Stimulus Package kwa wasanii: napendekeza serikali ikae nao, iwape hela, waandae matangazo kuhusu corona,yaruke hewani,tusiwajali kwenye kampeni tu!

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,586
2,000
Huo ndio ushauri wangu, wasanii, kwa makundi na aina ya sanaa zao, wapewe fedha waandae matangazo, kama ni TV, basi wanaweza kuwa hata kumi kwa tangazo, matangazo yakawa mengi,vituo vya redio na TV na magazeti, serikali ikadondosha kwa hata milioni 500-700

#stimulus package
 

Naby Keita

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
3,813
2,000
Bora useme ipelekwe kwa wauguzi huko .........kama matangazo wasanii kwa sasa na wao wajitolee tu
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,906
2,000
Nyinyi subirini tu muda wa kampeni uanze ili ccm iendelee kuwatumia kama toilet papers.
 

joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
5,530
2,000
Huo ndio ushauri wangu, wasanii, kwa makundi na aina ya sanaa zao, wapewe fedha waandae matangazo, kama ni TV, basi wanaweza kuwa hata kumi kwa tangazo, matangazo yakawa mengi,vituo vya redio na TV na magazeti, serikali ikadondosha kwa hata milioni 500-700

#stimulus package
Huo mchakato wa wasanii kulipwa pindi nyimbo zao zitakapo sikika redio umeanzia tokea enzi ya Kikwete anaingia madarakani mpaka anatoka,Magufuli nae anamaliza awamu yake ya kwanza haujulikani umeishia wapi.

Mkombozi wa wasanii ni digital platforms basi kidogo unadunduliza za kukusukuma ukisubiria balaa la Corona liishe ili upige show.
 

Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,204
2,000
Wasanii watoe matangazo ya nini?! Nchi inapumulia mashine mnazungumza wasanii. Hao wadeal na magonjwa nyemelezi kwanza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom