Steven Mashishanga: Nashangaa CCM ilivyokuwa kimya na Baraza la Mawaziri kubwa mno

Huyu mashishanga ni mnafiki tu, rais akianzisha wizara mpya sasa hivi na kumteua yeye kuwa mbunge na baadaye waziri atakataa?
 
Tunarudia makosa yale yale, kumjadili mtu badala ya hoja aliyotoa!

Lengo siyo kumjadili mtu ila ni kutoa tahadhari kwani unapokuwa kwenye system unakuwa na nguvu na ushawishi mkubwa ila ukiwa nje unaweza kuwa na mawazo mazuri kama ya mzee Masishanga lakini yanaweza yasipewe uzito unaostahili.Hii ndio hoja ya msingi.


Mnapokuwa madarakani tumieni vizuri nafasi zenu na siku zote mkumbuke viapo vyenu..
 
That is only possible kama tukiwa na states gvt, kama ilivyo marekani au china. Otherwise ukipunguza baraza la mawaziri kichwa kichwa na huu mfumo wetu ambao wakuu wa mikoa hawana meno. It will be more worse.

We need to decentralise government. Then hapo tunaweza punguza, baraza la mawaziri. This is a modern way ya kuongoza serikali. Madaraka yanapungua kutoka centre gvt, kwenda kwa wananchi. Through states, like they do in USA.

I once head this from a political party ...
 
Kauli ya Mashishanga kuhusu baraza la mawazri na mwenendo wa ccm ina ukweli na ya kuungwa mkono.Lakini tatizo la wana ccm wa leo wamekuwa wepesi kuongea pale tu wanapokuwa nje ya madaraka baada ya kustaafu.Walioko madarakani ndani ya chama na serikalini sijui wanakuwa waoga kushauri au sijui wanaogopa kumuudhi bwana mkubwa.Matatizo ya ukubwa wa baraza imwekuwa ni kelele ya wapinzani tu na wala hayakuanza leo lakini ccm mnaona sawa na walio karibu na raisi hawasemi hadharani kupinga kama Mashishanga na labda nao wanasubiri wastaafu ndio waongee.Hakika hili ni tatizo.

Mkuu, maneno unayosema ni sahihi kabisa, lakini hapa hili tatizo la kutii au kumuogopa mkulu ndio mfumo wa siasa zetu Tanzania. Sio kwa CCM tu bali katika vyama vyote, ni wachache sana wenye ujasiri wa kuvikosoa vyama vyao wakiwemo ndani ya mfumo. Matokeo yake tumeyaona katika vyama vyote, wakosoaji hushutumiwa, husemwa, huitishiwa vikao na pengine kuadhibiwa. Ni wale wachache tu wenye uthubutu wa kusema hadharani ndio wanaofanya hivyo, bila ya kujali nini kitawakuta.

Alichofanya Mashinganga kinaendana na ile falsafa ya kuwa "kwenye siasa, siasa si rahisi mtu kulenga jiwe ukiwa ndani ya nyumba (chama)".
 
Back
Top Bottom