Stika za usalama barabarani zauzwa kama njugu!

M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
151
Wanajamii,

Kuna jamaa kaja ofisini asubuhi hii kuorodhesha watu wanaohitaji stika za usalama barabarani. Ukihitaji unaandikisha jina lako na kumpatia Tshs. 5000/ = then yeye anakuletea.

Nijuavyo mimi stika ya usalama barabarani inatakiwa itolewe baada ya gari lako kukaguliwa na kuonekana lipo salama kuendelea luwepo barabarani. Lakini kama hali ni hii ya kuuziana stika bila ukaguzi ya vyombo vyetu vya usafiri, Je, tuna nia ya dhati kweli kuepusha ajali?
 
anapatikana wapi uyu jamaa aise namtafuta sana aturahisishie mambo kwa hali ya kawaida huwezi kagua magari yote dar kwa wiki mmoja inabidi iwe ivyo tu
 
Wangekuwa wanakagua sidhani kama tungekuwa na vimeo barabarani, magari yenye vidumu vya mafuta na mrija mrefu kama ya kupikia gongo, mengine ni injini tu, bodi yote chakali (tena ya abiria) mengine kuwasha hadi kusukuma mita 500!!! mengine hata haijulikani muundo "orijino", hakuna hata dashboard, nk...!!!!??
 
Duuh...mna bahati nyie, mi jana nimeifungia safari mpaka O'bay Police, halafu wakaningojesha sana tu!
 
''uongozi legelege hutoa matunda legelege'' kwa staili hii ajali zitaishaje??siku hizi gari kuua watu kumi ishirini tz its not a breaking news, tushazoea!hee nchi yangu na chama changu!
 
Hii ndiyo TANZA yenye NIA, na hapo tusubiri ya FIRE. Lazima warudishe hela ya Igunga
 
Stika za usalama barabarani mbona ishu ndogo sana hiyo!!!!! Toka zimebuniwa sijawahi kwenda police kutafuta hio, naletewa office au nikiwa bar!
 
Hilo zoezi ni kama mradi binafsi wa traffic kujiongezea mapato, zoezi ni hovyo halina tija na pesa yote wanakusnyia mfukoni na rushwa za 1,000, 2,000 ili kupata hiyo stika
 
Wanajamii,

Kuna jamaa kaja ofisini asubuhi hii kuorodhesha watu wanaohitaji stika za usalama barabarani. Ukihitaji unaandikisha jina lako na kumpatia Tshs. 5000/ = then yeye anakuletea.

Nijuavyo mimi stika ya usalama barabarani inatakiwa itolewe baada ya gari lako kukaguliwa na kuonekana lipo salama kuendelea luwepo barabarani. Lakini kama hali ni hii ya kuuziana stika bila ukaguzi ya vyombo vyetu vya usafiri, Je, tuna nia ya dhati kweli kuepusha ajali?

Magari ya watu wa maofisini siyo mabovu ndiyo maana hayaitajiki kukaguliwa, yanafanyiwa service kwa wakati na mengi hayana hata miaka mitatu. Magari ya kukaguliwa yako masokoni kule na daladala mnazopanda
 
Mi mwenyewe na shida na sticker kwa sababu sikuwepo wiki ya usalama barabarani. Msaada
 
Ndachuwa,

Watu wa maofisini ndiyo wapi hao?

"Service" ndiyo ile shughuli mnayoifanya Victoria Filling Station mwisho wa wiki?

- badilisha filter
- badilisha Oil
- badilisha mafuta gear box
- badilisha coolant
- osha gari ndani nje na engine
- DONE

HIYO NDIYO SERVICE unayoiandika hapa?!!!!!!!!
 
Mi mwenyewe na shida na sticker kwa sababu sikuwepo wiki ya usalama barabarani. Msaada

Tupo kwenye wiki ya usalama barabarani ...

Mtafute Traffic yeyote njiani, mpatie TZX 3000, mwambie akupatie "sticker" - done!
 
Hizi sticker mi huletewaga tu home kama nlivyoletewa leseni nayoitumia!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom