Steve Nyerere: Mchungaji Peter Msigwa nimemchukulia mwanamke ndio maana anaendekeza ugomvi na wasanii kutangaza utalii nchini

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
4,342
13,069
Nimeangalia hoja za Steve kuhusu kauli alizotoa Mh Msigwa bungeni jamaa amekuja na kashfa na sio hoja kwa nini anastahili nafasi aliyopewa na Mh Kigwangala.

Hivi ina maana anaamini kuwa anaweza kuleta watalii Tanzania ni Mara 10000 Bongozozo anaweza fanya hiyo kazi ila si yeye. Ni kweli yeye, wenzie na Mh Kigwangala walikua na nia nzuri ya kukuza utalii ila hawakua watu sahihi kwa kazi ile

 
Katika kuelekea mwishoni wa mwaka jana kulikua na harakati za kutangaza utalii wa nchi yetu kutumia "celebrities" wetu wa Kitanzania. Katika kampeni wasanii wa filamu pamoja na wa Bongo fleva walihusika kwa kushirikiana na kiongozi wa Wizara husika. Mimi ni mdau wa utalii na ninajua utalii wa Tanzania kwa kiasi changu. Kwa kufanya analysis ya kampeni ile naweza kusema malengo ya kutangaza utalii kwa namna ile yanatija ndogo sana kwa utalii. Kwa sababu zifuatazo..

1. Watanzania tunafahamu hifadhi zetu
Ukiangalia ile kampeni ilikua kana kwamba watanzania hatujui vivutio vyetu kitu ambacho si kweli. Kwa maana hiyo kumtumia Ayo, Naseeb na wengineo ambao 99% ya followers ni Watanzania haina mashiko sana (poor allocation of resources) sababu tatizo la sisi si kutokujua uwepo wa Serengeti, Ngorongoro au Ruaha ila tatizo ni uwezo wa kwenda kutembelea hivyo vivutio.

2. Utalii wa hifadhini ni ghali
Ukichukulia hifadhi zetu za taifa kitu pekee ambacho Mtanzania wa kawaida kwake ni nafuu ni Kiingilio tu cha hifadhini lakini vyote vilivyobaki si rafiki. Kuanzia gharama za malazi hadi usafiri ndani ya hifadhi.

Nini Kifanyike?

Kwa utalii wa Mbugani ili mtanzania wa kawaida aweze kufanya kuna haja ya kutatua tatizo la usafiri ndani ya hifadhi. Ambapo hifadhi inaweza kua na magari yao kama ilivyo kwa hifadhi ya Mkomazi ili kuweza watembeza watu ndani ya hifadhi. Pili kuboresha public campsites ndani ya hifadhi kwa kuweka miundo mbinu rafiki zaidi kwa watanzania kutembelea hifadhi zetu kwa gharama nafuu na usalama wa kutosha.

Baada ya kufanya hayo sasa hata Wizara ikiwatumia wasanii kutangaza utalii wa ndani na kuweza kuwajulisha upatikanaji wa huduma husika kwa gharama nafuu utalii wa ndani utakua.

****************
Zile hoteli za kitalii ndani ya hifadhi zinazotoa huduma za malazi kwa wasanii bure si kwamba wao hawakufanikiwa katika kutangaza hoteli zao, ni wamefanikiwa sana sababu target yao si wewe bali ni ile 1% ya watanzania ambayo wanaweza fanya utalii ukweli wa kuufanya. Hivyo kwa kumuona mbongo fleva/bongo movie ndani ya hoteli husika yule Mtanzania anayeweza nunua atahamasika.
 
Kuwe na affordable hotels kwa watu wa kipato cha kawaida. Wazungu wengi wanaofanya utalii wanategemea credit cards. Akishapata kazi mortgage , gari na starehe inayofuata ni kuzunguka dunia. Sehemu kama Egypt unaweza kupata holiday ya $2,000 hiyo ni package pamoja na nauli ya ndege, hotel na usafiri kwa siku saba.

Ukipata watalii 50,000 wanaotumia $2,000 kwa mwaka kuna faida. Wahudumu wa hoteli watakua na uhakika wa kusomesha watoto wao.
 
Kweli akili hana... yaani msigwa agombee demu na huyo bwege ? what a joke !! Musiba kwa status yake aliyo nayo ....demu wa steve nyerere ndiye atakaye wish kupata hata namba za simu za msigwa...achilia mbali kukutana nae tu na ku-shake hands
 
Kweli akili hana... yaani msigwa agombee demu na huyo bwege ? what a joke !! Musiba kwa status yake aliyo nayo ....demu wa steve nyerere ndiye atakaye wish kupata hata namba za simu za msigwa...achilia mbali kukutana nae tu na ku-shake hands
Naamini alikuwa ana joke tu 😂😂
 
Well said chief, labda kama lengo lilikuwa kuhamasisha tu domestic tourism lakini kwa kusema kutangaza utalii wetu in general (include international tourism) hapo waziri/wizara husika ilibugi sanaa.
Licha ya upigaji wa nyalandu.... lakini katika wakati wake alijitahidi kiasi kuutangaza utalii.... nakumbuka aliingia mkataba na team sunderland ambayo ili weza kuitafutia wizara husika kupata deal ya kuitangaza serengeti katika league ya EPL.. na tangazo lilikuwa linarushwa kweli kupitia zile bilboards za pembeni ya pitch..... binafsi naona ule utaratibu ulikuwaga ni mzuri sana kuweza kuwafikia watu wengi duniani kwa sababu league ya EPL ni platform kubwa ulimwengu...hivyo ndio ilikuwa sehemu sahihi kabisa kwetu kama nchi kuweza kuutangaza utalii wetu...nakuweza kufahamika zaidi
 
Kigwangwala hawa ndio unawatumia? Ikiacha ujinga huo wa mwanamke hata hizo habari za utalii zenyewe hajui anazungumzia nini.
Hebu mawaziri wetu waache kutumia ujinga katika fedha za umma, hii ndorobo hata mie nisiye na jina hawezi kunishawishi lolote maana akili hiyo hana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hearly,
Surely, nakumbuka those time matangazo yalikuwa ni ya serengeti/Ngorongoro sikosei, jamaa alienda extra miles, si huyu wa kupiga picha na kina Ebitoke.
 
Steve Nyerere fupi nyundo na sijui kingerefuka hata kidogo tuu kama mwanafunzi wa darasa la pili ingekuwa je? maana hapo ni mfupi km mwanafunzi wa darasa la awali na akili yake ambayo haina hata lepe la utanbuzie day and night anawaza wanawake I wonder ndio maana ana nanihulu
 
Kuwe na affordable hotels kwa watu wa kipato cha kawaida. Wazungu wengi wanaofanya utalii wanategemea credit cards. Akishapata mortgage, gari na kazi starehe inayofuata ni kuzunguka dunia. Sehemu kama Egypt unaweza kupata holiday ya $2,000 hiyo ni package pamoja na nauli ya ndege, hotel na usafiri kwa siku saba.

Ukipata watalii 50,000 wanaotumia $2,000 kwa mwaka kuna faida. Wahudumu wa hoteli watakua na uhakika wa kusomesha watoto wao.
Na hapa lilipo tatizo kubwa kwa nini watu hawaendi porini na si eti kwa sababu hatuvifahamu vivutio vyetu.
 
Back
Top Bottom