king Davidson
JF-Expert Member
- Feb 9, 2017
- 252
- 1,063
Kama ilivyo kawaida ya nchi yetu kuendeshwa kwa siasa za matukio,tumepitia kwenye matukioi makubwa sana ya kisiasa tukianza na kubwa zaidi tukio la KUTUMBUA, NO MIKUTANO YA SIASA, BUNGE GIZANI, UKUTA, BAA LA NJAA, NA current ni VITA YA MADAWA YA KULEVYA. tumeua siasa za hoja za wakiana Dr. SLaa na Prof. Kitila na kuleta ushabiki wa kisiasa. Uzi huu utahusisha tuikio kubwa kabisa lilio teka vyombo vya habari wiki mbili zilizo pita.
VITA YA MADAWA YA KULEVYA
Tumeona tukio hili bila kuzingatia taratibu za kisheria na taratibu za kiintelijensia watu wakitajana na kulopokalopoka juu ya wahusika wa madawa ya kulevya et wakiita VITA YA MADAWA YA KULEVYA. Baadhi ya viongozi wakikemea huu utaratibu ambao hata kanuni,sheria na Taratibu za vyombo vya usalama unakinzana nao, mfano Nape NNauye, katibu mwenezi wa itikadi na siasa wa CCM na Waziri wa habari, utamaduni na michezo mapema kabisa akiomba busara itumike katika kutajana tajana huku wao wakiita vita dhidi ya dawa ya kulevya. huku wasanii, wanasiasa , wafanya biashara na watu maarufu wakitajwa. hivyo kuibua vihoja, mipasho, urafiki na uhasama miongoni mwa wahusika. Steve Nyerere msanii maarufu wa bongo movie na mchekeshaji steve nyerere tumeaona akiingia kwenye mkenge huo japo hakutajwa. Sababu tu ya kijifanya mjuaji, mwanasiasa na mwanaharakati.Siasa sio sanaa za Maigizo na Uchekeshaji au Umbea na Majungu ya Bongo movie.Ujuaji na unafiki wake umesababisha kukosana na wasanii wenzake akiwamo TID, Umechafua viongozi (wabunge) na kuhatarisha uswahiba wake na godfather wa Dar es salaam Paul C Makonda, (Daud Albert Bashite) DAB Himself. mpaka sasa anaonekana mmbea na mnafiki ambayo ni taswira mbaya kwa msanii na mtu maarufu hasa kwa kuwa yeye mwanaume na mambo ya umbea na mipasho ni ya wanawake.
USHAURI; kwenye tukio lolote lenye utata ni vema kusema kidogo,kutulia na kufuatilia mambo kimya kimya,hata ukiulizwa na wahusika jifanye hujui chochote kuliko kuongea ongea vitu bila kufikiri. kuwa makini na aina ya watu wanao kuzunguka. Atambue Siasa ni vita ya hoja, ikihusisha Ubabe,fitina na harakati. Mipasho, umbea, majungu na maneno ya kanga aache bongo movie.huku ni zaidi ya jihad, ajifunze kwa wasanii wenzake Mh. Joseph Haule(prof.Jay) na Mh. Joseph Mbilinyi (Sugu).