Steven Mashishanga: Nashangaa CCM ilivyokuwa kimya na Baraza la Mawaziri kubwa mno

UWEZO_WAKO

Member
Nov 17, 2010
39
4
Na Lilian Lucas, Morogoro | Mwananchi

MKUU wa Mkoa mstaafu, Steven Mashishanga, amesema licha ya rais kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, angetakiwa kupunguza idadi ya wizara kufikia 15, ili kupunguza mzigo kwa Watanzania kuwahudumia.

Akizungumza nyumbani kwake jana, Mashishanga alisema rais amechelewa kutoa uamuzi licha ya kufahamu matatizo yaliyopo.

Mashishanga alisema rais kwa kuzingatia matatizo ya mfumko wa bei na uchumi, alitakiwa kupunguza idadi ya mawaziri kutokana na bajeti ya nchi kuwa finyu na angeweza kuongeza uwezo wa kuhudumia wananchi.

"Wakati wabunge wakijiandaa kwenda kwenye bajeti, ni wakati mzuri na mwafaka kwa rais wangu kupunguza idadi ya mawaziri, ili aweze kuhudumia Watanzania na angeona hali ya wananchi ilivyo asingekuwa na wizara zote hizi 30, ni nyingi kwa wakati tulionao," alisema.

Kuhusu CCM, Mashishanga alisema rais kama Mwenyekiti wa chama ana haja ya kuangalia kinavyofanya kazi hivi sasa, kwani kimekuwa kimya na huku kikijua fika matatizo yanayokikabili kwa ndani.

"Nashangaa chama changu kilivyokuwa kimya wakati wote! Kinatakiwa kujiangalia upya, ni hatari kama hakitajirekebisha wakati kinatakiwa kuwatetea wananchi kwa kila hali, kwani hakikujua kama kuna uvujaji wa mali? Kwa nini kilikaa kimya kisipojiangalia upya kuna hatari," alisema Mashishanga.

Pia, alipongeza wabunge walioonyesha uzalendo kuhakikisha mawaziri waliofanya vibaya kwenye wizara zao wanaondolewa na kuchukuliwa hatua, kwani bila kufanya hivyo mabadiliko hayo yasingefanyika.

Alisema licha ya rais kufanya mabadiliko hayo, aliwaomba Watanzania kutomlaumu badala yake waendelee kutoa ushauri bila kuchoka, huku akiwataka mawaziri walioteuliwa kutomwangusha.
 
That is only possible kama tukiwa na states gvt, kama ilivyo marekani au china. Otherwise ukipunguza baraza la mawaziri kichwa kichwa na huu mfumo wetu ambao wakuu wa mikoa hawana meno. It will be more worse.

We need to decentralise government. Then hapo tunaweza punguza, baraza la mawaziri. This is a modern way ya kuongoza serikali. Madaraka yanapungua kutoka centre gvt, kwenda kwa wananchi. Through states, like they do in USA.
 
Mzee king'ang'anizi! Alipigwa chin na Jk huyu.Mara leo klab ya wazee veterans,mara améshauri nini na nini ili mradi astoke nje ya reli ya media
 
Huyu atakuwa ni mbowe na siasa zake za majimbo, cdm achaneni na dhana ya siasa za majimbo, mfano halisi ni mbunge wenu Joshua alivyoropoka
 
Huyu atakuwa ni mbowe na siasa zake za majimbo, cdm achaneni na dhana ya siasa za majimbo, mfano halisi ni mbunge wenu Joshua alivyoropoka

No, nimeishi US, China, India and bado naishi uko. State gvt is much succesful. Any way Chadema wana vision zao, na mimi nina zangu, na USA, China, India wana zao.

But kaa chini ufikirie kwanini rasili mali za Taifa zinapotea na wananchi hawanufaiki. Hushangai kwanini watu wa Geita wanakimbilia Dar es Salaam wakati Geita wameacha almasi. Hushangai kwa nini kwa nini watu wa Mwadui wanakimbilia Dar es Salaam afu Mwadui yenye Dhahabu anafaidi Mzungu.

Ifike wakati tupunguze madaraka kutoka serikali kuu. Tuwaache wanaGeita wachague nini cha kufanya, na sio waziri au raisi anayeishi Dar es Salaam na wala hajui dhiki ya geita. Yeye ndo anawapangia wanaGeita nini cha kufanya. Afu wana Geita wanabaki masikini.

Tukifanya hivi. Hata baraza la mawaziri linaweza likawa dogo. Lakini kwa mfumo wa saiv. Its total impossible. Mtu mmoja ndo mwenye dhamana ya madini yote Tanzania,. Ndo maana tunaibiwa... Hata baraza la mawaziri likibadilika. Itakuwa same story, waTz bado tunanyonywa.
 
Mzee king'ang'anizi! Alipigwa chin na Jk huyu.Mara leo klab ya wazee veterans,mara améshauri nini na nini ili mradi astoke nje ya reli ya media

Alishindwa kusoma alama za nyakati na kumpigia debe wazi wazi sumaye!
 
No, nimeishi US, China, India and bado naishi uko. State gvt is much succesful. Any way Chadema wana vision zao, na mimi nina zangu, na USA, China, India wana zao.

But kaa chini ufikirie kwanini rasili mali za Taifa zinapotea na wananchi hawanufaiki. Hushangai kwanini watu wa Geita wanakimbilia Dar es Salaam wakati Geita wameacha almasi. Hushangai kwa nini kwa nini watu wa Mwadui wanakimbilia Dar es Salaam afu Mwadui yenye Dhahabu anafaidi Mzungu.

Ifike wakati tupunguze madaraka kutoka serikali kuu. Tuwaache wanaGeita wachague nini cha kufanya, na sio waziri au raisi anayeishi Dar es Salaam na wala hajui dhiki ya geita. Yeye ndo anawapangia wanaGeita nini cha kufanya. Afu wana Geita wanabaki masikini.

Tukifanya hivi. Hata baraza la mawaziri linaweza likawa dogo. Lakini kwa mfumo wa saiv. Its total impossible. Mtu mmoja ndo mwenye dhamana ya madini yote Tanzania,. Ndo maana tunaibiwa... Hata baraza la mawaziri likibadilika. Itakuwa same story, waTz bado tunanyonywa.

Ukiangalia vizuri utakuta kwamba huyo Makupa ni mjinga mmoja maarufu humu ambaye unapoteza muda kumjibu. Jina lake analolitumia humu linatosha kukuonyesha ni mtu wa aina gani.
Huyu ni mmoja wa wale wapumbavu ambao kwao jambo lolote jipya au geni ni baya, hata uwezo kidogo tu wa kuchambua hoja hana.
 
hawa wazee wanyamaze ndio walioifilisi nchi hadi leo hawa ndio ccm damu anaongea hivyo kwa vile kanyimwa shavu...kama yeye ni mpiganaji aje huku chadema
 
Mzee Mashishanga eti Msemaji wa Lumumba anasema wewe Umezeeka, kwa hiyo eti watu wasikusikilize!
 
Kipindi kabla ya kampeni za urais 2005 Mashishanga alikuwa team Sumaye na alikuwa anajitangaza wazi wazi kwenye majukwaa sasa imekula kwake naona anaendeleza chuki. Majeraha yake ya 2005 bado hayaja heal!
 
Kauli ya Mashishanga kuhusu baraza la mawazri na mwenendo wa ccm ina ukweli na ya kuungwa mkono.Lakini tatizo la wana ccm wa leo wamekuwa wepesi kuongea pale tu wanapokuwa nje ya madaraka baada ya kustaafu.Walioko madarakani ndani ya chama na serikalini sijui wanakuwa waoga kushauri au sijui wanaogopa kumuudhi bwana mkubwa.Matatizo ya ukubwa wa baraza imwekuwa ni kelele ya wapinzani tu na wala hayakuanza leo lakini ccm mnaona sawa na walio karibu na raisi hawasemi hadharani kupinga kama Mashishanga na labda nao wanasubiri wastaafu ndio waongee.Hakika hili ni tatizo.

Mashishanga anasema raisi kachelewa kutoa maamuzi.Bila shaka ni kweli, lakini nani aliyepo madarakani leo ndani ya chama anaweza kukosoa hadharani kama Mashishanga.Mlio ndani ya chama kwa sasa ndio wenye sauti na ushawishi mkubwa na mnaweza hata kumsaidsia mkuu wa kaya na siyo kusubri mpaka mstaafu ndio muwe outspoken.

Mashishanga anapendekeza raisi kama mwenyekiti anahitaji kuangalia chama kinavyofanya kazi na anashangaa kuona chama kiko kimya licha ya matatizo na anaonyo ni hatari kwa chama.Anahoji pia kama chama hakikujua kama kuna ufujaji wa mali.Ni maswali ya mingi lakini leo hii angekuwa ndani ya serikali au chama angeyasema haya?Tatizo wanaccm wa leo mmewaacha viongozi wanaogelea kwenye madaraka na kupiga mbizi na nyie mmebaki watazamaji huku jahazi linazama na badala yake mnangojea mstaafu ndio muongee.Ni hatari sana.

Na kama kuna baadhi ya watu wanakuwa waongeaji(outspoken) baada ya kufukuzwa,kutemwa,chuki binafsi au kusahaulika kupewa nafasi basi mtu wa aina hiyo ni mnafiki na wa kuogopwa kama ukoma na kamwe hawezi kuwa msaada kwenye chama bali ni bomu kwa chama chake.
 
Wakiwa nje wapo safe zaidi, wakiwa kwenye system hawawezi kuukata mkono unaowalisha....tumbo kwanza ebo!
 
Huyu mzee kachoka kiumri na kifkra, leo ndiyo kaliona la ukubwa wa baraza la mawaziri.
 
Tunarudia makosa yale yale, kumjadili mtu badala ya hoja aliyotoa!
 
Back
Top Bottom