Stickers za week ya nenda kwa usalama: bei ni Tshs 3000 au Tsh 5,000?

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,198
Mods, naomba niweke hii thread hapa kwenye habari za siasa ili watu wengi waine maana nahisi watu wanaibiwa hapa mjini na polisi.

Stickers za week ya nenda kwa usalama zimedhaminiwa na Airtel na Engen kwa maneno mengine police wamepewa bure. Hata hivyo kwenye sticker bei imeandikwa TSHS 3,000/= hivyo dereva anatakiwa alipe kiasi kilichoandikwa kwenye sticker. Lakini cha ajabu police wanatoza TSHS 5,000/=! Je hii ni sahihi au police wamegundua mradi mpya?
 
kwetu police wanadai Tshs 10,000

Kwa kweli kuna mambo mengine yanaonekana madogo lakini yanaudhi. Mimi askari wawili wa kike waliokuwa wanatoa hizo sticker kwa sh 5000 walikuwa wakiwaambia wanunuzi "Hivi mnatoa 5000 kamili mnashindwa hata kuongeza lunch" baadae unachukua sticker unagundua kumbe imeandikwa 3000. Hii si haki hata kidogo tatizo tumejengwa kuwa Taifa la watu waoga na hata wabunge wetu huwa hawaoni kuwa vitu kama hivi ni kero za kusema bungeni Waziri aeleze hizo elfu mbili za ziada zinaingia wapi.
Mfano mwingine ni sh. 30,000 zinazounganishwa na kodi ya barabara ya mwaka (Road license) ambayo kimsingi ni kwa ajili ya kucheki na kujaza car fire extinguisher kama imepungua. Unalipa ukienda fire unadaiwa fedha tena kama 15,000, askari hawa ukiwaambia umeshalipa TRA hawakuelewi na wanang'ang'ania fire extinguisher yako. Kwa kweli yaweza kuonekana madogo lakini ni kati ya mambo yanayonifanya nitafute MABADILIKO mwaka huu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom