Store or Duka la vinywaji vikali...sprits | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Store or Duka la vinywaji vikali...sprits

Discussion in 'Matangazo madogo' started by FirstLady1, Mar 9, 2012.

 1. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 180
  Wadau salama !
  Naombeni mawazo yenu ya kina kabla sijaamua kujikita kwenye hii business
  Je ni mtaji kiasi gani unaweza kunitosha kufungua duka au store ya vinywaji Kwa jiji la DSM au Mwanza ..
  Vinywaji kama:-
  Whisky
  Wine..
  Nk ..
  Nk..
  Naomba pia muongozo kwani sijawahi fanya business hii ila wazo limenijia na nafikilia kuifanya.
  Naomba tuwezeshane kimawazo kwa wale mliona uzoefu wa mabusiness.
  **Natanguliza shukrani **
  FL1
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,981
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Fungua Bar tuwe tunakuja kunywa, mi niweke kaunta
   
 3. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,496
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Inahitaji mtaji mzito kidogo . Kama ni duka la saizi ya kati sio chini ya 100m .
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 180
  hahaha Fidel80 am serious bana ,Bar mie siiwezi kukimbizana na wahudumu
  Nipe mawazo najua utakuwa mteja wangu mkubwa ,,,Huduma mpaka mlangoni
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,981
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Huo mtaji si bora afungue Bar tu
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 180
  Bucho bana Misri haikujengwa siku moja hebu punguza na fanya calculation zako upya
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kwa mimi binafsi nilishindwa kuendesha duka la Wines &Spirits kutokana na kuwa ni mnywaji mno, nikaishia kulifilisi flat kabisa! KWAHIYO SITOONGEA NENO!

  Lakini ukiwa na nia ya kufungua duka la aina hiyo kwanza ujiridhishe sana na sehemu husika!
  Duka la Wines and Spirits linatakiwe liwe strong sana, lakini liwe na system ya surveilance maana mtu akichukua katoni moja ya eg Barcadi au Amarula, then ana uhakika kula siku kadha.
  Ni njema kama litakuwa mjini, au eneo lenye constant patrols za wanausalama, hii ni kutokana na Sales zake kuwa za amounts kubwakubwa, na ni rahisi sana kuingiliwa na wajasiriamali wenye mtaji AMBAO NI NGUVU YAO WENYEWE!
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,981
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mi ukiniweka meneja kazi itafanyika kwa ufanisi alafu Asprin anakuwa jikoni
  Hapo inategemea na mtaji wako unaweza anza kidogo kidogo huku ukiendelea kuongeza mtaji.
  Unaweza anza na creti 200 za bia ili wateja wasikose biya na unaweka mavinywaji yanayo nyweka sana kama mdogo ake safari, mjomba ake safari, binamu yake safari bila kusahau viloba vya kutosha kwa bei ya jumla hayo maBallantines mdogo mdogo
   
 9. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,496
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  huu ndo ukweli FL . Huwezi kuamini lakini chunguza utakuja kuniambia . Pombe sio chai .
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 180
  PJ mmh
  Kwa hiyo ulikuwa unaingia dukani unafungua Whisky moja unakandamiza ,huku ukiamini utailipia pale ukiwa na hela
  ikawa safari moja uanzisha nyingine mpaka duka letu ukalifilisi.
  Asante sana kwa mchango wako na ushauri nimepata kitu.
  Ne je ni kweli mpaka niwe na mtaji kuanzia 100m?
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,981
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Umenikumbusha si ulitaka chai chai kwa nini ulalamike unaunguaaaaa
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 180
  Fidel80 huna nia njema
  Meneja Fidel80
  Asprin Jikoni
  Bigirita...Kuhakikisha stock haikosekani
  TF...???
  Hapa nitafunga bar
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 21,271
  Likes Received: 3,946
  Trophy Points: 280
  MPWA UNA MAMBO......PICHA YA JK MPAKA KAUNTA....UKO SERIOUS


  [​IMG]
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu FL1,
  Ona mfano wa duka la vinywaji vikali!

  Ushauri wa Bure:
  Jaza aina tofauti za viroba kwa wingi sana, maana ndizo pombe kali za Wanywaji wa hali ya kati na chini!... ha ha haa!
  Kuhusiana na mtaji wa 100M, si lazima...wekeza hela kwenye uimara wa duka kwa kuanzia, mtaji waweza weka hata nusu ya hiyo fedha(lakini isipungue).

  inside_shop.jpg
   
 15. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,609
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Kuna kipindi nilikuwa nina mpango wa kufanya hii biashara hasa kuagiza spirits kutoka Europe na sehemu nyingine niliposhauriwa kuna feki nyingi sikuendelea tena lakini bado nina amini ni biashara nzuri sana kwa sababu ya wingi wa wanywaji.

  Mtazamo wangu kama hauingizi kutoka nje ni vizuri ukaanza na mtaji mdogo(chini ya 100m) ukailewa hiyo biashara kwanza
   
 16. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  POMBE SHOP ni wazo zuri sana mkuu, lakini pia lazima uangalie mazingira unayoweka wateja wako wakubwa ni wapi,naamini unataka kuuza jumla kwa wenye Bar na wauzaji wengine wa rejareja. Nakushauri ufanye research ya soko lako kwanza, vinginevyo utawekeza fedha nyingi kwenye bidhaa isiyo na mlaji.
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 180
  asante sana kwa ushauri amoeba
  nimekuelewa nitaufanyia kazi
   
 18. L

  LAT JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  FirstLady

  pia hii wanaita Liquor Shop au Bottle store, ukiweza kupata space kubwa unaweza ukawa na coldroom au Beer Cellar (walk in display cold freezers) ukaweka vinywaji vya aina zote vikiwa baridi especially beers, ukauza vinywaji hivi kwa wingi sana, wenye sherehe na shughuli mbali mbali watakimbilia kwako kwani utauza wholesale na vinywaji vikiwa baridi, hii style niliionaSouth Africa,

  wazo ni zuri ukiweka ubunifu ikawa na uniqueness, kwa nje unaweza weka jiko zuri na mchoma nyama na kuku kama take away ili kuweza ku attract biashara

  beer cave.jpg
   
 19. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  fungua mwanza pale mjni italipa vizuri dar biashara itakuwa ngumu, usiende kufungua makoroboi, mahina weka duka sehemu iliyo pembezoni mwa barabara kuu c'se wateja wako wengi watakuwa ni wale wenye usafiri binafsi. Na pia kuhusu mtaji si lazima uwe wa mamilioni 40 unaweza kuwa na hata chini ya 15m.

  nakushauri kwenye hilo duka uweke na wine za hapa nyumbani ndio zinapendwa sasa hivi, kuna vikundi vya wajasiliamali wanatengeneza natural wine nzuri sana with pure organic grapes na hazina makemikali na bei zao ni rahisi. Binafsi huwa nanunua wine za nyumbani ni nzuri sana ukilinganisha na za nje. Ukishaonana nao unaweza kukubaliana nao wakutengenezee wine zenye specifications unazozitaka wewe, hapa utafanikiwa sana. Kuhusu vikundi vya wasindikaji unaweza kuwapata dodoma, tabora. Hii pia itakusaidia kumatch na budget yako

  Hii biashara ni ngumu kwa kiasi fulani ukizingatia hali ya kifedha ya watanzania wengi, usiweke ma whisk ya 600,000/= yataozea dukani. Jaribu kuweka bidhaa ambazo ni affordable kwa wengi, kwa mwanza am sure italipa c'se soko bado halijavamiwa
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 180
  Asante sana kwa mawazo mazuri kuna mtu kasema 100m ndo inaweza nitosha nafanyia kazi mawazo yako asante
   
Loading...