Katiba ya shirikisho la Afrika Masharki

IAfrika

JF-Expert Member
Oct 4, 2014
275
216
Kama tunavyojua kwa sasa, marais wa Jumuiya waliamua kuwa kongamano la kisiasa (confederation) itakuwa muungano wa kisiasa wa mpito wa kukaribisha shirikisho la kisiasa (federation). Tofauti kubwa kati ya kongamano la kisiasa na shirikisho la kisiasa ni kuwa uanachama wa au kuondoka kongamano ni kwa hiari ya nchi kivyake, lakini katika shirikisho uanachama ni wa kudumu, yaani unahitaji ruhusa ya nchi wanachama kujiondoa kutoka kwa shirikisho. Kuanzia hapa nimetumia shirikisho sawa na kongamano.

Wataalam wa katiba kutoka nchi za Afrika Mashariki wamekuwa wakikusanya maoni ya wahusika, na hadi sasa walishaenda Burundi kabla kuwepo na korona.

Wataalam wa Katiba wangependa kusikia maoni ya umma na wadau juu ya maswali na maswala yafuatayo:

  • Ni majukumu gani ya mungano yawekwe chini ya utawala wa Shirikisho la Kisiasa?
  • Muundo wa utawala wa Shirikisho unapaswa kuwa vipi?
  • Kanuni kuu za utawala (principles of governance) wa shirikisho zinapaswa kuwa zipi?
  • Je! nchi za shirikisho zinapaswa kuhusiana vipi na mamlaka ya kongamano?
  • Katiba inayounda Shirikisho la Kisiasa itapitishwa vipi?
  • Ni mambo gani mengine yanayopendekezwa na wadau yanapaswa kushughulikiwa katika Katiba ya Shirikisho la Kisiasa la EAC?
  • Maamuzi ya mamlaka ya shirikisho yatafanywa kwa njia ipi?
  • Je! Shughuli za shirikisho zinapaswa kufadhiliwaje?

Link ndio hii hapa Briefing: What you should know about the drafting of the East Africa Community Political Confederation - RegionWeek

Wale wadau wa "impossible" na "not in the next 60 years" stay out of this one kaeni kando kidogo, hio sio hoja au anzisha uzi wako, usichafue uzi huu ulio wa muhimu na manufaa.

Ukisearch East Africa Federation au Constitution kwenye YouTube utapata everyone is super excited for EAF except East Africans. They have even given it a name of EAF already kama ilivyo hapa…



Manufaa ya jumuiya yamekuwepo, kwa mfano, eneo la Afrika Mashariki ndilo lililotanganama zaidi ya miungano ingine ya Afrika, na uchumi wa Afrika Mashariki ndio umekuwa ukiimarika kwa kasi cha juu duniani. EA is the fastest-growing region in the world, and it is not by accident that it is happening since the formation of EAC two decades ago.

Migogoro kati ya nchi ya Jumuiya haitawahi kuisha, na hakutakuwa na wakati mwafaka wa kuwepo na shirikisho la kisiasa la kulinda na kugawa yale manufaa yanayotokana na muungano isipokuwa sasa. Isisahaulike kuwa hakuna nchi ya Jumuiya hadi sasa imejihusisha kwa vita na nchi ingine ya Jumuiya tangu mwaka wa 1999. Feuds between or among states will never end, neither will there ever be a perfect time to come together and form a political Union.

My take....

Majukumu ya Ushirikiano yanapaswa kuwa machache sana (limited) kwa sababu hii itakuwa serikali kubwa ambayo haifai kuwa katika kila jambo la mwananchi. Majukumu ya mamlaka ya ushirikiano yanapaswa kuwa pamoja na ulinzi (defense), biashara baina ya nchi zinazoshirikiana pamoja na sarufi moja na benki kuu (interstate commerce and monetary union), sera ya nchi za kigeni na biashara za kimataifa (foreign policy and trade). Mambo mengine yaachiwe inchi wanachama au kufanywa pamoja na nchi wanachama.

Alafu mfumo wa utawala uwe wa kugawa mamlaka kati ya bunge, mahakama huru, na rais pamoja na serikali yake ili mamlaka mengi yasiwekwe kwenye ofisi moja. Bunge ambalo litagawanywa mara mbili liwe na baraza la kuwakilisha wananchi kulingana na idadi ya watu na seneti ya kuwakilisha nchi ambazo zinaungana, alafu bunge hili liwe ni la kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi. Pia rais na makamu wake awe wa kuchaguliwa moja kwa moja na wapigakura wasio pungua zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa. Kisha maamuzi ya uteuzi katika nyadhfa kuu serikalini ya rais yawe nje ya bunge na ya kuidhinishwa na seneti. Ili hii iwe confederation na sio federation, maamuzi ya serikali ya shirikisho yafanywe kupitia makubaliano na summit ya marais wa nchi au council ya mawaziri.

Tuanzie hapo...
 
Mimi naona tushirikiane kwenye biashara ya forodha na Maswala ya usafirishaji,elimu ya juu na afya
 
Mimi naona tushirikiane kwenye biashara ya forodha na Maswala ya usafirishaji,elimu ya juu na afya
Haya maswala yote uliyotaja yameshatimizwa kupitia mikataba ya Jumuiya na yapo katika hatua tofauti ya kutekelezwa. Hivi sasa Jumuiya ipo katika awamu ya mwisho ya utengamano wa kisiasa itakayo anza na kongamano(confederation) kisha baadaye shirikisho(federation).
 
Huu uzi ni wamuhimu sana lakini naona tunaupita tu sijui kwa nini.Maoni yangu ni kwamba Hatuna haja ya Political Federation.Tunahitaji itu viwili tu.Free movement of people,Policy harmonization,Free trade,Open Governance.Mengine nitaleta bdae
 
Huu uzi ni wamuhimu sana lakini naona tunaupita tu sijui kwa nini.Maoni yangu ni kwamba Hatuna haja ya Political Federation.Tunahitaji itu viwili tu.Free movement of people,Policy harmonization,Free trade,Open Governance.Mengine nitaleta bdae
Ni uzi muhimu utakao sadia wanajumuiya kujitayarisha kutoa maoni yao kwa tume ya kutunga katiba ya muungano.

Free movement of people ipo hivi sasa ila unahitaji kibali kutembea Afrika Mashariki. Kile ambacho hakiko ni right of residence ambayo ni muhimu kwa kufanya bishara kwa nchi zingine.

Policy harmonisation huwa inafanywa ila hakuna utelezwaji wala uajibikaji.

Free trade na hata open governance ni kuenda mbele wakati mmoja na kurudi nyuma wakati mwengine.

Manufaa ya Political Federation ni kuwa itahusisha watu na sio vingozi au wanasiasa tu katika utawala wao. Maamuzi ya federation sio ya kutekelezwa kwa hiari ya nchi au wanasiasa bali ni makubaliano ambayo kila mhusika anapaswa kutekeleza kwa uajibikaji. Hii inamaanisha ikipitishwa kuwe na free movement of people hakuna yule atakaye enda kinyume na hayo makubaliano au sheria. Kisha cha muhimu kabisa nikuwa federation ndio itaweza kugawa faida za kifedha ya muungano kwa nchi zote kupitia makadirio ya bajeti au revenue sharing ili kuhakikisha nchi zote wanachama zinaendalea kwa pamoja na sio tu Uganda, Kenya au Tanzania inakuja kwa kikapu cha shiriko inachukua inachopenda na kurudi zake makwao kama ilivyo sasa. Federation itashikanisha nchi husika kwa pamoja ilizishirikiane kwa gharama na faida ya muungano.
 
Back
Top Bottom