Stephen Wassira; Ole wao mawakala wa mafisadi, dawa yao inachemka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stephen Wassira; Ole wao mawakala wa mafisadi, dawa yao inachemka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 24, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Monday, 23 May 2011 18:53 newsroom


  NA STEPHEN BALIGEYA

  KUNA watu wanalipwa ujira kidogo na kuambiwa kuhamasisha wengine nao waandamane lakini hawaulizi kwa nini wanaandamana, badala yake wanauliza tunaanzia wapi? Hiyo ni kauli ambayo iliwahi kutolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Steven Wasira, akieleza jinsi ambavyo kumekuwa na wimbi la watu kutumiwa kwa kuwa tu wamelipwa ujira kidogo.Kimsingi, Wasira alitaka kueleza kwamba, kumezuka tabia ya baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa, kuandaa mkakati wa watu kuandamana ili kujiwekea mtaji wao kisiasa. Tena kinachofanyika ni kwamba, kundi la vijana wanaolipwa, linaandaliwa kuhamasisha watu wengine kushiriki maana
  maandamano ambayo wakati mwingine vijana hao hawajui ni kwa nini wanaandamana.

  [​IMG]

  Mfumo wa kuandaa maandamano bila kujua kwa nini wanaandamana, bali wenye malengo na maandamano hayo wakijua undani wake, uliwahi kutia aibu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwaka 2007 na 2008, wakati fulani ilitokea wanafunzi wakaulizwa kwa nini wanagoma na kuandamana, wengine walisikika wakieleza kwamba, hawajui kwani wameelezwa na viongozi kugoma, unaweza usiamini kama msomi anaweza kubeba bango, alafu hajui undani wa kinachomfanya abebe bango.


  Aidha, wapo waliogoma kwa kulazimishwa baada ya kuchapwa viboko na vijana ambao waliandaliwa mahususi kwa ajili ya kuhakikisha maandamano na mgomo yanafanikiwa. Mwanafunzi aliyekutwa darasani au kitandani kwake amejipumzisha alichapwa viboko na wakati mwingine kusababisha wengine kujeruhiwa. Hao ni wasomi ambao kimsingi, hakuna mtu anaweza kuamini, kama wanaweza kutumiwa bila kujitambua, lakini hilo liliwezekana na kufanyika na bado linaendelea kufanyika kwenye vyuo vingi nchini.


  Katika miaka hiyo iliyotajwa ndio miaka ambayo kulianza vuguvugu la kisiasa la siasa za vyama vya upinzani kuingia vyuoni kwa kasi kubwa na matokeo yake, viongozi wa wanafunzi kutokana na itikadi ya vyama. Viongozi wa wanafunzi wakitekeleza maelekezo ya vyama wanavyovitumikia na wakati mwingine, wasomi hao kutofautiana wao kwa wao juu ya mantiki ya kugoma na kuandamana wakati mambo yenyewe yalishawasilishwa kwenye ngazi husika. Mfumo huo haushangazi kuona mbunge mmoja wa chama cha siasa, kwenda kuwahonga sh.5,000 baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, ili waende kwenye mkutano wa kujadili katiba. Swali linalotawala zaidi ni kama wasomi hawana uwezo wa kuona umuhimu wa kujadili katiba mpaka waongwe na kama ndivyo nini mwelekeo wa taifa?. Haishangazi leo kuona wasomi wakiaminishwa kwamba, mtu makini wa nchi hii lazima awe na mwelekeo wa chama cha upinzani, na anayetoka chama kilichopo madarakani, hapaswi kusikilizwa.

  Hao ni wasomi ambao wanategemewa kusaidia taifa badala yake mawazo yao na fikra zao zimekomea katika kuamini kwamba, ili uwe msomi lazima umzomee mtu kwa kutofautiana kwa hoja.Wakati watu wakijivunia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa chemchem ya kushindana kwa hoja , kimegeuka chuo cha itikadi, chuo cha kuzomea kama njia ya kushindana kwa hoja.

  Mtu makini angetegemea kuona wasomi hao wakitumia hoja zao kupingana na wanayempinga, lakini kwa kuwa usomi wa leo ni wa kiitikadi, umebaki wa kuzomeana na kukashifiana. Vyuo vikuu badala ya kuwa vya wasomi, vimebaki vya kuuliza maandamano yanaanzia wapi, badala ya kuuza kwa nini tunagoma na kuandamana na je njia hiyo ndiyo suluhu ya tatizo?. Ni wasomi hao ambao wakiishiwa fedha za kujikimu kutokana na wakati mwingine kuzitumia vibaya, wanaandaa mgomo ili wapoteze muda, pasipo kujua athari za kupoteza muda huo.Huo ni mwendelezo wa kuharibiwa na siasa za kifisadi na kushindwa kujitambua kwa kina, kwa maana ya fikra jadidi na kubakiza fikra za kuazima ili wafanikishiwe mambo yao.


  MAWAKALA WA MAFISADI WAJITOKEZA
  Mfumo huo wa kutumiwa bila kujitambua umeanza kujionyesha wazi kwenye Chama Cha Mapinduzi kwa sasa, ambapo mawakala wa mafisadi wameanza kujipambanua hadharani. Kama mtu anaweza kutoka leo, na kujiita katibu msaidizi wa CCM wilaya na kutangaza mbele ya waandishi wa habari, kwamba aliombwa na watu fulani kushiriki kuanzisha Chama Cha Jamii (CCJ), kuna maana gani hapa?. Ukiwa wakala wa watu sifa kubwa lazima ukubali kuuza utu wako, kitu ambacho kinambakiza wakala wa mafisadi kuwa kama pia na dudu ambalo linapumua lakini halijui kwa nini linapumua.Katika kipindi hiki ambacho chama kinaweka mkakati wa kusafisha chama ili kirudi katika njia zake imara, isingetegewa mtu ndani ya chama tena mwenye nafasi katika chama, asimame na kuanza kuwatuhumu, viongozi wake eti walianzisha CCJ.


  Hivi kwa akili ya kawaida, CCJ ni muhimu kuliko mafisadi ambao wamekifanya chama kuwa kama dodoki ambalo linabeba uchafu wa kila namna na lisilokuwa na uwezo wa kuchagua tusi?Hivi kweli CCJ ni muhimu kuliko kuokoa chama na kuokoa maisha ya Watanzania ambao wameendelea kuzeeshwa kutokana na ufisadi wa baadhi ya watu ambao wameliweka taifa mfukoni?.

  Katibu huyo msaidizi ambaye anajiita wa CCM wilaya ya Moshi anataka kuwaambia Watanzania kwamba, kuna kitu cha ajabu mtu kuhama chama kama haridhishwi na mwenendo wa chama chake?. Kimsingi, ni mwanasiasa uchwara pekee anayeweza kupoteza muda wake kujadili mwanzilishi wa CCJ, kwani chama alichopo mwanasiasa siyo mama yake wala baba yake, na kama mwenendo wa chama hauendani na itikadi misimamo yake, mwanasiasa ana uhuru wa kuhama. Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kueleza kwamba, alikuwa na uwezo wa kuhama CCM kwa sababu siyo mama yake mzazi, na hivyo anaweza kwenda chama anachoona kinamfaa yeye, kulingana na mwono wake. Mwenyekiti wa TLP na Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Agustino Mrema alihama CCM, na kuasisi NCCR Mageuzi, na kisha akakiacha na kwenda TLP na bado Watanzania wanaendelea kumwamini pamoja na kuhama vyama. Wanamwamini Mrema, kutokana na utendaji wake, na siyo ugwiji wa kuhama vyama, ndivyo ambavyo mwanasiasa yeyote anavyoweza kufanya kama anaona mwenendo wa chama chake hauridhishi. Aidha, Watanzania makini bado wanaimani na utendaji wa Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi Harrison Mwakyembe na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. Kwa hiyo, hata kama watahama CCM leo, utendaji wao ndio utahukumiwa na Watanzania na sio kwamba watahukumiwa kwa kuhama CCM, kwani Watanzania shida yao ni watetezi bora bila kujali wako chama gani.


  Lakini kwa kuwa mafisadi wanazidi kujikita kufifisha juhudi za wapambanaji hao, suluhu yao imebaki kuwatumia watu kama hao wanaojiita makatibu wa CCM, mkakati ambao ulishabainika zamani. Hakuna shaka kwamba, mkakati huo wa mawakala wa ufisadi na mafisadfi ambao wamejificha ndani ya chama kwa mgongo wa majukumu yao kwa chama, umeshabainika na wanachokifanya ni uasi ambao hauna nafasi tena. Kinachofanywa nao ni utekelezaji wa mpango wa mafisadi kudhoofisha juhudi za CCM kuwatosa, ili waonekane wanaotakiwa kuangaliwa ndani ya chama ni wengi. Je, wanataka kuwaeleza Watanzania na wanaCCM, kwamba Sitta, Mwakyembe na Nnauye nao ni mafisadi kama wao? Wameiba nini na wamekosea nini katika kutetea maslahi ya wanyonge?. Mawakala wanaouza utu wao kwa fedha lazima watambue kwamba, damu na machozi ya masikini siku zote havipotei bure, bali mungu husimama juu yao na ole wenu mawakala. Lazima mafisadi na mawakala wao wafahamu kwamba, kila kitu kina wakati wake na wakati ukifika hakuna kinachoshindikana , kwani ni sawa na kifo kikifika hata kama ukikihonga mabilioni hakisikii lazima kikuchukue tu. Kwa mfumo huo huo, nguvu ya fedha siku zote hushindwa na nguvu ya watu ambayo ni sauti ya mungu, na daima sauti ya fedha ambayo ni sauti ya shetani inadumu kwa muda mfupi na mwisho wake huwa kilio badala ya furaha. Ni heri mawakala wa mafisadi na ufisadi wakajiepusha katika kitanzi hiki kwa kuhama chama kuliko kujitia kitanzania wakiwa ndani ya chama, maana damu ya wanaCCM na Watanzania itakuwa juu yao na vizazi vyao.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Dictatorship naturally arises out of democracy, and the most aggravated form of tyranny, slavery and discrimination out of the most extreme liberty. It is frighterning that all CCM leaders are talking about CITIZEN's being DUMB's they don't know what they wanted; This is the person who left CCM for his personal benefits and went back to CCM; kwahiyo alikuwa hajui kwanini alihama CCM na kurudi CCM?
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee naye apumzike, hizi kazi wapewe vijana waje humu jf tuwape makombora hadi wanyoke
   
 4. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Kipofu akimwongoza kipofu mwenzake wote watatumbukia shimoni!
   
 5. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wasira sijakupata vizuri. Kwanza nani alipewa elfu 5,000 udom na ni nani aliwapa hiyo hela ili waandamane? Pili, mbona unalaumu watu kutumiwa na mafisadi inaonekana wazi kuwa unawafahamu vizuri sana hao mafisadi. Sasa kwa nini usiwataje ili mjivue gamba kirahisi? Na kwa nini hao mafisadi unaowasema kuwa wanatumia watu kukichafua chama wasifunguliwe mashtaka ya ufisadi au unawaogopa? Mheshimiwa jaribu kuwa muwazi na kumung'unya mung'unya na kuficha baadhi ya mambo ya msingi na kukazania mambo madogo madogo!
   
 6. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,176
  Likes Received: 1,177
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa viongozi wa selikali na chama hawana mamlaka ya kuwajibisha watendaji wenye makosa? Kazi ni kulalamika tuu maana hata kuwataja wanaogopa!
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  MZEE wetu Wassirra mbona wabunge wetu ndio wanaongoza kwa kuzomea na hili tunataka jibu
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Bila shaka hii thread sasa itakuwa salaam tosha kwa mafisadi na hao vibarua wao wanaodhani watanzania ni watu wasio na kumbukumbu ambao unaweza kuwahamisha kirahisi kutoka kwenye mada muhimu na kuwapeleka kwenye CCJ ambayo hata bango lake sasa hivi halijulikani lilipo. Wanamjua adui wa ustawi wa maisha yao na huyo ndiye wanayetaka kupambana naye. Hayo makando kando yao hayatawapumbaza watu ili wamsahau adui wa kweli na kuwatengenezea 'adui' asiye na madhara.
   
 9. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Acha ujinga wako, wasira hakulipwa kutoka wala kurudi CCM. Alitumia haki Yake ya kidemokrasia na utashi na si vinginevyo.
   
 10. delabuta

  delabuta Senior Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hi Wasira watu wanaoandamana hawajui kwa nini wanaandamana? kweli nimeamini kwamba husomi alama za nyakati hivi kwanini ccm mnakuwa wagumu wa kuelewa na wepesi kusahau, nahizo nukuu zako za udsm sio za kweli ninawasiwasi na uelewa waka kaa pembeni tuachie vijana huna jipya.
   
 11. ADAM MILLINGA

  ADAM MILLINGA Senior Member

  #11
  May 24, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uyo wasira co mtu kabisa alizuia msafara wa chadema na wakapigwa mabomu ya machozi watu wakajeruiwa hana maana kabisa we angalia tu sura yake ilivyo ndomana walimnyima ubunge mnafiki na mfitini mkubwa
   
 12. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Steven Wasira........ni ajabu mwenye cheo hajui hata maana ya cheo chake....yeye vitisho tu badala ya uelewa....huyu alitakiwa awe interface
   
 13. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha haki ya kidemokrasia wala nini ,huyu mzee aliomba kurudi ccm baada ya kusota sana na kupigika kwa jua pale Namanga Dar akiuza samaki na biashara yake ikadoda na mpaka sasa hajamaliza kulipa deni huko alikokopa; hivi sasa anatumia nafasi aliyonayo kufisadi ili alipe hilo deni na ndio maana kila leo yuko safarini!! Bila ya huruma ya marehemu Mzee Kawawa angekuwa bado anauza samaki!!
   
Loading...