Mbowe, Steven Nyerere mikononi mwa polisi

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Jan 12, 2017
4,824
5,560
Anashikiliwa kujibu kile kinachosambaa kwenye zile audio tatu zilizosambazwa ambapo kawaongelea viongozi mbali mbali

Habari kamili zitawajia hivi punde

============

VIDEO: Steve Nyerere mikononi mwa polisi

FRIDAY , 24TH FEB , 2017
Utata umeibuka juu ya kukamatwa kwa msanii wa filamu nchini Steven Mengele a.k.a Steve Nyerere, mara baada ya kuwepo kwa taarifa hizo ambazo zimetolewa ufafanuzi na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro.
Steve%20Nyerere%202.jpg

Steve Nyerere

Akizungumza leo na wanahabari, Kamishna Sirro amesema yeye hajamuita Steve Nyerere lakini huenda akawa ameitwa na maafisa wake wa upelelezi kwa ajili ya mahojiano, jambo ambalo ni sahihi.

Sirro amesema kuna kikosi maalum alichokipa kazi hiyo na endapo msanii huyo anahojiwa ataweza kuachiwa kama kikosi hicho kitajiridhisha kuwa anastahili dhama, lakini kama kitaona bado kinamuhitaji, kitaendelea kumshikilia.

Msanii huyo ameingia kwenye 'headline' hasa mitandaoni baada ya kusambaa kwa sauti zinazodaiwa kuwa ni mazungumzo kati yake na Mama wa Msanii Wema Sepetu, kuhusu sakata la dawa za kulevya linalomkabili Wema Sepetu.

Katika hatua nyingine, Mwenyenyiki wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefika katika kituo hicho kikuu cha polisi Dar es Salaam, na kisha kupandishwa kwenye gari ya polisi na kupelekwa kusikojulikana.
Mbowe%207.jpg


Freeman Mbowe

Kamishna Sirro alipoulizwa kuhusiana na kinachoendelea kwa mwenyekiti huyo, amesema kuwa jeshi hilo lina mamlaka ya kumuita Mbowe wakati wowote kwa ajili ya mahojiano.

Msikilize hapa akifafanua baada ya kuulizwa maswali na waandishi wa habari
 
kama ni kweli, inatengenezwa chuki kubwa sana kati ya wasanii na serikali, wacha tuone, ila kesi yake naona nyepesi tu, si akanushe basi, kwamba sio yeye, tcra wapo wafanye yao,
 
Anashikiliwa kujibu kile kinachosambaa kwenye zile audio tatu zilizosambazwa ambapo kawaongelea viongozi mbali mbali

Habari kamili zitawajia hivi punde
hizi zote mbwembwe tu. kikubwa kupitia audio ile tumeshajua mengi maovu nyuma ya pazia kuhusu CCM na usanii (na wasanii) wake!
 
Back
Top Bottom