziwa vizuri na kichwani alikuwa amevaa kilemba.

Mbele ya meza kubwa ya mapokezi kulikuwa na watu wazima wawili wenye asili ya Kiasia waliokuwa wamesimama na mabegi yao, na ilionekana kuwa walikuwa ni mke na mume walioishi maisha marefu ya ndoa yenye furaha na walifika hapo kwa ajili ya mapumziko.

Nyuma ya ile meza kubwa ya mapokezi kulikuwa na wahudumu wawili vijana, mmoja wa kiume na mwingine wa kike, waliokuwa katika sare nadhifu za kazi: mashati meupe yaliyokuwa na kola za rangi ya samawati, suruali za rangi ya samawati na makoti ya suti ya rangi ya bluu iliyokolea, na shingoni wakiwa wamevaa tai ndogo za samawati zilizowakaa vizuri.

Mhudumu wa kiume aliyeitwa Abbas Saleh alikuwa anazungumza na wale wenzi wenye asili ya Kiasia, na yule mhudumu wa kike aliyefahamika kwa jina la Rose Mahenge alikuwa akiongea na simu huku akiweka vizuri mazingira ya pale mezani.

Alikuwa msichana mrembo sana mwenye uso wa umbo duara, akiwa na umbo kubwa lililovutia mno lenye kiuno chembamba lakini imara, kilichoshikilia minofu laini ya mapaja yake makubwa, na hakuwa amezidi miaka therathini.

Rose alimuona Sammy wakati akipita katika eneo lile la mapokezi na haraka aliishusha ile simu na kuacha kazi aliyokuwa akiifanya, uso wake ukachanua kwa tabasamu pana lenye bashasha lililovifanya vishimo vidogo mashavuni kwake vichomoze haraka.

Japokuwa alikuwa amevaa sare za kazi lakini bado uzuri wake haukujificha kabisa. Alikuwa na macho mazuri malegevu lakini yaliyoonekana kuwa makini kuliko hata simba jike anayewinda.

Alikuwa mrefu wa wastani na mweupe kwa rangi ya ngozi iliyokuwa na mng’aro wa aina yake na mvuto wa kipekee, na hakuhitaji vikorombwezo vya aina yoyote kuinakshi ngozi ile

Sammy alimpiga ukope huku akipunga mkono wake kumsalimia, tabasamu kabambe la aina yake lilichanua usoni kwake na kumfanya Rose ajikute akiachia kicheko hafifu kilichowafanya watu wote wageuke kumtazama Sammy kwa makini, na baadhi yao walijikuta wakiachia tabasamu.

The guy is so handsome… ni mpole, mcheshi, mchapakazi na zaidi ya yote ana moyo wa upendo na huruma,” Rose aliwaza huku akiendelea kumtazama Sammy kwa tabasamu.

Kwa kuwa Sammy hakuwa akipenda kutazamwa na kugeuka kivutio alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuzitupa hatua zake haraka haraka kulivuka eneo lile akielekea eneo zilipokuwa ngazi za lile jengo la hoteli za kuelekea juu. Alipoaliacha eneo lile la mapokezi aliupita mlango wa kuingia kwenye kaunta kubwa ya vinywaji.

Itaendelea...

SEHEMU YA 3
Taxi - (3)

Kisha alielekea upande wa kushoto na mbele yake akauvuka ukumbi mkubwa kiasi wa kisasa wa chakula, uliokuwa na meza nyingi za kulia chakula zenye umbo mstatili zilizozungukwa kwa viti nadhifu vyenye foronya laini.

Katika ule ukumbi wa chakula kulikuwa na watu wachache waliokuwa wakijipatia stafustahi katika meza zilizokuwa zikimefunikwa kwa vitambaa visafi vya rangi nyeupe na juu yake kuliwekwa kadi ngumu za kupendeza zenye orodha ya vyakula na vinywaji vilivyokuwa vinapatikana katika hoteli ile.

Mbele kidogo Sammy alipishana na wazungu watatu, wanawake wawili na mwanamume mmoja waliokuwa wanaelekea kwenye ukumbi wa chakula. Sammy aliwasalimia na kuifuata korido ndefu iliyokuwa upande wake wa kulia na kisha akavivuka vyumba viwili vya lifti za kuelekea ghorofa za juu za lile jengo la hoteli.

Katika eneo lile, kulikuwa na wahudumu wawili wa ile hoteli waliokuwa wakisubiri lifti ya kuelekea juu, na wakati huo huo mlango wa chumba kimoja cha lifti iliyokuwa imefika sehemu ya chini ya jengo ulifunguka na kuwaruhusu watu kadhaa kutoka ndani yake, huku wakiwapisha wale wahudumu kuingia.

Sammy alielekea mbele zaidi akaupita mlango mkubwa wa kuelekea kwenye ukumbi wa mazoezi, na juu ya mlango ule kulikuwa na kibao cheusi chenye maandishi meupe yaliyokuwa yakisomeka ‘GYM’, yaani Ukumbi wa mazoezi.

Upande wa kushoto wa eneo lile kulikuwa na mlango mwingine uliokuwa unaelekea sehemu ya maliwato na hatua chache mbele yake, mwisho kabisa wa ile korido kulikuwa na mlango mkubwa wa vioo uliokuwa na maandishi juu yake yaliyoandikwa “Administration”, na upande wa kulia kulikuwa na ngazi za kuelekea juu ya lile jengo la hoteli.

Sammy alizikwea zile ngazi hadi ghorofa ya kwanza, akaufikia mlango mwingine mkubwa wa vioo uliokuwa na maandishi juu yake yaliyoandikwa “Administration”.

Aliusukuma ule mlango na kutokea kwenye korido pana iliyokuwa na ofisi kadhaa, ofisi yake ilikuwa mkono wa kulia mara baada ya kuingia katika eneo lile. Juu ya kizingiti cha mlango wa ile ofisini kulikuwa na kibao cheusi kilichokuwa na maandishi meupe: “Event Manager”. Ulikuwa ni mlango mkubwa na imara wa mbao ngumu za mninga.

Sammy alitoa kadi ngumu ya kielektroniki, mfano wa kadi ya benki, kutoka kwenye mkoba wake na kuipitisha juu ya kile kitasa maalumu cha mlango ule na kuusukuma ule mlango. Ukafunguka na kumruhusu kuingia ndani.

Ilikuwa ofisi kubwa na nzuri iliyokuwa na mandhari tulivu kama ilivyo kwa ofisi yoyote ya kisasa yenye vitu vyote muhimu. Sammy aliwasha swichi ya kiyoyozi makini aina ya Boss kilichoanza kusambaza hewa safi ya ubaridi mle ndani.

Alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kukatisha katikati ya kile chumba kukielekea kiti chake, kisha akavua koti lake na kulitundika kwenye “henga” maalumu ya kutundikia koti.

Aliminya midomo yake, akaitia mikono yake mifukoni kwa utulivu akionekana kutafakari jambo kwa kitambo kifupi, kisha alisogea kwenye dirisha pana la kioo, lililokuwa limefunikwa kwa mapazia mawili mepesi na marefu ya rangi ya bluu, kando ya meza yake kubwa ya ofisi.

Aliyasogeza yale mapazia pembeni na kuruhusu mwanga wa jua upenye mle ndani kupitia ukuta msafi wa kioo cha lile dirisha. Kwa dakika kadhaa alitulia pale dirishani huku akiyatazama mandhari ya lile jengo la hoteli kwa upande ule wa nyuma, kana kwamba alikuwa akiyaona kwa mara ya kwanza.

Upande ule wa nyuma kulikuwa na bustani nzuri ya nyasi laini aina ya ‘Citronella’ zilizokuwa zimekatwa vizuri na kupendeza, huku mandhari yake ikipambwa na aina mbili za maua mazuri: ‘Magnolia grandiflora’ ya rangi ya maziwa na maua aina ya ‘lotus’ yenye mchanganyiko wa rangi nyeupe, pinki na zambarau.

Katika eneo lile kulikuwa na sehemu za kupumzika zenye viti na meza chini ya miamvuli mikubwa yenye rangi za kupendeza na mabwawa makubwa ya kuogelea, sehemu zenye viti maalumu vya kupumzikia chini ya miti mizuri aina ya coconut palms pamoja na vibanda vidogo vya faragha.

Kwa utulivu huku akiwa bado ameweka mkono wake wa kushoto mfukoni na mkono wa kulia akiwa ameuegemeza pale kwenye kioo cha dirisha, alijikuta akivutiwa kuwaangalia wazungu wawili, mwanamke na mwanamume waliokuwa wameketi chini ya lile ghorofa kwenye vibanda vidogo vya faragha wakiongea huku wakipapasana sehemu mbalimbali za miili yao kwa mahaba.

Kama mtu aliyekumbuka jambo, alishusha pumzi za ndani kwa ndani kisha akaenda kuketi kwenye kiti chake kikubwa cha ngozi halisi cha kiofisi cha kuzunguka na chenye magurudumu madogo yaliyokiwezesha kusogea.

Mbele yake kulikuwa na meza kubwa ya ofisini ambayo juu yake kulikuwa na kompyuta mpya aina ya iMac Pro, mashine ndogo ya kuchapa barua (printing machine) aina ya HP LaserJet na ‘trei’ mbili zilizokuwa na maandishi ya ‘IN’ ikimaanisha kazi zilizoingia na ‘OUT’ ikionesha kazi zinazotoka, huku lile trei la kazi zilizoingia likiwa tupu.

Pia juu ya ile meza mbele yake kulikuwa na kibao kidogo kilichokuwa na maandishi ya “Samuel Komba - Event Manager”, simu ya mezani, majalada kadhaa, vitabu, kidau cha wino, mhuri na kichupa kidogo chenye wino mweupe wa kufutia maandishi.

Kando ya ile meza jirani na lile dirisha pana la kioo, kulikuwa na rafu kubwa ya vitabu na majalada mbalimbali yaliyopangwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Mbele yake kulikuwa na seti moja ya makochi madogo ya ngozi laini ya sofa yaliyoizunguka meza fupi ya kioo yenye umbo la yai na chini ya meza ile kulikuwa na magazeti na majarida kadhaa tofauti.

Ukutani kulikuwa na picha kubwa mbili, moja ya Rais wa Tanzania na ya pili ilikuwa ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, na sakafu ya ofisi ile ilifunikwa kwa zulia maridadi jekundu.

Sammy alipotaka kuwasha kompyuta yake simu yake ya mkononi ikaanza kuita kwa fujo, Sammy aliichukua ile simu na kuangalia namba ya mpigaji lakini hakuweza kumtambua kwani ilikuwa ngeni. Akaipokea.

Hello!” Sammy alisema mara baada ya kuiweka ile simu kwenye sikio lake.

“Hallo” sauti nyororo ya mwanamke ilisikika kutoka upande wa pili wa ile simu. Mara kukazuka ukimya uliomshangaza kidogo Sammy.

“Ndiyo!” Sammy alisema huku akijaribu kusikiliza kwa makini.

“Nani mwenzangu?” ile sauti nyororo ya kike ilisikika ikiuliza kwa mshangao na kumfanya Sammy akunje sura yake.

“Kwani wewe ulikusudia kumpigia nani?” Sammy naye aliuliza kwa mshangao.

“Sina uhakika…” ile sauti nyororo ya kike ilijibu na kumfanya Sammy aachie kicheko hafifu.

“Nadhani utakuwa umekosea namba,” alijibu huku akilamba midomo yake.

“Inawezekana!” ile sauti nyororo ya kike ilisema.

“Huwa inatokea… usijali sana,” Sammy alisema na kukata simu.

Taxi - (4)

Alipoiweka simu yake mezani mara simu ya mezani ikaanza kuita na kumshtua. Sammy aliitazama ile simu kwa muda kana kwamba alikuwa akijishauri kuipokea au la, kisha akainyanyua na kuipeleka kwenye sikio lake.

Hello…” Sammy alisema mara tu alipoiweka ile simu kwenye sikio lake.

Mr Kambona, I need you in my office right now!” (Nahitaji kukuona ofisini kwangu sasa hivi!) sauti nzito ya Meneja Mkuu wa Udzungwa Beach Resort, Dk. Daniel Masanja ilisikika kutoka upande wa pili wa ile simu na kumshtua Sammy.

Ooh… okay, Sir!” (sawa bosi) Sammy alisema mara baada ya kugundua kuwa alikuwa anaongea na mkuu wake wa kazi. Hata hivyo, simu ilikwisha katwa kabla hata hajaitikia.

Sammy alipigwa butwaa na kuitazama ile simu kwa sekunde kadhaa huku akipitisha ulimi wake chini ya mdomo, kisha akameza funda la mate kutowesha koo lake lililoanza kukauka.

“Hata hatusalimiani… kwani kuna tatizo lolote?” Sammy alijiuliza huku akiirudisha ile simu kwenye eneo lake na kuinuka. Akachukua koti lake na kulivaa, kisha akatoka haraka na kuziendea ngazi, akashuka haraka haraka akielekea sehemu ya chini ya lile jengo.

Aliufikia ule mlango mkubwa wa vioo uliokuwa na maandishi juu yake yaliyoandikwa “Administration” mwisho kabisa wa ile korido, akausukuma na kuingia, kisha akatokea kwenye korido pana kama ile ya ghorofa ya kwanza.

Alivuta hatua zake akiupita mlango wa kuingia katika ukumbi mkubwa kiasi wa mikutano uliokuwa na kibao cheusi juu ya mlango kikiwa na maandishi meupe ya “Board Room”.

Mbele yake kulikuwa na mlango mwingine wa kuingia katika ofisi ya Daniel Masanja uliokuwa na kibao cheusi juu ya mlango kikiwa na maandishi meupe ya “General Manager”.

Sammy alisimama pale nje ya mlango na kuupimia utulivu wa eneo lile. Eneo lilikuwa tulivu na hapakuwa na sauti yoyote ya maongezi iliyosikika kutokea ndani ya ofisi ya Meneja Mkuu.

Sammy alishika kitasa cha mlango na kukinyonga kisha akausukuma ule mlango na kuingia ndani. Alimkuta katibu muhtasi wa Meneja Mkuu aliyeitwa Salha Kibari, akiwa ameinamisha uso wake kwenye kompyuta akiwa ‘bize’ na kazi za kiofisi.

Salha alikuwa msichana mrefu, umri wake haukuzidi miaka therathini na tano, alijaaliwa uzuri wa sura ya kitoto na macho makubwa malegevu, alikuwa na umbo namba nane lililokuwa likiwapagawisha wanaume wengi wakware waliokuwa wakimtazama kwa macho ya matamanio alipowapita.

Ujio wa Sammy ulimfanya Salha ainue uso wake kumtazama Sammy huku akiachia tabasamu lenye bashasha mbele ya Sammy.

“Karibu, Bosi Sammy,” Salha alimkaribisha Sammy huku akiendelea kutabasamu.

“Asante, Salha… habari za asubuhi?” Sammy alisalimia huku akiufunga mlango nyuma yake baada ya kuingia.

“Nzuri, Bosi, kwema nyumbani?”

“Kwema…” Sammy alisema kisha alimuashiria Salha kuwa alihitaji kuingia ofisini kwa Dk. Masanja.

Salha alibetua kichwa chake kukubali na kumsindikiza Sammy kwa macho wakati akiuelekea ule mlango. Sammy aligonga mlango wa ofisi ya Dk. Masanja mara moja na kuufungua, akaingia ndani ya ile ofisi.

Ilikuwa ofisi nzuri na pana zaidi kuliko ile ya Sammy, ikiwa na mazingira nadhifu na yaliyovutia zaidi kwa mpangilio wa samani za kisasa, ilikuwa na zulia jekundu sakafuni na meza ndefu ya ofisini yenye viti kumi na viwili. Viti sita upande wa kushoto na viti vingine sita upande wa kulia.

Ndani ya ile ofisi Dk. Masanja, mwenye umri wa miaka 55, alikuwa ameketi kwenye kiti chake kikubwa cha ngozi halisi cha kiofisi cha kuzunguka na chenye magurudumu madogo, nyuma ya meza yake kubwa ya ofisini mwisho wa ofisi ile upande wa kulia.

Alikuwa mrefu na mnene, maji ya kunde na mwenye sura mviringo iliyoonesha utulivu, na macho yake yalikuwa makubwa yenye uchovu lakini yaliyokuwa na kila dalili ya kuonya. Kichwani alikuwa na upara uliokuwa unawaka na usiokuwa na unywele hata mmoja.

Alikuwa amevaa shati zuri jeupe lenye mistari midogo ya rangi ya bluu, la mikono mirefu, brandi ya Maria Santangelo kutoka nchini Italia, tai nyekundu shingoni brandi ya Massimo dutti kutoka Hispania, na suti ghali ya kijivu ya single button, brandi ya Piacenza, kutoka Italia. Pia alikuwa amevaa miwani.

Muda wote alikuwa ameegemea kiti chake cha ofisi, mche wa sigara ulikuwa unateketea taratibu kwenye pembe ya mdomo wake na macho yake yalikuwa yanatazama gazeti alilokuwa amelishika mkononi, huku uso wake ukiwa umekunja ndita kama mtu aliyekuwa amechukizwa na jambo fulani.

Ukimya mzito ndani ya ofisi ile ulimfanya Sammy asikie sauti hafifu ya hatua zake mwenyewe, wakati alipokuwa akitembea taratibu kukatisha kile chumba akielekea kule kwenye meza alikokuwa ameketi Dk. Masanja.

Dk. Masanja aliendelea kuketi kwa utulivu kwenye kiti chake nyuma ya ile meza kubwa akiwa katika uso wa kusawajika kidogo, huku akikodolea macho yake kwenye lile gazeti pasipo kumwangalia Sammy, hakutaka kuongea neno lolote, hata baada ya kugundua kuwa Sammy alikuwa ameingia ndani ya ile ofisi.

Sammy alisimama, akamtazama bosi wake kwa wasiwasi kidogo kisha alikunja sura yake huku akionekana kuanza kupata shaka fulani. Halikuwa jambo la kawaida kwa Dk. Masanja kuwa mkimya kiasi kile! Sammy alishangaa sana.

Juu ya meza ya Dk. Masanja kulikuwa na kompyuta mpakato (laptop) ya rangi ya fedha aina ya MacBook Pro, magazeti, vitabu na majalada machache yaliyokuwa yamepangwa kwa ustadi mkubwa pembeni ya kibao kidogo kilichochongwa kwa unadhifu kikiwa na maandishi yaliyosanifiwa na kuandikwa: “Dr. Daniel Masanja – General Manager” pamoja na kidau cha wino na mhuri wa ofisi.

Upande wa kulia wa ofisi ile kulikuwa na rafu kubwa ya mbao iliyosanifiwa kwa ustadi wa hali ya juu, na ilipambwa na vitabu na majalada mbalimbali, huku juu yake kukiwa na picha kubwa ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na ya Rais wa Tanzania zilizokuwa zimetundikwa ukutani. Kwenye sakafu ya ile ofisi kulikuwa na zulia nene jekundu.

“Shikamoo, Boss!” Sammy alisalimia huku akimtazama Dk. Masanja kwa wasiwasi kidogo.

Dk. Masanja hakuitikia ile salamu ya Sammy wala hakumtazama usoni, aliendelea kulikodolea macho lile gazeti aliloshika mkononi huku uso wake ukiwa umesawajika na mawazo yake yakiwa mbali sana.

“Boss mbona leo unaonekana hauko sawa, kuna tatizo lolote?” Sammy aliuliza huku akiwa na mshangao mkubwa.

“Sina shida na salamu yako,” Dk. Masanja alisema huku akivuta mtoto wa meza na kuchukua bahasha ndogo ya khaki iliyokuwa na barua ndani yake, akanyoosha mkono wake kumpa Sammy bila hata kumtazama usoni. Uso wake ulikuwa bado umekunja ndita.

Sammy alishtuka sana na kuitazama ile bahasha kwa mshangao mkubwa, alishusha pumzi za ndani kwa ndani na macho yake yakatulia kwenye uso wa Dk. Masanja. Alimkazia macho huku akionesha wasiwasi mkubwa.

Endelea kufuatilia stori hii ya kusisimua...
 
Ila ndugu Muandishi punguza kuelezea vitu kama ofisi vitu vya ndani story inakuwa inaboa unatumia maneno mengi kuelezea mazingira ya sehem muhusika alipo kuliko story yenyewe
Nashukuru kwa maoni yako lakini hiyo ndiyo style yangu ya uandishi, na-enjoy kuelezea kile ninachokiona kwenye akili yangu. Kama hupendi sina namna nyingine ya kukulazimisha...
 
Taxi - (5)

ILIPOISHIA

Dk. Masanja hakuitikia ile salamu ya Sammy wala hakumtazama usoni, aliendelea kulikodolea macho lile gazeti aliloshika mkononi huku uso wake ukiwa umesawajika na mawazo yake yakiwa mbali sana.

“Boss mbona leo unaonekana hauko sawa, kuna tatizo lolote?” Sammy aliuliza huku akiwa na mshangao mkubwa.

“Sina shida na salamu yako,” Dk. Masanja alisema huku akivuta mtoto wa meza na kuchukua bahasha ndogo ya khaki iliyokuwa na barua ndani yake, akanyoosha mkono wake kumpa Sammy bila hata kumtazama usoni. Uso wake ulikuwa bado umekunja ndita.

Sammy alishtuka sana na kuitazama ile bahasha kwa mshangao mkubwa, alishusha pumzi za ndani kwa ndani na macho yake yakatulia kwenye uso wa Dk. Masanja. Alimkazia macho huku akionesha wasiwasi mkubwa.

SASA ENDELEA...

“Kwani kuna tatizo gani, Boss?” Sammy aliuliza kwa wasiwasi huku akionekana kuchanganyikiwa kidogo.

“Unashtuka nini, kwani hujawahi kupewa barua?” Dk. Masanja alimuuliza Sammy huku akimtazama kwa mara ya kwanza tangu aingie ofisini kwake.

“Nimeshawahi kupewa, tena nyingi tu…” Sammy alisema huku akihisi jasho jepesi likianza kumtoka na ubaridi wa woga wa aina yake ukimtambaa mwilini.

“Sasa! Kinachokushtua ni nini?” Dk. Masanja aliuliza tena huku akiwa amemkazia macho Sammy.

“Hakuna tatizo, ila…” Sammy alitaka kusema lakini Dk. Masanja alimkata kauli.

“Kama hakuna tatizo basi chukua barua yako na usinipotezee muda wangu hapa,” Dk. Masanja alisema kwa sauti iliyovuma kwa ghadhabu huku akimkazia macho Sammy.

Sammy alimtazama yule mzee kwa makini, alitaka kunyoosha mkono wake kuichukua ile barua lakini akasita. Dk. Masanja alimkazia macho huku akimsisitiza kuichukua ile barua.

Sammy aliipokea na kuichana pale pale, akaifungua na kutoa karatasi iliyokuwa ndani yake, na hapo akakutana na na kichwa acha habari kilicoaandikwa: “Yahusu kusimamishwa kazi kwa utovu wa nidhamu na kuihujumu kampuni”

Sammy alipigwa butwaa na kuiachia ile barua ikadondoka sakafuni. Alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akihisi mapigo ya moyo wake yakibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!

I can’t believe this! Unawezaje kunifanyia hivi?” Sammy aliuliza huku akikihisi joto kali sana likimtambaa mwilini! Alionekana kupatwa na mshtuko mkubwa sana kutokana na barua ile.

Dk. Masanja hakujibu bali alibaki kimya akimtazama Sammy kwa hasira. Kikapita kitambo kifupi cha ukimya huku wakitazamana kama majogoo waliotaka kupigana.

“Nimehukumiwa bila makosa! Sijawahi hata kupewa barua ya onyo, iweje leo naandikiwa kuwa mimi mtovu wa nidhamu na naihujumu kampuni! Lazima kuna kitu kinaendelea hapa, si bure,” Sammy alisema kwa uchungu.

“Kama unadhani hujatendewa haki unaweza kukata rufaa kwenye ngazi husika, ila kwa sasa hutakiwi kuwepo hapa na kampuni haitahusika na jambo lolote linalokuhusu,” Dk. Masanja alisisitiza.

Sammy alionekana kunywea sana utadhani kifaranga cha kuku kilichonyeshewa na mvua. Alifungua mdomo wake kutaka kusema lakini maneno hayakutoka, akabaki mdomo wazi huku akimkodolea macho Dk. Masanja. Donge la fadhaa lilikuwa limemkaba kooni.

Dk. Masanja alionekana kumpuuza Sammy na kuyahamishia macho yake kwenye lile gazeti alilokuwa ameshika mkononi, japo ilionekana wazi kuwa akili yake haikuwa pale.

Sammy aliinamisha uso wake chini na kuanza kutafakari, fikra zikamjia kwamba huenda alikuwa ndotoni, hata hivyo, hisia zake zilimtanabaisha kuwa ile haikuwa ndoto bali ni kitu halisi kilikuwa kinatokea.

Hakujua ni utovu upi wa nidhamu aliowahi kumfanyia mkuu wake wa kazi, kiasi cha kusimamishwa kazi. Hakukumbuka ni lini aliwahi kuihujumu kampuni! Kilichomjia akilini ni jinsi alikuwa akijitoa kwa moyo wake wote kuitumika kampuni ile na alivyomuheshimu mkuu wake wa kazi. Hakutaka kabisa kuamini kwamba kitu kama hicho kingeweza kutokea.

I’m totaly confused! Au pengine huyu boss ana hofu ya kupokonywa cheo? Kwani tangu nimepata tuzo ya kimataifa kutoka taasisi ya Institute of Hospitality ya Uingereza naona kama amebadilika sana!” Sammy aliwaza.

Hata hivyo, aliyafuta mawazo hayo haraka kichwani kwake, kwani alikuwa na uhakika kuwa Dk. Masanja hakuwa na shida yoyote ya kung’ang’ania kile cheo, ingawa naye alikuwa kaajiriwa hapo New Udzungwa Beach Resort lakini alikuwa amejitosheleza kwa vitu vingi.

Mara mbili alitaka kuacha kazi ili akasimamie biashara zake lakini kampuni ilimuomba na hata kumuongezea mshahara mara dufu ili asiache kazi.

Si hivyo tu, alikuwa anamiliki migahawa miwili ya kisasa, mmoja ukiwa jijini Dar es Salaam na mwingine jijini Mwanza, alikuwa na ranchi ya ng'ombe wa kisasa wasiopungua therathini, shamba kubwa la matunda na mazao mbalimbali eneo la Ruvu mkoani Pwani, na nyumba kadhaa za kisasa alizozipangisha katika majiji ya Dar es Salaam na Mwanza.

Mkewe pia alikuwa anamiliki maduka makubwa mawili ya vipodozi na nguo za kike, maarufu kama boutique, yalikuwa katika majiji ya Dar es Salaam na Mwanza, na alikuwa mbioni kufungua duka jingine jijini Arusha. Pia mara kwa mara alikuwa akisafiri nje ya nchi kwenda kununua bidhaa.

Sasa Sammy alijiuliza, kama haikuwa hofu ya kunyang’anywa cheo kulikuwa na tatizo gani kubwa? “I need to find out,” aliwaza na kuzidi kutweta.

Pamoja na uwepo wa kiyoyozi mle ofisini kilichotoa ubaridi mkali lakini alianza kutokwa jasho. Mara kikohozi kidogo kikamtoka, na nyuma yake wimbi la machozi lilikuja mbio. Alijaribu kuyazuia machozi yasimtoke bila mafanikio, aliyafuta kwa kutumia viganja vyake vya mikono.

“Boss, unaweza kuniambia kwa nini unanifanyia hivi?” hatimaye Sammy alimudu kuuliza huku akiwa amefadhaika sana.

“Umefanya jambo la kipumbavu sana lililonifedhehesha mno… sasa toka ofisini kwangu kabla sijasahau kuwa sisi ni marafiki!” Dk. Masanja alimwambia Sammy huku akimtazama kwa macho makali yaliyokuwa yakiwaka kwa ghadhabu.

Sammy alijikuta akihamaki sana, alitaka kusema neno lakini akashindwa kutokana na donge la hasira kumkaba kooni, na mara alishangaa kuona ukungu mwepesi ukianza kutanda mbele ya macho yake. Alianza kupumua kwa nguvu huku miguu yake ikianza kuishiwa nguvu…

_____

Hakujua ni muda gani alikuwa ameutumia akiwa kasimama ofisini kwa Dk. Masanja na hakuamini kama ni kweli mambo yale yalikuwa yamemtokea.

Itaendelea...

Cc the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater Bigjahman moneytalk marybaby nipo2 ram kisukari Smart911 Madame S carbamazepine Astelia culture gal Prisoner of hope Mine eyes kuku mweus Thad hearly Shunie moneytalk Tumosa Mine eyes Kudo swahiba92 ludist Toyota escudo Clkey macson3 boga la kiangazi LEGE Smart911 Richard irakunda skfull popie Krizy Beat hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Mlenge Kacheda mjasiliamali
 
Taxi - (6)

Hakujua ni muda gani alikuwa ameutumia akiwa kasimama ofisini kwa Dk. Masanja na hakuamini kama ni kweli mambo yale yalikuwa yamemtokea.

Alipozinduka kutoka kwenye lindi la mawazo alijiona yuko ndani ya choo cha jengo la ofisi katika ghorofa ya kwanza akiwa amesimama huku analia kilio cha kwikwi. Kilikuwa kilio cha dhati kabisa kilichotoka moyoni, ambacho aghalabu huisha chenyewe pindi uchungu unapopungua au kuisha kabisa.

Hakujua alitokaje mle ofisini kwa Dk. Masanja katika sehemu ya chini kabisa ya jengo na alipandaje ngazi hadi ghorofa ile ya kwanza ilipokuwa ofisi yake. Pia hakukumbuka vyema kama aliichukua ile barua ya kusimamishwa kazi aliyokuwa amepewa na Dk. Masanja au la.

Alijaribu kuitafuta kila sehemu, kuanzia kwenye mifuko yake ya suruali, mfuko wa shati na hata kwenye mifuko ya koti, ili kuona kama alikuwa nayo, lakini hakuiona. Alihisi kufedheheka sana.

Hakuwa na sababu ya kuendelea kusimama mle chooni, isipokuwa kuondoka ili akaitafute haki yake kunakostahili. Hakujua angeanzia wapi kutafuta haki dhidi ya Dk. Masanja, aliyeaminika sana na uongozi wa kampuni ile.

Kipindi chote cha miaka 10 ya kazi yake katika hoteli ya Udzungwa Beach Resort, Sammy alikuwa amefanya kazi yake kwa uaminifu mkubwa na hakuwahi kufikiria kama ingetokea siku angetoswa kwa namna ile bila sababu ya msingi, tena na watu aliowafanyia kazi na kwa uaminifu mkubwa!

Alikuwa akifanya kazi muda mwingi bila kupumzika ili kuhakikisha hoteli ya Udzungwa Beach Resort inaendelea kuwa hoteli bora kabisa katika Afrika Mashariki, na kupitia yeye hoteli ile imefanikiwa kuzoa tuzo kila mwaka, huku yeye akipata tuzo ya ubunifu na ufanyakazi bora zaidi ya mara mbili.

Na hata kulipotokea mtikisiko wa kiuchumi, Sammy alijitahidi kubuni mbinu mbalimbali za kuendelea kuwavutia wageni waliokuja nchini, kwa safari za kitalii, mapumziko na shughuli zingine, ndiyo maana mwezi mmoja tu uliokuwa umepita alipewa tuzo ya kimataifa kutoka taasisi ya Institute of Hospitality ya nchini Uingereza.

Alianza kuilaumu sana nafsi yake kwa kupoteza muda wake mwingi kuwatumikia watu wasiokuwa na shukrani. Alijiangalia vizuri kwenye kioo kilichokuwa ukutani juu ya sinki la kunawia mikono na kuiona michirizi ya machozi ilivyoacha alama ya mtiririko mashavuni kwake.

Please help me Lord,” (Mungu nisaidie) Sammy alisema huku akifuta machozi, alianza kuhisi kichwa chake kikizidiwa na uzito.

Alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku mwili wake ukitetemeka, alihisi kuanza kuchanganyikiwa.

Aaarrgggh! Damn you, Masanja…” Sammy alishindwa kujizuia, akajikuta akipiga kelele kwa hasira na kupiga teke kila alichokiona mbele yake. Muda ule alikuwa anahema kwa nguvu.

Ghafla mlango wa chooni ulipigwa kumbo kwa nguvu na kufunguka, vijana wawili waliokuwa na sura zenye wasiwasi waliingia na kusimama huku wakimtazama kwa mshangao.

“Vipi, Boss, kuna tatizo?” kijana mmoja alimwuliza Sammy huku akiwa na wasiwasi mkubwa.

I’m fine, James… usiwe na wasiwasi,” Sammy alimjibu yule kijana huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Una uhakika Boss?” aliuliza tena yule kijana akiendelea kumkodolea macho.

“James, nimesema I’m fine. Mnaweza kwenda ninahitaji kuwa peke yangu, I need to be alone,” Sammy alisema na kufungua bomba la maji. Wale vijana walishangaa sana, hata hivyo hawakuuliza tena bali waliondoka na kuufunga mlango.

Sammy alikinga mikono yake kwenye lile bomba la maji, akanawa uso wake na mengine kujimwagia kichwani, kisha alitoa leso yake akajifuta maji usoni huku akijiangalia vizuri kwenye kioo katika namna ya kuukagua uso wake kwa makini. Aliporidhika alitoka kwa nia ya kwenda ofisini kwake.

Alishangaa kumuona Ofisa Usalama wa hoteli ile kutoka kampuni ya ulinzi ya Spark K7 akiwa amesimama akilinda ofisi yake. Sammy alipotaka kuingia ndani ya ile ofisi yule ofisa usalama wa hoteli alimzuia huku akimkazia macho yake. Sammy alijikuta akitweta.

“Samahani, Boss, huruhusiwi kuingia humu ndani,” alisema yule ofisa usalama wa hoteli.

“Kwa nini unanizuia nisiingie? Inamaana hujui mimi ni nani? Don’t you know me?” Sammy alimuuliza yule ofisa usalama wa hoteli huku akiwa amemkazia macho kwa hasira.

“Kwa nini unanizuia nisiingie? Inamaana hujui mimi ni nani?” Sammy alimuuliza yule ofisa usalama wa hoteli huku akiwa amemkazia macho kwa hasira.

“Nafahamu wewe ni nani, Boss, lakini haya ni maagizo kutoka kwa Meneja Mkuu wa hoteli,” yule ofisa usalama wa hoteli alijibu na kumfanya Sammy azidi kunyong’onyea.

Okay, basi naomba uniruhusu niingie nichukue mkoba wangu, siwezi kulazimisha kuwepo katika ofisi ambayo sitakiwi,” Sammy alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Samahani Boss, huruhusiwi kabisa kuingia humu ndani, kama ni mkoba subiri hapo hapo nitakuletea,” yule ofisa usalama wa hoteli alisisitiza huku akifungua ule mlango na kuingia ndani akimwacha Sammy pale pale nje akiwa katika mshangao mkubwa.

Muda mfupi baadaye yule ofisa usalama wa hoteli alitoka akiwa amebeba ule mkoba mdogo aina ya Pad & Quill na kumkabidhi Sammy.

“Bosi, hakikisha kama vitu vyako vyote vimo kwenye mkoba,” alisema yule ofisa usalama wa hoteli akiwa amesimama pale pale alipokuwa amesimama mwanzo.

Sammy aliufungua na kutazama haraka haraka ndani ya ule mkoba kuona kama vitu vyake vilikuwa sawa, akashusha pumzi ndefu.

Muda huo wafanyakazi wawili watatu walitoka kwenye ofisi zao kushangaa na wengine walichungulia milangoni kushuhudia tukio lile, wote walijikuta wakipigwa na butwaa wasijue kilichokuwa kikiendelea, ingawa hakuna aliyethubutu kuuliza.

Sammy aliwatazama haraka haraka kisha akaanza kuondoka kutoka eneo lile, alitembea akiwa ameinamisha kichwa chake na kufungua ule mlango mkubwa wa kioo kisha alizifuata ngazi za jengo lile za kushuka chini, na kuanza kuzishuka taratibu, hata hivyo alionekana kutembea pasipo mpangilio.

Alipofika eneo la chini aliendelea kutembea pasipo mpangilio huku akitupa macho yake kuangalia huku na huko, alionekana kuchanganyikiwa sana. Jasho jingi lilikuwa linamtoka usoni na kumfanya kutoa leso yake laini na kujifuta paji la uso wake.

Itaendelea...
 
Taxi - (7)

Wakati akitembea alipishana na wahudumu wawili wa kike wa ile hoteli waliokuwa wakiwasindikiza wageni kwenye vyumba walivyopanga baada ya kufika hapo hotelini.

Wale wahudumu na wageni walimsalimia Sammy kwa bashasha lakini yeye hakuonekana kuwajali, alikuwa mbali sana kimawazo na aliwapita bila kusema neno lolote. Kutokana na kuchanganyikiwa, alikuwa akihisi kila aliyekutana naye ni kama alikuwa anamdhihaki.

Jasho jingi lilizidi kumtoka usoni na sehemu mbalimbali za mwili wake, ingawa kulikuwa na viyoyozi vikubwa vilivyokuwa vikisambaza hewa safi na baridi eneo lote.

Wale wahudumu na wageni waligeuka kumtazama Sammy kwa mshangao kisha walitazamana wao kwa wao katika hali ya kuulizana ingawa hakuna aliyekuwa na majibu.

Sammy alipita katika eneo la mapokezi na kugeuza shingo yake kuwatazama watu wachache waliokuwepo eneo lile, macho yake yalitua kwenye uso wa Rose aliyekuwa amesimama akimtazama Sammy kwa makini.

Katika mawazo yake, Sammy aliona kama vile Rose alikuwa akimwangalia kwa huzuni kubwa na wakati huo huo aliwaona wale watu wengine kama waliokuwa wakimdhihaki na kumcheka. Hali ile ilimfanya ahisi kuchanganyikiwa zaidi na kutaka kupiga kelele.

Alilivuka haraka eneo lile la mapokezi na kuufikia ule mlango mkubwa wa vioo uliojifungua wenyewe, akatoka nje na kuanza kushuka ngazi huku akitembea pasipo mpangilio kama aliyekuwa amekunywa pombe. Pale nje bado kulikuwa na mvua ya manyunyu mepesi.

Fred, yule askari wa ulinzi wa kampuni ya Spark K7 alimuona na kusemesha lakini Sammy hakuonekana kumsikia. Alianza kupiga hatua kuondoka eeneo lile lakini alihisi kizunguzungu na kusimama, akajiegemeza kwenye gari moja aina ya Landcruiser GX V8 la rangi nyeusi lililokuwa limeegeshwa mbele ya duka la kubadilishia fedha za kigeni.

Oh my God…” Sammy alisema kwa sauti ya chini na kushika kichwa chake huku akikunja sura na kufunga macho, kisha akakusanya nguvu na kuanza kutembea kuelekea kwenye lango kuu la kutokea magari la hoteli ile.

Alitembea akipita katika barabara ya lami katikati ya mazingira safi yenye ukijani wa nyasi fupi na maua mbalimbali hadi kwenye lango kuu la kisasa la kutokea hotelini hapo lililokuwa na maandishi makubwa ya “OUT”.

Kwenye lile lango kulikuwa na askari watatu wa ulinzi wa kampuni ya ulinzi ya Spark K7 waliokuwa na bunduki wakiwa makini kukagua magari yaliyotoka katika hoteli ile.

* * * * *

Gari la kifahari aina ya Range Rover Velar la rangi nyeupe lilikuwa linapita katika barabara pana na tulivu ya lami ya Ufukweni katika eneo la Oysterbay yenye kila aina ya ustaarabu ikipambwa na taa za barabarani, lilikatiza likiyapita majumba ya kifahari yaliyokuwa yamezungukwa na miti mirefu na kuta zenye usalama wa uhakika.

Eneo lile la ufukwe wa Oysterbay lilikuwa na makazi ya kisasa kabisa ya viongozi na lilikuwa kimya sana. Lile gari lilianza kupunguza mwendo na hatimaye likasimama kando ya barabara ile chini ya miti mikubwa na mirefu ya kivuli, takriban mita hamsini tu kutoka katika uzio wa Udzungwa Beach Resort.

Ndani ya lile gari kulikuwa na watu watatu waliokuwa kimya kabisa lakini wakiwa makini kama simba anayewinda pundamilia. Wa kwanza alikuwa dereva wa gari aliyeitwa Madjid Chege, alikuwa mtu mzima wa umri wa kati ya miaka 45 na 50, alikuwa mrefu na maji ya kunde.

Chege alikuwa amevaa miwani myeusi ya jua na alipenda kuivaa hata kipindi ambacho hakukuwa na jua, hakuwa mtu wa maneno mengi lakini alikuwa mcheshi, na muda huo alikuwa amevaa suruali nyeusi ya kitambaa, shati la samawati la mikono mirefu na tai nyeusi.

Kwenye siti ya mbele kushoto kwa dereva alikuwa ameketi kijana mmoja mrefu na mwenye umbo la kimazoezi, alikuwa na macho makali na mikono imara. Jina lake aliitwa Silas Polea lakini alipenda zaidi kuitwa Spoiler, na alikuwa na umri wa miaka 35.

Spoiler aliyezaliwa na kukulia nchini Kenya alikuwa na uwezo mkubwa katika mapigano kwani alipata mafunzo ya kujihami ya karate na judo, na alifikia ngazi ya mkanda mweusi (third degree black belt).

Pia alikuwa na uwezo mkubwa wa kutumia silaha mbalimbali katika mapigano ikiwemo kisu (ndiye aliyewahi kumpa mafunzo halisi juu ya matumizi ya kisu cha kurusha jambazi aliyeitwa Joram Mbezi maarufu kwa jina la Kisu kwenye mkasa wa Kizungumkuti), kwani alikuwa na uwezo wa kulenga mboni ya jicho, hata la ndege, na kisu kikatua pale pale.

Alikuwa amevaa suruali ya jeans ya rangi ya bluu, buti ngumu nyeusi za ngozi ya mamba, t-shirt nyekundu na jaketi la jeans la rangi ya bluu. Pia alivaa kofia nyekundu ya kapelo na miwani myeusi ya jua na alikuwa ameyakaza macho yake kuangalia kwenye lango la kutokea magari la hoteli ya Udzungwa Beach Resort.

Mtu wa tatu alikuwa mwanamume wa makamo aliyeitwa Hassan Oduya, alikuwa mtu mzima mwenye umri wa miaka 65, kichwa chake kilikuwa kimejaa mvi nyingi na alikuwa na ndevu nyingi nyeupe zilizokizunguka kidevu chake.

Mr. Oduya alikuwa mfanyabiashara mkubwa na mwanasiasa maarufu nchini aliyeishi eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Alikuwa mrefu kiasi na alikuwa amevaa suti ya pande tatu aina ya Brioni Vanquish ya rangi ya kijivu, iliyokuwa imemgharimu fedha nyingi sana, ambazo zingetosha kujenga nyumba ya maana Uswahilini. Pia alikuwa amevaa miwani ya macho na mkononi alivaa saa ya thamani kubwa aina ya Rolex Submariner.

Mr. Oduya alikuwa ameketi kwenye siti ya nyuma na alishika simu aina ya Samsung Galaxy Note 9 na muda mwingi alikuwa akiongea kwenye simu, na mdomoni alikuwa amebana mche wa sigara aina ya Parliament.

“…yes, sasa nipe taarifa nzuri, Doctor,” Mr. Oduya alisema akiwa mwenye shauku kubwa.

Everything is okay! Nimeifanya kazi kama tulivyokubaliana, mambo mengine yamebakia kwenu,” sauti ya upande wa pili ilisema na kuufanya uso wa Mr. Oduya uchanue kwa tabasamu la ushindi.

Well done, Doctor,” (Kazi nzuri, dokta) Mr. Oduya alisema kwa furaha huku akibetua kichwa chake.

“Wewe umefanya kwa sehemu yako, hiyo ni hatua ya kwanza, kuanzia kesho nataka tuingie katika hatua ya pili kama nilivyokueleza jana…” Mr. Oduya aliongeza huku tabasamu bashasha usoni kwake likiwa limekataa kabisa kwenda likizo. Kisha alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kukata simu.

Itaendelea...
 
Taxi - (8)

Muda ule ule walimuona Sammy akitoka kwenye lile lango kuu la kutokea magari la hoteli ya Udzungwa Beach Resort akionekana kama mtu aliyechanganyikiwa sana huku akitembea taratibu pasipo mpangilio.

Sammy alisimama pale nje ya uzio wa ile hoteli na kutazama huku na huko kama aliyekuwa akitafuta kitu, huenda alikuwa akitafuta usafiri wa kumfikisha alikotaka kwenda.

Mr. Oduya alimtazama Sammy kwa kitambo na kushusha pumzi za ndani kwa ndani kisha akaachia tabasamu huku akibetua kichwa chake katika namna ya kukubali jambo.

“Kijana anaonekana kachanganyikiwa hasa,” Mr. Oduya alisema huku akiachia kicheko hafifu.

“Sasa unaweza kushuka, hakikisha anaingiwa na hofu, ila usimuumize kwani tutamtumia baadaye,” Mr. Oduya alimwambia Spoiler.

Spoiler aliteremka mara moja kutoka ndani ya lile gari na kuanza kuvuta hatua zake taratibu akipita kando ya barabara upande aliokuwa Sammy, aliitoa simu yake akajifanya kuperuzi huku akiwa makini zaidi kumtazama Sammy.

“Mafuru atakuwa makini kukulinda,” Mr. Oduya alimwambia Spoiler na kuongeza, “Ukimalizana naye njoo haraka kule Kinondoni, tunahitaji kumuhoji yule mwandishi wa habari,” alisema na kumgusa Majid kwenye bega lake, “Okay, let’s go.

Majid alitii amri na kuondoa gari haraka kutoka eneo lile huku wakimwacha Spoiler akiendelea kumfuatilia Sammy aliyekuwa bado kasimama huku akionesha wasiwasi.

Muda ule ule Sammy alianza kupiga hatua zake taratibu akipita chini ya miti kukwepa manyunyu mepesi ya mvua na kuelekea kule alikokuwa anatokea Spoiler.

Aliliona lile gari la Mr. Oduya likielekea kufuata uelekeo wake lakini hakulitilia maanani, aliendelea kutembea taratibu na kupishana nalo huku akitupa macho yake kuwaangalia waliokuwemo ndani, na mara macho yake yakatua kwenye uso wa Mr. Oduya aliyekuwa ameketi kwenye siti ya nyuma. Mr. Oduya alimtazama Sammy na kuachia tabasamu pana.

Sammy aligeuza shingo yake kulisindikiza lile gari wakati likimpita na kutokomea mtaani huku akijaribu kujiuliza jambo kuhusu Mr. Oduya, hakujua kwa nini yule mzee alitabasamu baada ya kumuona. Alijiuliza lakini hakuweza kupata jibu.

Muda ule Spoiler alikuwa amesimama kando ya barabara akiwa ameshika simu yake huku akimtazama Sammy kwa makini wakati alipomkaribia. Kisha aliirudisha ile simu kwenye mfuko wa suruali yake na kuanza kumkabili Sammy.

Alimsogelea na kumzuia kwa mbele kisha akaegesha kiwiko chake cha mkono juu ya bega la Sammy huku akimkazia macho yaliyokuwa yanawaka kwa ghadhabu. Sammy alionekana kushangaa sana.

Alimtazama Spoiler kwa mashaka na kuuondoa ule mkono kwenye bega lake huku akionesha kutokufurahia kitendo kile. Wakabaki wametazamana kama majogoo yaliyotaka kupigana, hali ya taharuki ilionekana kujitokeza katika eneo lile ikiashiria kuzuka kwa tafrani wakati wowote.

Sammy alihisi damu yake ikichemka mwilini kwa hamu ya kumfanyia mazoezi ya karate mpuuzi yule lakini alisita mara moja baada ya kuona kile ambacho hakutarajia kukiona katika macho ya Spoiler. Dalili zote za ukatili, dharau, unyama na dhihaka ya hali ya juu. Akaduwaa.

“Sikiliza we boya, mimi ni mtu katili sana, hasa pale ambapo mtu ninayemuuliza swali akajifanya hamnazo, kwa hiyo usinilazimishe kukuumiza. Nitakuuliza maswali na ninaomba unieleze ukweli wa kile unachokijua,” Spoiler alimwambia Sammy huku akiendelea kumkazia macho.

“Kwani unataka nini kutoka kwangu?” Sammy alimuuliza Spoiler huku akimtazama kwa wasiwasi.

“Najua unafahamu jambo kuhusu uhusiano wa bosi wako Dk. Masanja na Mr. Oduya, je, umeshamweleza yeyote?” Spoiler alimuuliza Sammy huku akimtazama moja kwa moja machoni.

“Sifahamu chochote, kwani vipi?” Sammy naye aliuliza huku akimtazama Spoiler moja kwa moja machoni bila kupepesa macho yake.

“Ninajua kuwa jana usiku ulisikia mambo mengi yaliyokuwa yanazungumzwa ofisini kwa bosi wako… kama hujamweleza mtu ulichosikia basi usijaribu kufungua bakuli lako, vinginevyo nitaku…” Spoiler alisema huku akinyoosha vidole vyake vyote vya mkono wa kulia kisha akapitisha katika shingo yake kuonesha ishara ya kuchinja.

“Tafadhali usijaribu kunitisha,” Sammy alisema huku akihisi donge la hasira likimkaba kooni.

Okay! Kumbe wewe ni jeuri! Nikwambie kitu kimoja… very soon nitapafahamu nyumbani kwako, nitamfahamu mkeo na hata shule wanayosoma watoto wako, kama unao… hivyo usinilazimishe kufanya kitu utakachokuja kukijutia baadaye,” Spoiler alimwambia Sammy kwa ghadhabu huku akimkwida shati na kumsogeza karibu na uso wake.

Don’t touch my family or I’ll kill you,” (Usijaribu kuigusa familia yangu vinginevyo nitakuua) Sammy alisema huku akitetemeka kwa hasira na kujitoa kwa nguvu kutoka kwenye mikono ya Spoiler.

Alirudi nyuma hatua moja huku akihisi donge la hasira likizidi kumkaba kooni na kumfanya apumue kwa nguvu, hakutaka kabisa kutishiwa maisha au kunyanywa na yule mkora na alikuwa tayari kwa lolote.

Walibaki wakitazamama kwa kitambo fulani huku Sammy akijaribu kuyatafakari maneno ya Spoiler yaliyomkumbusha tukio fulani alilolishuhudia usiku wa kuamkia siku ile. Sasa alijua kwa nini alikuwa amesimamishwa kazi.

Wakati akitafakari alishtukia akikwidwa tena na mikono yenye nguvu ya Spoiler kwa vidole vyake vikubwa na kumbana huku akimsogeza karibu yake, wakabaki wanaangaliana uso kwa uso kwa ghadhabu, kila mmoja alikuwa amepandwa na hasira.

Sammy alijaribu kujitoa katika mkono wa Spoiler lakini ilikuwa kama kujaribu kujitoa katika pingu, kwani vidole vya Spoiler vilizidi kung’ang’ania katika shati lake na kusababisha vifungo viwili viachie.

“Kama unadhani nakutisha basi jaribu kuropoka, nitayafanya maisha yako kuwa ya huzuni sana,” Spoiler alisema na kumsukuma Sammy.

Sammy alipepesuka na kuteleza, akaanguka chini na kupata michubuko midogo kwenye kiwiko cha mkono wake wa kushoto, alihisi kufedheheshwa sana. Aliinuka haraka akiwa ameghadhabika sana na kujiweka tayari kwa lolote.

Kuona hivyo Spoiler alikunja ngumi ya mkono wake wa kulia na kutengeneza alama ya dole gumba, kisha akapeleka lile dole gumba na kuminya pua yake kwa dharau huku akikunja sura yake kana kwamba alikuwa amenusa harufu mbaya.

Alifunua jaketi lake ili kumuonesha kitu Sammy, na hapo macho ya Sammy yakatua kwenye kisu kikubwa cha springi kilichokuwa kimewekwa ndani ya ala na kutuna kiunoni kwa Spoiler.

Sammy alijikuta akisisimkwa mwili wake na damu ikaanza kumchemka na kukimbia kwenye mishipa yake ya damu, vinyweleo mwilini na nywele kichwani zilimsisimka kwa hasira. Hali ile ilisababisha mapigo ya moyo yaende mbio huku jasho jepesi lianze kumtoka sehemu mbalimbali za mwili wake!

Spoiler alitaka kukichomoa kile kisu lakini alisita na kugeuza shingo yake kuwatazama watu walioanza kusogea eneo lile huku wakishangaa. Miongoni mwao alikuwemo askari mmoja wa ulinzi wa kampuni ya Spark K7 aliyekuwa ameshika bunduki akilinda eneo la uzio wa hoteli.

Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusisimua...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom