Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Hahahaaaa, mkuu the_legend moja ya sifa kubwa za mwandishi yeyote mzuri ni kufanya utafiti kabla hajaandika kuhusu kitu chochote, kama nilivyowahi kueleza mwandishi anatakiwa kuiona hadithi yake kama vile anaona sinema, asikie na sauti za wahusika, jambo linaloitwa visualization”.

Ngoja nikudokeze kidogo, zipo sifa kubwa tisa anazotakiwa kuwa nazo mwandishi, na kama utaweza kufit kwenye sifa hizi lazima utakuwa mwandishi mzuri sana unayeandika stori zinazogusa miyo ya watu:

1. Organizational skill: mwandishi mzuri wa hadithi anapaswa kuwa na uwezo mkubwa wa kuandaa na kupangilia taarifa zake kuhusiana na kisa anachokusudia kukiandika.

2. Analytical ability: mwandishi mzuri wa hadithi lazima awe na uwezo wa kuchambua taarifa na kujua kama zitagusa mahitaji halisi ya wasomaji wake, na awe na uwezo wa kutofautisha mambo muhimu na yasiyo muhimu kabla ya kuyaweka kwenye kurasa.

3. Interest in diverse topics: hadithi nzuri inahitaji kufanyiwa utafiti wa kina. Mwandishi mzuri anapaswa kufanya utafiti kwa kila jambo analoliandikia bila kujali ukubwa au udogo wa jambo lenyewe.

4. Empathy for your audience: mwandishi lazima awe na uwezo wa kuzama ndani ya mitazamo ya wasomaji wake na kuyaelewa mambo wanayoyapenda, mitindo yao, tabia zao, matamanio yao n.k. ili kuhakikisha kuwa wanashiriki kwenye hadithi yake na kuwa sehemu ya hadithi kwa kuamini kuwa ni sehemu ya maisha yao, pia awe na uwezo wa kuwafanya wasichoke kuifuatilia.

5. Writing skills: mwandishi anapaswa kuwa na uwezo wa kuandika kwa ufasaha kwa lugha iliyobebwa na msingi imara wenye kumvutia yeyote atakayesoma, lugha ambayo inapaswa kuwa ya uwazi na lazima awe na uwezo mzuri katika matumizi ya sarufi.

6. Ability to think visually: mwandishi anapaswa kuwa na uwezo wa kuyabeba mawazo yake sambamba na picha (visualization), awe na uwezo wa kuiona taswira kupitia maandishi yake na awaoneshe wasomaji wake kile kinachoendelea kwenye hadithi yake.

7. Creativity: Ubunifu ni jambo muhimu sana kwa mwandishi, ubunifu unahitajika sana kwa ajili ya kuweza kuandika hadithi nzuri itakayogusa mioyo na hisia za wasomaji. Hata hivyo, huwezi kuwa mbunifu kama husomi kazi za waandishi wengine.

8. Presentation and selling skills: mwandishi lazima awe na uwezo mkubwa wa kuwasilisha mawazo yake kwa ufanisi na kuiuza kazi yake kwa wateja.

9. Ability to work on a team: kiutendaji wakati mwingine mwandishi hujikuta akilazimika kufanya kazi na watu wengine wenye mahitaji na mitazamo tofauti, hivyo, anapaswa awe na uwezo wa kufanya kazi kwenye kundi…

Nimeona nitoe somo kidogo kwa faida ya wengine. sasa tuendelee na KIZUNGUMKUTI...
Dah, hii akili kubwa aisee!
 
Mwisho wa safari hii ndefu iliyojaa "KIZUNGUMKUTI" ndiyo mwanzo wa safari nyingine itakayotufanya tujiulize, mambo haya "HADI LINI!" Usikose kufuatilia stori hii...
Dah, kweli hii ilikuwa safari iliyojaa kizungumkuti! Hongera sana Bishop Hiluka hakika Tanzania imebarikiwa kuwa na watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri!
 
Bishop Hiluka, ahsante Sana kwa simulizi nzuri na yakusisimua sana.Nimeburudika,nimeelimika halikadhalika nimejifunza mambo mengi mno kama uaminifu kazini, usalama,kuwa makini na kila mtu haijalishi ni nani na ana nafasi gani au kitengo gani ofisini au katika maisha ya kilasiku.

Pia nimeburudika kwa tafsiri fasaha ya lugha ya kingereza pamoja na maneno mazuri ya kuvutia ya lugha fasaha katika kila lugha ulizozitumia.

Mpangilio makini wa simulizi pamoja na ufundi sanaa wa kunyumbua mitaa kwa kuitaja majina yake pia kuzielezea barabara na kukumbuka hata vitu vidogovidogo ambavyo baadhi ya waandishi huvisahau,
mfano.'...simu aliyopigiwa kisu na Carlos katika simu ya jacky ambayo ilikuwa imeunganishwa na programu ya ulinzi' na jinsi namba hiyo ilivyofatiliwa na mwisho kugundulika ni namba ya jmbazi(KISU).

Hujakosea kwani wahusika wameuvaa vema uhusika wao na nafasi zao wamezitendea haki kikamilifu ila sikufurahishwa na kifo cha mapema mno cha Carlos, alikufa pasipo kutumia hata noti moja walizopora.

Mambo mazuri ni mengi kiasikwamba mengine hayasemeki hapa...ila unajua kumpamba mwanamke isivyokawaida kwakweli,Jacky aliitumia papuchi yake vizuri hadi raha.....day
Ila big up sana mwandishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunashukuru sana mkuu..hadithi ilikuwa ni ya kizungumkuti kwelikweli..ila napenda kutoa tu angalizo efficiency ya polisi ilikuwa kali sana..na sisi wananchi tungependa polisi wetu wawe kama hivi..lkn hawa wa kubambikiza kesi,rushwa,na upendeleo wa kivyama..kamwe hawatafikia level hii kwenye issue za kipelelezi!
 
Kizungumkuti!

Na Bishop Hiluka

“Hii ni trela tu, picha kamili keshokutwa! Hakyamungu keshokutwa hakai mtu hapa… mi naapa! Nitakunywa na nitatembea uchi ukumbi mzima kama mademu wakinimaindi poa tu, au vipi kichaa wangu?” Kabwe alipiga kelele kilevi, wakati huo huo Liston alikuwa analazimisha kumshika matiti dada mmoja aliyepita karibu yake…


Fuatilia stori hii hadi mwisho ya kusisimua kuyajua yote yanayoleta kizungumkuti...

KATIKATI ya jiji la Dar es Salaam hali ya hewa ilikuwa ya joto sana kama kawaida, hata katika majira yale ya saa tano za asubuhi. Asubuhi ile pilika pilika za watu zilikuwa zimeshamiri katikati ya jiji hilo kubwa zaidi Tanzania, na hivyo kulifanya kuchangamka sana kama ilivyokuwa kawaida yake.

Katika eneo la Mnazi Mmoja, barabara ya Lumumba kulionekana msululu mrefu wa magari, zikiwemo daladala zilizokuwa zikizunguka kutokea mtaa wa Uhuru katika kituo cha daladala cha Mnazi Mmoja na kupita barabara ya Bibi Titi kabla hazijaingia katika mtaa wa Mkunguni na kisha kutokea barabara ya Lumumba.

Katika barabara ile ya Lumumba, gari dogo la kifahari aina ya BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati lililotokea katika barabara ya Morogoro kwa mwendo wa taratibu na kujiunga katika msululu ule, kisha lilichepuka na kwenda kusimama chini ya miti ya kivuli iliyokuwa imepandwa kando ya ile barabara.

Hata hivyo, dereva wa gari lile alionekana kutoridhika na eneo lile, akaanza kutafuta sehemu nzuri zaidi na baadaye alikwenda kuliegesha gari lake kwenye eneo lililokuwa na magari mengine mawili matatu yaliyokuwa yameegeshwa pale, na vijana kadhaa walionekana wakiosha magari.

Vijana wawili waosha magari walimfuata haraka yule dereva wa lile gari na kuonekana kumzonga, kila mmoja alionekana akitaka apewe tenda ya kuosha lile gari lakini yule dereva hakuonekana kuwajali. Alibaki ametulia kimya akiusikilizia muungurumo laini wa lile gari kwa kitambo kirefu.

Ndani ya gari lile kulikuwa na watu wawili tu, mwanamume mmoja ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha lile gari na mwanadada mrembo sana ambaye alikuwa ameketi pembeni yake kwenye siti ya abiria.

Yule mwanamume alikadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka arobaini na arobaini na tano. Alikuwa mrefu wa futi sita na ushee, mweusi na shababi kwelikweli aliyekuwa na mwenye mwili uliojengeka kwa misuli.

Macho yake yalikuwa makali na alikuwa amevaa kofia ya rangi ya bluu aina ya kapelo, t-shirt ya pundamilia iliyokuwa na miraba ya bluu na myeupe aina ya form six na suruali ya jeans ya rangi ya bluu. Miguuni alikuwa amevaa buti ngumu za ngozi zilizokuwa na rangi nyeusi.

Mwanamume yule aliitwa Carlos Mwamba na aliendelea kutulia kwenye siti yake nyuma ya usukani akiwa ameibana njiti moja ya kiberiti kwenye pembe ya mdomo wake, huku akiendelea kuusikilizia muungurumo laini wa lile gari.

Kushoto kwa Carlos Mwamba, kwenye ile siti ya mbele ya abiria yule mrembo aliyekuwa ameketi aliitwa Jackline Mgaya na alikuwa mke wa ndoa wa Carlos, wakiwa wameoana takriban miaka mwili iliyokuwa imepita.

Jackline au kama alivyopenda kujulikana kwa kifupi kwa jina la Jacky alikuwa na umri usiozidi miaka therathini, alikuwa mrefu na mweupe mwenye haiba nzuri ya kuvutia sana.

Alikuwa na nywele nyeusi za kibantu alizokuwa amezikata vizuri na kubaki ndogo ndogo na hivyo kumfanya aonekane mzuri wa asili. Alikuwa na sura yake ya duara na macho makubwa ya kike na legevu yaliyokuwa yamezungukwa na kope ndefu na nyeusi.

Pua yake ilikuwa ndogo na iliyochongoka mfano wa pua ya kihabeshi na mdomo yake ilikuwa laini yenye maki na kingo pana kiasi zilizokuwa zimekolezwa kwa lipstick ya rangi ya chocolate pamoja na vishimo vidogo mashavuni mwake vilimfanya azidi kuonekana mrembo zaidi.

Jacky alikuwa na masikio madogo yasiyochusha aliyokuwa ameyatoga na kuyavalisha hereni kubwa za kitamaduni zilizokuwa na umbo la mviringo. Alikuwa amevaa blauzi nyepesi ya arangi ya pinki iliyoyaficha vyema matiti yake imara yenye ukubwa wa wastani yaliyokuwa na chuchu nyeusi imara zilizosimama kikamilifu ndani ya blauzi ile.

Shingoni alikuwa kavaa mkufu mwembamba wa dhahabu uliokuwa umeizunguka ile shingo nyembamba na kidani cha dhahabu kilichokuwa na herufi ya “J” kilikuwa kimepotelea katikati ya uchochoro mdogo wa yale matiti.

Kwenye mkono wake wa kushoto alikuwa amevaa bangili kadhaa za pembe na vidole vyake viwili vya mkono huo alikuwa amevaa pete ndogo za madini ghali ya tanzanite na green tourmaline.

Mkono wake wa kulia alivaa saa ndogo ghali na nzuri ya kike aina ya Cartier La Dona, ambayo bei yake ilikuwa si haba kama angeamua kuibadili kwa pesa za madafu, kwani ilikuwa imemgharimu kiasi cha dola za Marekani 137,000.

Cartier La Dona Watch ilikuwa ni saa ghali sana iliyotengenezwa kwa madini ya dhahabu nyeupe ya Karati 18 ikiwa na kesi imara iliyokuwa na milimita 27 kwa 29 na mkanda wake pia ulikuwa umetengenezwa kwa dhahabu nyeupe, ikiwa na gerentii ya miaka hamsini.

Alikuwa ameinunua nchini Switzerland walipokwenda kwenye fungate muda mfupi tu baada ya ndoa yao iliyoacha gumzo jijini Arusha na kwenye viunga vyake.

Gari ikiwa bado inaunguruma taratibu Jacky alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kutazama nje kwa kitambo fulani huku macho yake yakielekea moja kwa moja kwenye jengo la ghorofa la Benki ya Biashara.

Alilitazama lile jengo kwa makini akionekana kama aliyekuwa akijiuliza jambo kuhusiana na lile jengo, kisha aliyashusha macho yake kuutazama mkoba wake mzuri wa kike wa rangi ya pinki uliokuwa umelala juu ya mapaja yake mazuri.

Aliufungua ule mkoba na kutoa humo mkebe mdogo wa duara wa rangi nyekundu kisha aliinua macho yake kujitazama kwa kitambo kifupi kwenye kioo cha lile gari cha katikati kinachotumika kuangalia nyuma huku akigeuza geuza uso wake pembe zote.

Alikunja uso wake huku akiminya midomo yake mizuri yenye maki, na hapo mashavu yake yakapiga misingi, pembe za midomo yake zikafinya, akashusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akigeuka kumtazama Carlos aliyekuwa ametulia tuli kama maji mtungini na kuachia tabasamu bashasha.

Carlos aliendelea kutulia pale nyuma ya usukani akionekana kuwaza mbali sana, alimtupia jicho Jacky mara moja tu, kisha akayahamisha macho yake na kutazama kwenye lile jengo la Benki ya Biashara huku sura yake ikiwa haioneshi tashwishwi yoyote.

Jacky alimtazama Carlos kwa makini kisha akaufungua ule mkebe akatoa vipodozi na kuanza kujiremba akiongezea urembo kwenye sura yake huku akijitazama kwenye kile kioo cha gari cha katikati kinachoonesha nyuma.

Itaendelea...

Cc the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
Pamoja sana, nimeianza sasa
 
taratibu naanza nayo hii, hahaaa jamaa bwana.its insanely crazy yaan story zako huwa zinabadilika hadi raha.

nafikiri utakuwa mtazamaji mzuri wa movies za marvel studio,maana wale ndo mabingwa wakubadirisha uhusika wa characters wao
 
taratibu naanza nayo hii, hahaaa jamaa bwana.its insanely crazy yaan story zako huwa zinabadilika hadi raha.

nafikiri utakuwa mtazamaji mzuri wa movies za marvel studio,maana wale ndo mabingwa wakubadirisha uhusika wa characters wao
Inasemwa kuwa kwa asili kila binadamu ni mtunzi lakini ili uwe mtunzi/mwandishi mzuri unahitaji kuwa na mambo kadhaa kama: kuijua vizuri lugha (language), sarufi (grammar), msukumo wa ndani (inspiration) na ubunifu (creativity). Hata hivyo huwezi kuwa na ubunifu kama husomi au kufuatilia kazi za wengine ambazo zitakufanya utengeneze njia yako...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom