STOP BARRICK GOLD CAMPAIGN - Wabunge Simameni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

STOP BARRICK GOLD CAMPAIGN - Wabunge Simameni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Jul 16, 2008.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  KUTOKANA HALI HALISI YA SEKTA YA MADINI HAPA NCHINI ,PAMOJA NA KUWEPO KWA RIPOTI YA BOMANI AMBAYO BUNGE LINATARAIJIWA KUIJADILI KATIKA KIPINDI HIKI CHA BAJETI.

  kUNA TAARIFA ZA KUAMINIKA KUWA BALOZI WA CANADA PAMOJA NA UJUMBE MZITO WAPO BUNGENI DODOMA TANGU WIKI ILIYOPITA NAKIKUTANA NA WABUNGE MBALIMBALI NA KUFANYA LOBBYING HUKU HOJA ZAKE KUU ZIKIWA NI KUWASHAWISHI WABUNGE WASIPITISHE MAPENDEKEZO YA KAMATI YA BOMANI KAMA YALIVYO KWANI YATAWAFANYA WAWEKEZAJI KUKIMBIA NCHI.

  BALOZI HUYO PAMOJA NA UJUMBE WAKE WAMEKUWA WAKIWASHAWISHI WABUNGE KUWA MAPENDEKEZO HAYO YAPELEKWE KWA WATAALAMU WA BENKI YA DUNIA KWANZA KABLA YA KUPITISHWA NA BUNGE.

  KWA KUWA HUU NI MKAKATI WA KUWASAIDIA WATU NA MAKAMPUNI YA BARRICK NAWASHAURI WANA JF KUHAKIKISHA KUWA TUNAWATAKA WABUNGE WETU WASIKUBALIANE NA USHAWISHI HUO NA KILA MMOJA WETU AHAKIKISHE KUWA ANAWASILIANA NA MBUNGE WAKE ILI KUUKWAMISHA MPANGO HUU AMBAO NI WA KUENDELEA KUCHUKLUA RASILIMALI ZA NCHI YETU.

  NITAWALETEA TAARIFA ZA KINA ZAIDI KUWA KESHO ATAKUTANA NA WABUNGE GANI KWANI AMEKUWA AKIWAITA WACHACHE WACHACHE KUANZIA WA UPINZANI NA HATA WALE WA CCM.

  THIS IS A CRY FOR HELP.... HELP TANZANIA AND OUR RESOURCES.....
   
  Last edited by a moderator: Jul 17, 2008
 2. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Leo amekutana na wabunge wengi sana na amekuwa na vikao nao vingi sana sasa kama balozi mwenyewe ndio anaendesha kampeni hizi kuna haja ya sisi watanzania kuhakikisha kuwa tunakuwa mstari wa mbele kulinda rasilimali zetu.

  Tupaze sauti zetu .
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Mmeyaona sasa?
  Haya Pambaneni na wananchi WAANDAMANE!
  NO MORE SPECIAL INTERESTS LOBBYING..WE NEED THE PEOPLE'S LOBBYING!
   
 4. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Piga simu kwa Tundu Lissu na shirika lao la LEAT, Piga simu kwa Shivji na shirika la la Haki Ardhi, Piga simu kwa Kamati ya Viongozi wa Dini na Wanaharakati kuhusu Madini wale waliotoa ripoti ya The Golden Opportunity, wape nakala ya ripoti ya Bomani. Waambie nao waweke kambi Dodoma. Ni mapambano kati ya kina Mangungo wa Msovero na umma wa watanzania. Lazima wakina Karl Peters wakimbie. Fanya hima kabla jua halijatua. Huu ni wakati wa Maji Maji

  Asha
   
 5. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mpaka kieleweke,

  Kwanini tusikubali yaishe tu??unadhani tutabadilisha chochote..?Kama waliweza kumnyamazisha mama Kilango kwa mkwara Mzito wewe unazani hili tutaweza.

  Mie naona tuwazirie nchi,Ndiyo sie wajinga..waache waendelee
   
 6. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2008
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkulu nimekupata vyema, niliwaona bungeni na naibu spika akasema wataongea na spika, kumbe ni mambo za barrick, siclair, na wengineo sio? Sasa nimepata akili. Ni jambo nyeti sana mkulu hilo, nadhani hii inatakiwa iwe rai special na lifanyike linalowezekana wakati wewe ukiendelea kutushushia nyeti mkuu
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kwa nini Benki ya Dunia iingelie na kuhalalisha ripoti ambayo inaonyesha wazi kuwa Tanzania inanyonywa? Bei ya aunsi moja ya dhahabu ni Dola za Kimarekani $1000.00 Serikali ya Tanzania inapata $30.00 ambayo ni asilimia 3% na makampuni haya yanapewa misamaha ya kodi na ushuru!

  Screw World Bank, @#$% IMF, and all Sinclair cronies can go to hell!
   
 8. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nashauri kuwa wote wawasiliane na wabunge wao popote pale walipo kuhakikisha kuwa wanakuwa na msimamo na kuwakatalia hawa jamaa .

  Ntajitahidi kuweka namba za simu za wabunge wote na majimbo yao ili kesho tuanzie huku JF kuhakikisha kuwa tunakwamisha mpango huu wa kuendelea kumaliza madini yetu.

  Nitawapa yaliyojiri zaidi na hata usiku huu atakutana na wabunge hotelini kwake kwa ajili ya kuendeleza mkakati huo ambao umefanyika sasa kwa wiki nzima huko Dodoma .
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Hao World Bank ndio hao hao waliokuwa wakimpa misifa Mkapa eti ya uchumi kukuwa.
  Wakae pembeni kwanza tuchukuwe nchi yetu halafu ndiyo waje tunegotiate.
  Lakini nchi ipewe wananchi kwanza kwa kuzingatia mapendekezo pamoja na mengineyo...Yale ya kamati ya madini.
   
 10. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu kumbuka kuwa sera ya madini ilitengenezwa na wataalamu wa Benki ya dunia hivyo wanajua wakifanikiwa kuipeleka huko basi wataweza kuwainfluence kama walivyofanya hapo awali.
   
 11. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Huna haja ya kumpigia simu Tundu Lisu wala Shivji wala shirika lolote.Lobbying maana yake ni ushawishi and not anything illegal.Cha msingi ni kwa wabunge kuelewa kuwa huyo balozi anatetea maslahi ya waliomtuma hivyo basi na wao wasisahau maslahi ya waliowatuma.
  Pili tuache kufikiria kuandamana and all that crap, tutafute njia za sisi pia kulobby kwenye mabunge ya nchi nyingine,hii ndio dunia tukilialia tu hakuna tutakachopata.Stand up send our ambassadors to lobby all around the world.
   
 12. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kumbe sasa tunaanza kujua janja la mabalozi kusifia serikali zetu kuwa zinafanya vizuri wakati wananchi wakiendelea kukamuliwa na kukosa hata mlo mmoja kwa siku.

  Nafikiri cha kuelewa barrick wanafanya biashara kama ni biashara lazima tufaidi wote.
  Hawawezi kuchukua raslimali zetu na kutuachia mashimo.
   
 13. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hima! Hakikisha ripoti ya Bomani anapewa Invinsible na Enigma. Haraka! Hakikisha tunaipata hapa JF, ili wajue tunajua nini wanapaswa kusema na kufanya. Ili wajue nini wananchi tunatarajia kutoka kwao. Vinginenvyo, watafanya Ze Comedy na kudhihirisha maneno ya Sinclair kuwa Kikwete hatazingatia mapendekezo ya Kamati. Weka ripoti ya Bomani hapa, from X to Z tuwashike mashati hao wabunge wetu, waseme yale tunayotaka waseme kwa niaba yao na si yale wanayotumwa nao hao vitangulizi vya wakoloni mamboleo. Shime, zingatia upesi!

  Ni ombi la kutimiza wajibu. Hii ni Jihad

  Asha
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kwamba..Nina uhakika kuwa KATIBA YETU ILIVUNJWA!
  Na hatuwezi kutumia style kama ya serikali ya marekani kwani kwetu sisi nchi yetu ni kama state moja tu kati ya hamsini walizo nazo.
  Hivyo ndugu yangu hatutaki mikataba ya kinyonyaji kwasababu wananchi hawakuulizwa na hawakuambiwa kinachoendelea!
  Wana haki ya kuuliza...Wana HAKI ya kudai maelezo...WANA HAKI YA KUDAI HAKI!
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Ninachoshindwa kuelewa ni kwanini issue hii inakuwa treated hapa JF as if it is emmergency or breaking news as the heading suggests???!!! Hivi mlikuwa hamjui kuwa hii kitu ilikuwa inaendelea kila siku?
  Kama mmesoma vizuri maelezo ya Mtsimbe rais wa TPN, mojawapo ya malengo yao ni kulobby serikalini. Sasa cha msingi ni kwamba such lobbying isiishie ndani ya Tanzania.
  Badala ya kutumia energy nyingi kujaribu kubadilisha mienendo ya dunia wakati mwingine ni busara zaidi kujifunza baadhi ya mienendo usiyoiridhia na kwenda nayo kama ilivyo.Lobbying is one of those.
   
 16. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hiyo lobbying iende mpaka kishwa chako uweze kutambua ukweli kwamba wabunge wako ni "Ndio Mzee", wakiambiwa na mzungu 'jump' wanaulizwa 'how high', sasa na sisi tukafanye lobbying kama wanavyofanya wao ili wasiruke ovyo ovyo. Agenda juu kipungu.....

  Asha
   
 17. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Yaani naona tumefika pabaya nchi imeanza kudharauliwa kiasi hiki kiasi kwamba mtu anakwenda hata kwenye vyombo vyetu vya kutunga sheria kufanya LOBYING. Hii sasa itatufikisha mahala pa kutunga sheria za kuwalinda mafisadi.

  Hawa inatakiwa wakemewe kabisa kwa kuingilia mambo yetu ya ndani. Wao inatakiwa waje wawekeze kulingana na sheria tulizo nazo na si vinginevyo ambaye hataki harudi kwao basi.
   
 18. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Ukienda kucheza mpira ukakuta mchezaji akipigwa kiatu hakuna faul basi na wewe ukimuona mshambuliaji anaelekea golini kwako piga kiatu.Kama huwezi basi jitoe kwenye mashindano.Kwa bahati mbaya in this case huwezi kujitoa kwenye uchumi wa dunia so kilichobaki ni sisi pia kulobby.Kama hatuwezi kulobby Canada basi twende Gambia etc. This is how the world is. Tusipoteze nguvu bure kubadilisha hiki.k
  Kuna vitu vingi vinavyobadilishika tupeleke nguvu zetu huko.
   
 19. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa tupeleke nguvu zetu kuondoa Chama Cha Mafisadi maana wameshindwa kabisa kucheza huu mchezo wanashindwa na wenzao wa Chile, Bolovia, Venezuela. Ndio tabu ya kuwa madarakani na watu wenye conflict of interest na wakina Barrick, TRE nk! Hawa makuwadi wa soko holela na utandawizi. Viongozi dhaifu kimaono na kimaadili! Hao ni wakina Mangungo wauza nchi kwa shanga, ndio nishani anazopewa Kikwete na misifa ya kuachia. Unadhani madini yetu ni ya kujinadi ovyo ovyo kama vyangudoa? Tanzania si jamvi la wageni jamani!

  Asha
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Barrick wamelobby serikali ya Canada iwasaidie kulinda maslahi ya biashara zao. Makampuni ya Tanzania nayo yanyaweza kufanya the same mfano IPP inaweza kulobby serikali ya Tanzania ilinde maslahi ya biashara zake abroad.
  Kwa hiyo tatizo sio serikali pake yake, initiative inaweza kuwa ya serikali, kampuni au hata shirika lisilo la kiserikali.
   
Loading...