Steven Mangele (maarufu Steven Nyerere) kuna uhusiano gani wa bongo movie na CCM?

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
430
780
Assalam wana jamvi! poleni na majukumu ya hapa na pale katika maisha!

Moja kwa moja niende kwenye hoja!

wakati mwingine ni kweli yamkini hainihusu, lakini hiki ndo kizazi chetu, ndo vijana wetu, na watoto wetu lakini pia ndo ndugu zetu!

Muhusika niliemtaja kwa mtazamo wangu ni kama kwa sasa anajinufaisha kisiasa kwa kutumia bongo movie! je, bongo movie ni kundi la wana CCM? na yeye ni nani hasa bongo movie? je, takukuru wamemchunguza huyu mtu? je hawanyanyasi wenzake kwa vitisho na kuwalazimisha kuwa lazima waimbe nyimbo za kusifu na kuabudu CCM?

Ni sahihi yeye kuwa CCM lakini kwanini aje na kampeni za mara kwa mara kukisapoti chama cha mapinduzi kwa jina la bongo movie!

Kama si bakhresa kuja na hii channel ya movie zao, hawa watu walikua wanapotezwa, kwa sasa wanasikika zaidi kwenye matukio ya kisiasa kuliko kazi zao, kuna haja gani ya kuitisha press kuongelea siasa za wazi badala ya kazi? wapo wasanii wazuri wanajua kazi zao, walau! je huyu steven kwanini wamempa nguvu hiyo ya kuwaendesha kuelekea dimbwi la siasa?

Juzi kati kulikua na ugomvi mkubwa sana, kuwa bwana steven alikua anataka kuwa msemaji wa wanamuziki, bila shaka nadhani target yake pasi na shaka anataka akayafanye ya bongo movie kwenye muziki, lakini vichwa vichache kumbe hua vinaona tabia zake vikampa makavu, akaishia kulalamika 'yaanini mie' hii ni mbaya sana, inaathiri sana maendeleo ya sanaa ya uigizaji.

Wajifunze alama za nyakati, wanaweza kutwishwa mzigo ambao si wao, wakaharibu vyao, Tanzania ya 2022 si ya 2005!

Siku njema, na mapumziko mema ya wikiend
 
Mengele anataka fadhila za CCM kupitia Bongo Movie, ingawa mimi nimemuona kwenye filamu moja tuu akicheza sehemu ndogo ya mlinzi wa getini
 
Steve Nyerere ni shujaa wangu wa muda wote. Fikiria mtu asiye na elimu kiasi kwamba hata kuandika tu caption huko Insta huwa ni tatizo lakini kaweza kujipandisha hadi kukaa meza moja na mawaziri pamoja na wakubwa wengine? Steve ana ushawishi mkubwa sana nchi hii tofauti na elimu yake. Mimi nampongeza na ninamshauri azidi kukaza kama inamletea msosi mezani.
 
Bongo Movie na CCM akili zao zinafanana,yaani ni pipa na mfuniko, kwahiyo watajijua wenyewe .
 
Back
Top Bottom