Steven Masato Wassira mbaroni kwa kumpiga Mwanahabari

Mdakuzi

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,202
6,581
Kuna habari toka Musoma zinasema kwamba, aliyekuwa mgombea Urais (CCM), Mhe, Steven Wassira amekamatwa na polisi kwa kumpiga Mwandishi wa Habari aliyekuwa akimhoji kutokana na kukerwa na swali alilomuuliza.

Ova
============
Mwanasiasa mkongwe, Stephen Wassira jana aligeuka mbogo na kupambana na waandishi wa habari waliokuwa wakijaribu kumpiga picha, muda mfupi baada ya Mahakama kutupilia mbali maombi yake ya kukata rufaa dhidi ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge wa jimbo la Bunda Mjini.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa Wasira ambaye alikuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika alijaribu kumvamia mpiga picha wa gazeti la Mwananchi aliyetajwa kwa jina la Jamson akitaka kumnyang’anya kamera ili afute picha alizokuwa anampiga.

“Njoo, njoo hapa wewe kijana. Nakuambia futa hizo picha kwa usalama wako. Nakuambia futa hizo picha. Hivi mnanitafuta nini maana mnanifuatilia tangu nikiwa kule Mahakama Kuu hadi huku,” Wasira anakaririwa na gazeti la Mwananchi.

Mwandishi wa gazeti la Mtanzania, Judidhi Nyange alieleza kuwa baada ya kushindwa kumnyang’anya kamera, Wasira alijaribu kumgonga na gari lake wakati anaondoka kwa hasira lakini alishindwa. “Baadae, Wasira alitaka kumgonga na gari wakati anaondoka lakini ilishindikana.”

Wasira aliyekuwa anatetea nafasi yake ya Ubunge wa jimbo la Bunda Mjini kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwa tiketi ya CCM, alishindwa na Esther Bulaya aliyewania nafasi hiyo kwa tiketi ya Chadema.

Wapiga kura wake walifungua kesi ya kupinga matokeo katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza lakini Mahakama hiyo iliitupilia mbali.

steven wasira.jpg
 
Yule mzee kwasasa atakuwa anamatatizo ya kisakiolojia waandishi wanao mfuatilia yule mzee wanapoteza muda wamuache tu mtu mwenyewe alisha poteana kwenye game.
 
Kuna watu wanahamu ya kupigwa kilichompeleka kwa tyson hata sikijui mwache apigwe tu kwa maana hakuna namna
 
Huyu mzee haamini kapigwa mweleka na binti mdogo ktoka chama alichotabiri kinakufa, watu wakae nae mbali maana anaweza fanya mauaji bure, kutoka kushindwa urais hadi ubunge pia kakosa! lazima amevurugwa.
 
Invisible futa huu uzi asije akakunasa kibao na wewe mkuu, ila akikupiga na wewe hapo lazima tutaingilia
 
CAN YOU IMAGINE WHAT TYPE OF QUESTION ASKED?...........

binafsi nahisi Mwandishi alimkera na swali linalohisu......!?
mh. / huoni kwa umri ulionao HUU sasa ni wakati wa kupumzika kuhusiana na maswala ya kisiasa?
I think so.....
 
Back
Top Bottom