Stika za fire extinguisher | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stika za fire extinguisher

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dear, Dec 2, 2009.

 1. D

  Dear Member

  #1
  Dec 2, 2009
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wadau ,
  Mimi bado nina kamba hapa JF.na sijui kama hili limeshapewa ufafanuzi hapa jamvini,
  Mimi bado sijaelewa hizi stika za zimamoto za kuwekwa kila mwaka kwenye gari na kulipiwa gharama kubwa tu,na nafikiri ndio imeanza sasa hivi,
  Naomba mnisaidie kunifahamisha kama hizi stika ni lazima na zinasaidia nini,maana kama mimi Fire extinguisher ninayo na bado haijaexpire na kisa cha mimi kwenda kuilipia polisi ni nini?,au nayo FE iwe inalipiwa kodi kuwa nayo,
  Je mwaka unaokuja kama nalipia tena na bado haijatumika au kuisha muda wake niitupe? maana ni nilazima niilipie kila mwaka kwa madai yao.
  Vile vile naomba nieleweshwe kama huu mradi ni kwa ajili ya kuongezea mapato jeshi letu au ni biashara ya mkubwa Fulani,
   
 2. kilema

  kilema Member

  #2
  Dec 2, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  UFISADI MTUPU! kwanini stika na siyo Cylinder ya fire extinguisher. Mlio wa fedha au fedha unataka?
   
 3. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Makubwa madogo yana nafuu eti mtu anauliza nyumba ndogo zirasimishwe au la... wewe nunua hiyo stika 5,000 tu badika uone kama mtungi unahitajika otherwise utembee na hela ya hongo

  Juzi nilikuwa kwenye basi kuelekea dom tukapita pandambili pale lilipoungua lile basi la Taqwa likielekea Kigali na Chacha wangwe alipomaliziwa mbele tukakuta trafik akamuuliza dereva amuonyeshe stika ya fire badala ya kumuuliza wapi mtungi wote tukashangaa
  Kweli hapa bongo ...utabaki kushangaa

  Mod ipeleke hii kunakohusika
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Juzi nilivimbishiana kifua na trafiki mmoja pale morocco baada ya kusimamisha gari yangu cha ajabu ananiuliza stikaya zima na kiukweli sikuwa nayo lakini fire extinguisher ilikuwepo kwa kweli ilikuwa mtifuano mzito mpaka kuja kulimaliza hilo suala. Askari anataka kunilipisha faini kwa kutokuwa na stika ya zima moto mpaka alipokujaaskari mwenzake mwenye akili timamu alimshauri aniachie lakini nikanunue stika!!! Watu wetu wanakuwa kama kasuku kila wanachoamrishwa kufanya wanafanya tu bila hata ya ku-reason out!!!
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  jamani hiii mada imekosea njia ama mletaji kaona hapa ndo kuna watu wengi atapata msaada???
  du sijui nicheke ?
   
 6. D

  Dear Member

  #6
  Dec 2, 2009
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  First Lady,
  ni wapi inatakiwa kuwekwa hii mada,
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mimi nafikiri huu ni mpango wa serikali (chama kilichopo madarakani) kujipatia fedha kwa ajili ya kupigia kampeni za uchaguzi mwakani hasa katika kuwahonga wana nchi! Hamna la maana hapo ! Kwani gari ikiungua si yangu au serikali ilinisaidia kununua ? Wasitufanye wajinga sisi! Tunawaelewa sana na hawawezi kutupumbaza kamwe
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  inatakiwa ikae pale kwenye hoja mchanganyiko au
   
 9. a

  alex50 JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Hivi nisipolipia hio stika ya fire nitashatakiwa kwa sheria ipi? Na hio ilipitishwa lini na wabunge.
  Mafisadi wanataka kutumaliza mpaka tone la mwisho
   
 10. D

  Dear Member

  #10
  Dec 2, 2009
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  First Lady,
  kama unavyoona mimi ni mgeni so siyajui maeneo ya humu,sasa nitoe kamba mguuni na kunielekeza lakini usinicheke mtoto wa mwanamke mwenzangu
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  haya dear endelea tu si muda utakuwa mwenyeji hasa na utafahamu maeneo yote hata mtoto huwa anaanza kukaa ,kutambaa ,kusimama ,hata kutembea mwenyewe
  Karibu sana
   
 12. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Polisi amwagiwa kinyesi na kibaka

  [​IMG] Askari kanzi ambaye alipakazwa kinyesi na mtuhumiwa wakati akimkamata katikati ya jiji la Dar es Salaam mchana wa leo.
  [​IMG] Kibaka aliyempaka kinyesi askari akiwa chini ya ulinzi wa Askari kanzu.
   
Loading...