Steven Wasira, ndiye msaliti pekee aliye rejea chama chake na kupanda kisiasa

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
8,694
2,000
Tangu kuasisiwa kwa vyama vingi1992 kumekuwa na tabia ya wanasiasa kuhama vyama vyao na kujiunga vyama vingine.

Rafiki yangu mmoja amewahi kunipa siri ya huku kuhama hama. Moja, ni mwanasiasa kudhani ni muhimu sana ndani ya chama chake kuliko chama chenyewe. Hivyo anaota mapembe, anakuwa haambiliki, na kulazimisha anayoyataka yy ndiyo yawe misingi ya demokrasia. Anahama kwa kuwa anafikiri kwa kufanya hivyo at a kimono chama hatimaye kisambaratike.

Mbili, wengi wao hufanya hivyo ili kuongeza umuhimu na thamani yao. Kwa maana ya kwamba wakihama watafuatwa na kubembelezwa kwa kuahidiwa vyeo ili warudi. Hili linaweza kufanyika lkn ni kwa muda tu na baadaye msaliti anatoswa na kususwa kabisa.

Na historia inaonyesha kwamba katika wasaliti wote waliowahi kutokea ktk vyama vyote ni mmoja tu aliyeweza kupaa kisiasa. Huyu ni Steven Wasira aliyekuwa mbunge wa Bunda kwa miaka mingi na kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo uwaziri.

Wasira aliihama ccm na kutimkia NCCR 1995 baada ya jina lake kukatwa na kunyimwa kugombea kupitia ccm. Aligombea ubunge kupitia NCCR 1995 na kumbwaga waziri mkuu wa wakati huo ndg Joseph Sinde Warioba (na ndiyo chanzo cha jina la utani Tyson). Lkn ushindi wake huo ulitenguliwa na mahakama kuu mwaka 1996 na ndipo mwaka 1998 aliamua kurejea ccm.

Na hata baada ya kurejea ccm Wasira aliendelea kulamba vyeo vikubwa vikubwa tu na akawa tegemeo kubwa ndani ya chama na serikali.

Tofauti na Wasira hakuna mwingine aliyepata kuheshimiwa na kuthaminiwa kwa muda mrefu ndani ya chama chake baada kukisaliti na kurejea. Wengine wamekuwa wakipozwa kwa kupewa cheo kwa muhula mmoja tu kisha kutoswa na kusahaulika kabisa. Mifano ni mingi sana. Kila msomaji wa makala hii ajikumbushe mwenyewe.

Hili liwe funzo kwa wanasiasa wote wasio na msimamo imara na thabiti ndani ya vyama vyao.
 
munkango

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
336
500
Vipi kuhusu Daniel Nsanzugwanko? Huyu nafikiri pia alikuwa upinzani alirejea CCM na alikuwa waziri kipindi cha JK
 
Elevat Kapela

JF-Expert Member
Dec 9, 2017
529
1,000
Sababu nyingine wengine huhama vyama walkway majasusi, wanaenda sehemu kupata taarifa na kutengeneza mtandao mkubwa ambao akihitajika kwa waliomuagiza anaanza kutafuta mgogoro wa lazima na kuhama na wanachama wengine ili chama hicho kife. Kwa kuwa alikuwa ameagizwa akirudi anazawadia vyeo vingi na heshim.
 
Eliphaz the Temanite

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
3,019
2,000
Tangu kuasisiwa kwa vyama vingi1992 kumekuwa na tabia ya wanasiasa kuhama vyama vyao na kujiunga vyama vingine.

Rafiki yangu mmoja amewahi kunipa siri ya huku kuhama hama. Moja, ni mwanasiasa kudhani ni muhimu sana ndani ya chama chake kuliko chama chenyewe. Hivyo anaota mapembe, anakuwa haambiliki, na kulazimisha anayoyataka yy ndiyo yawe misingi ya demokrasia. Anahama kwa kuwa anafikiri kwa kufanya hivyo at a kimono chama hatimaye kisambaratike.

Mbili, wengi wao hufanya hivyo ili kuongeza umuhimu na thamani yao. Kwa maana ya kwamba wakihama watafuatwa na kubembelezwa kwa kuahidiwa vyeo ili warudi. Hili linaweza kufanyika lkn ni kwa muda tu na baadaye msaliti anatoswa na kususwa kabisa.

Na historia inaonyesha kwamba katika wasaliti wote waliowahi kutokea ktk vyama vyote ni mmoja tu aliyeweza kupaa kisiasa. Huyu ni Steven Wasira aliyekuwa mbunge wa Bunda kwa miaka mingi na kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo uwaziri.

Wasira aliihama ccm na kutimkia NCCR 1995 baada ya jina lake kukatwa na kunyimwa kugombea kupitia ccm. Aligombea ubunge kupitia NCCR 1995 na kumbwaga waziri mkuu wa wakati huo ndg Joseph Sinde Warioba (na ndiyo chanzo cha jina la utani Tyson). Lkn ushindi wake huo ulitenguliwa na mahakama kuu mwaka 1996 na ndipo mwaka 1998 aliamua kurejea ccm.

Na hata baada ya kurejea ccm Wasira aliendelea kulamba vyeo vikubwa vikubwa tu na akawa tegemeo kubwa ndani ya chama na serikali.

Tofauti na Wasira hakuna mwingine aliyepata kuheshimiwa na kuthaminiwa kwa muda mrefu ndani ya chama chake baada kukisaliti na kurejea. Wengine wamekuwa wakipozwa kwa kupewa cheo kwa muhula mmoja tu kisha kutoswa na kusahaulika kabisa. Mifano ni mingi sana. Kila msomaji wa makala hii ajikumbushe mwenyewe.

Hili liwe funzo kwa wanasiasa wote wasio na msimamo imara na thabiti ndani ya vyama vyao.

Huna adabu.... He is elderly man he should be respected like binadamu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom