Stori ya binti: Usikate tamaa kwani Mungu hakati tamaa katika kukutetea

Emmanuel180

JF-Expert Member
Dec 17, 2019
342
626
Binti mmoja alikuwa akiendesha gari akiwa na baba yake. Wakiwa njiani ghafla mvua kubwa ikaanza kunyesha na kuleta tufani, yule binti akamuuliza baba yake, "Nifanyeje?" Baba yake akamwambia "endelea kuendesha"

Magari yakaanza kusimama na kuegesha pembeni kwa kuhofia tufani ambayo ilikuwa kubwa mno. "Nifanyeje?" Binti akamuuliza baba yake "Endelea kuendesha," baba yake akajibu.

Mbele yake tena akaona malori makubwa kabisa yakiegesha pembeni. Akamwambia baba yake, "Inabidi nisimame, angalia hata magari makubwa yanaegesha pembeni na sioni vizuri mbele. Hali ni mbaya sana!" Baba yake akamwambia, "Usikate tamaa, wewe endelea kuendesha!"

Tufani sasa ilizidi, lakini yule binti hakusimama na mara akaanza kuona japo kwa shida kidogo mbele yake. Baada ya maili kadhaa akajikuta yuko kwenye ardhi kavu ambako hakukuwa na mvua, na jua lilikuwa linaangaza. Baba yake akamwambia, "Sasa unaweza kusimama na toka nje." Binti akauliza "Kwanini sasa?"

Baba yake akamwambia "Ukitoka nje, tazama nyuma ili kuangalia watu waliokata tamaa na bado wako katikati ya tufani, kwa sababu hukukata tamaa tufani yako imekwisha sasa." Huu ni ushuhuda wa kila mmoja wetu ambaye anapitia kwenye "tufani na dhoruba nyingi za dunia." Siyo kwa sababu kila mmoja, pamoja na wenye nguvu, wanakata tamaa haimaanishi hata wewe pia ukate tamaa. Kama utaendelea kupambana na kusonga mbele dhoruba yako itakwisha.

Mweleze mtu yeyote anayepitia kwenye magumu. Mwambie: "Asikate tamaa, maana MUNGU hakati tamaa katika kukutetea. Yeye hashindwi, hasinzii wala halali mpaka utakapopata haki yako."

Tuisikilize Sauti ya Mungu nasi tutayavuka majaribu japo yawe magumu kiasi gani. Kuna wakati CHANGAMOTO zinakuja ili ZIKUPIME kama uko “serious” na lengo ulilojiwekea. Duniani wanaoruhusiwa kufanikiwa ni wale ambao wameamua kuwa “serious” na wanachokitafuta.

Dunia ikiona Ukipewa changamoto kidogo tu UNAKIMBIA, UNAACHA ama UNAANZA kulalamika. Hapo unaimbia kuwa hauko tayari KUFANIKIWA katika unachotafuta na hauko “serious” kabisaaa. Kwanini Dunia iache kumsapoti aliye “serious” kuliko wewe? Itahakikisha fursa zinazidi kukukimbia na milango inafungwa kabisa ukiionyesha hauko “serious”

View attachment 2123024View attachment 2123025
 
Swali:
Mfano nipo Mlima Kitonga halafu mbele kuna tufani/dhoruba na sioni kitu mbele, je niendelee kuendesha gari kuelekea mbele bila kukata tamaa au nipaki gari pembeni kwanza?

N.B: Somo zuri sana.
..
.
 
Kuna nyakati haya maneno ni faraja na nyakati ni huzuni

Inauma lakini pamoja na yooote maisha lazima yandelee
 
Back
Top Bottom