Stesheni ya treni ya 'Mwakyembe' Ubungo ni giza totoro

Dr Guitar tz

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
312
247
Saa 1:30 jioni hii nipo hapa kituo cha Ubungo linapoanzia safari zake hili treni la mjini Dar. TRL walichojenga ni Platform tu, hakuna benchi, maji, vyoo wala taa.

Shirika watambue tuna miaka zaidi ya 50 ya Uhuru, ni aibu mambo mengine jamani, hata ma benchi tu hakuna? Na mamilioni ya tani za mbao yanaenda nje kila siku, huduma hii ni ya umma na kwa vile wame link kituo hichi na Ubungo bus terminal kuna uwezekano wa hata watalii toka nje ya nchi kutumia huduma hii kweli wakiona hali hii ni wazi itawakwaza.

Ushauri kwenu TRL au halmashauri boresheni huduma hii tuendaneendane na miaka yetu 50 ya uhuru.
 
Bro treni hiyo tunaitumia tangu 2012 na kituo chetu kikubwa kwa sie wa Ubungo Maziwa ni hicho

We mgeni nini?
Ukimaliza kawaambie na vile vituo vya Mwananchi, Kamata na Dar Station
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom