Stephen Wassira: Nini maana ya uongozi wa kimkakati?

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,293
24,173
February 10, 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Mwanasiasa mkongwe Ndugu Stephen Wassira anashusha madini kuhusu Uongozi wa kimkakati akihojiwa na watangazaji Sam Sasali, Hassan Ngoma na Babbie Kabae



Stephen Wassira ambaye zamani alipata kuwa kiongozi ktk nafasi ya uWaziri, mkuu wa mkoa, mbunge na afisa balozi Marekani anatumia uzoefu wake kuangazia wakati wa ukoloni, awamu baada ya uhuru za Nyerere, Mwinyi , Mkapa , Jakaya Kikwete na mikakati ya viongozi hao na hali ya sasa.

Stephen Wassira alibanwa kuhusu suala la Dira ya Taifa kukosa undelevu na kila kiongozi anayeingia madarakani huja na yake. Wassira akakumbushwa nchi kama Marekani dira ya taifa aje Rais mwingine au chama kingine iwe Republican au Democrats, Dira ya Marekani haiyumbi. Lakini kwa Tanzania kila kiongozi anayechukua mamlaka huja na jambo linaloitoa nchi kutoka ktk Dira mfano Kilimo Kwanza tatizo ni nini?

Watangazaji wanauliza kushirikishwa kwa wananchi ktk maamuzi makubwa na nafasi ya kuwepo hoja kizani ndiyo hujenga dira madhubuti itakayozingatiwa kila awamu na haitaathiriwa na mabadiliko ktk uongozi, je hali ya kisiasa na kijamii Tanzania inazingatia hilo?

Mfano Mradi mkubwa wa reli mpya ya SGR unaogharimu ma-Trilioni ya shilingi za kiTanzania unaonekana haupo ktk Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 iliyozinduliwa miaka 20 iliyopita , na Wassira anakiri haijulikani lini SGR Mpya itakamilika . Mradi huu umeanzishwa na CCM Mpya.

Wassira azungumzia fedha za World Bank za elimu na changamoto za jinsia / gender nini kifanyike mimba zipungue shuleni. Pia nini maana ya uzalendo na utaifa pamoja na misemo iliyozuka awamu hii kulinganisha na awamu zilizopita.

Stephen Wassira mahojiano yake yanajikita ktk taifa kuwa na Dira / Visheni anazungumzia juu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania 2025 toka taifa hili linapata uhuru na awamu zote za uongozi zilivyopambana na changamoto za nyakati zao kuhakikisha nchi inavuka na kuwa nchi ya uchumi wa kati ya viwanda na maisha bora zaidi kwa wananchi.

Source: CLOUDSMEDIA

More info / Ziada kuhusu dhana ya dira:

Visheni ya Dira ya Maendeleo 2025
Tanzania yakaribia kuwa taifa la uchumi wa kati
Ndoto ya Tanzania kuwa nchi ya uchuni wa kati ifikapo mwaka 2025 ipo karibu kutimia.
Hayo yalisemwa jana na Dkt. Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Uchumi na Jamii (Economic and Social Research Foundation- ESRF) katika semina iliyoandaliwa kwa pamoja baina ya taasisi hiyo na Benki ya Dunia kujadili safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati.

Akizungumza katika semina hiyo, Dkt. Tausi Kida alisema kuwa hadi kufikia sasa pato la wastani la mtanzania ni dola za kimarekani (USD) 910 wakati inahitajika kwa taifa kufikisha kiwango cha pato la wastani la USD 995 kuwa taifa la uchumi wa kati.

“We are almost there – tumekaribia kabisa kufika” Kinachotakiwa sasa ni kuzidisha juhudi ili kasi ya ukuaji wa uchumi usishuke bali izidi kuongezeka – alisema.

Ili kuifikia lengo hilo, Dkt. Tausi Kida alishauri pia kufanyika mageuzi katika sekta ya kilimo kwa kuongeza tija sambamba na kuongeza usindikaji wa mazao ya kilimo hii ikiwa ni katika jitihada za kuondokana na kilimo cha kujikimu na kujikita zaidi katika kilimo cha kibiashara chenye kulenga mahitaji ya soko la ndani na nje.

Sambamba na hilo, Dkt Tausi Kida alishauri pia kuongeza uwekezaji katika rasilimali watu hususani kuboresha upatikaji wa huduma za afya, elimu na maji kama njia ya uhakika ya kuondokana na umaskini ifikapo mwaka 2025.

Akifafanua zaidi, Dkt Tausi Kida alieleza kwamba tangu mwaka 2000, Tanzania imekuwa ikitekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa (Development Vision 2025) inayolenga kuifikisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Dkt. Tausi Kida aliwaeleza washiriki wa semina kuwa dira hiyo imelenga kubadili uchumi wa Tanzania kutoka kutegemea sekta ya kilimo yenye tija ndogo na kuwa taifa lenye kutegemea zaidi uchumi wa viwanda na hasa viwanda vyenye kutengeneza bidhaa zenye ubora wa kumudu ushindani wa soko la kimataifa.

Akifafanua zaidi, Dkt Kida alisema kuwa Dira hii ya Maendeleo ya Taifa inalenga pia kuondoa kabisa umaskini nchini Tanzania ifikapo mwaka 2025. “It is envisioned that by 2025 abject poverty shall be something of the past – ni ndoto yetu kwamba ifikapo mwaka 2025 suala la umaskini litakuwa ni jambo lilipitwa na wakati nchini Tanzania” alisema.

Alieleza kwamba Tanzania imekuwa ikitekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa kupitia mikakati mbali mbali ikiwa ni pamoja na Mkakati wa Kwanza na wa Pili wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini nchini Tanzania – mikakati ambayo ilifahamika zaidi kwa jina la MKUKUTA na Mipango ya Miaka mitano mitano ya Maendeleo ya Taifa ambapo kwa sasa taifa linatekeleza mpango wa pili kwa kipindi cha miaka ya 2016/17 – 2020/21 alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird alisema kwamba Benki ya Dunia itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania uliojengeka kwa zaidi ya miaka 54 sasa.

Ushirikiano huu unalenga kuiwezesha Tanzania kuwa moja ya mataifa yenye uchumi mkubwa duniani. Bi Bella aliuambia mkutano kwamba katika miaka hiyo yote, Benki ya Dunia imekuwa ikitoa misaada ya kifedha kwa Tanzania hasa kupitia Shirika lake la Kimataifa la Fedha (International Development Association – IDA) ambalo limekuwa likitoa misaada katika nyanja mbali mbali hususani afya, elimu, hifadhi ya jamii, maji, nishati, uchukuzi, miji, mazingira, sekta za fedha na utawala bora.

Semina hiyo ilifanyika jana, Jumatano tarehe 21 mwezi wa 3 mwaka 2019 katika ukumbi wa mkutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Dhumuni kuu ya semina hiyo lilikuwa ni kujadili safari ya Tanzania katika kuekea uchumi wa kati. Semina hiyo ilichagizwa na mada iliyotolewa na ndugu Yutaka Yoshino, mchumi mwandamizi wa Benki ya Dunia ambaye alitoa mada juu ya uzoefu wa mataifa ya Vietnam na Bangladesh katika kufanya mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya viwanda ambapo yamefanikiwa kupiga hatua na kuwa mataiafa ya uchumi wa kati katika miaka ya hivi karibuni.

“Both countries were at the same level of per capita income as Tanzania in early 1990s – pato la wastani kwa mataifa haya lilikuwa sawa na lile la Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1990” alisema. Baadhi ya mataifa ya Afrika yaliyofanikiwa kutoka katika kundi la nchi maskini zaidi duniani na kuwa mataifa yenye uchumi wa katika miaka ya hivi karibuni ni pamoja na Ghana, Nigeria, Sudan na Zambia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida (kulia) akisalimiana na baadhi ya washiriki kutoka Ubalozi wa Ufaransa wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)-juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mtendaji Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird akiongozana na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano mara baada ya kuwasili kushiriki semina ya pamoja kati ya Benki hiyo na Taasisi hiyo juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mtendaji Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird akitoa neno la ufunguzi wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Mchumi wa Benki ya Dunia, Bw Yutaka Yoshino akitoa mada kuhusu safari ya Tanzania kuelekea uchumi kati wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Dr Jehovaness Aikaeli kutoka Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akielezea umuhimu wa umma na sekta binafsi kushirikiana kutokana uhaba wa rasilimali wakati wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark tawi la Tanzania, Bw John Ulanga (wa pili kushoto) akizungumzia ukosefu wa masoko nchini Tanzania ambao unakwaza ukuaji wa kilimo ambao ndio uti wa mgongo kwenye viwanda wakati wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida (kulia) akizungumzia umuhimu wa kuangalia rasilimali watu kwa kuzingatia weledi na elimu yao katika ushiriki wa kujenga uchumi wakati wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania CTI Bw. Subhash Patel (wa pili kulia) akizungumza sheria na vikwazo mbalimbali vinachangia kukwamisha ukuaji wa sekta binafsi wakati wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Bi. True Schedvin (kulia) kutoka Ubalozi wa Sweden alisema katika safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati ni vyema Tanzania kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo kazi, afya elimu na masoko wakati wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa washiriki akiuliza swali kwa wajadili wa mada wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano akifuatilia kwa umakini maoni yaliyokuwa yakiwasilishwa wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mtendaji Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird akifunga semina hiyo ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau wa maendeleo,sekta binafsi pamoja na taasisi mbalimbali za serikali waliohudhuria semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar

Source: Tanzania yakaribia kuwa taifa la uchumi wa kati - TradeMark East Africa
 
Wasira ndiye mtanzania pekee aliyefanya kazi serikalini kwa muda mrefu kuliko wote hapa nchini.
 
February 7, 2020

Washington, Maryland DMV
USA

Mpango mkakati wa Mh. Zitto Kabwe akipewa nafasi ya Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mpango mkakati wa Mh. Zitto Kabwe akipewa nafasi ya Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akijibu maswali ya waTanzania diaspora Marekani na wadau mbalimbali wa maendeleo waliotaka kujua Tanzania ya kesho inatambua changamoto gani zitatuliwe kiuchumi, kijamii na kisiasa nchi irudi tena katika reli ya taifa lenye umoja na uchumi imara.



Mh. Zitto Kabwe anaainisha matatizo ya serikali ya CCM Mpya jinsi isivyokuwa na Uongozi Mkakati wala kuongozwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

Mfano mradi mkubwa wa SGR reli mpya haukufuata Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na kusababisha kutochochea uchumi wa Tanzania. Na reli hii haina muda time frame utaisha lini pamoja yakuwa wahandisi wa reli walikadiria utachukua walau miaka 15 wakati CCM mpya walidhani utakwisha 2019.

Mh. Zitto Kabwe anaainisha umeme toka bwawa la Stiegler's Gorge maarufu kama Bwawa la Umeme la Rufiji mega watt 1 labda itaanza kuzalishwa na kuongozwa ktk gridi ya taifa mwaka 2030 subject to serikali itaweza kuendelea kuwalipa wakandarasi ktk muda muafaka na mikopo ya wadau wa maendeleo kupatikana kwa wakati.

Na miradi mingi mikubwa mingine imeanzishwa kwa matamko na pesa asilimia kubwa kulipwa kwenda nje ya nchi bila mikakati thabiti na kuzidisha kuyumbisha uchumi wa nchi na kipato cha mwananchi mmoja mmoja kiasi cha raia kulia ugumu wa maisha umezidi maradufu na pesa kukosekana mifukoni na mitaani.

Source : Mutwiba
 
February 10, 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Mwanasiasa mkongwe Ndugu Stephen Wassira anashusha madini kuhusu Uongozi wa kimkakati akihojiwa na watangazaji Sam Sasali, Hassan Ngoma na Babbie Kabae



Stephen Wassira ambaye zamani alipata kuwa kiongozi ktk nafasi ya uWaziri, mkuu wa mkoa, mbunge na afisa balozi Marekani anatumia uzoefu wake kuangazia wakati wa ukoloni, awamu baada ya uhuru za Nyerere, Mwinyi , Mkapa , Jakaya Kikwete na mikakati ya viongozi hao na hali ya sasa.

Stephen Wassira alibanwa kuhusu suala la Dira ya Taifa kukosa undelevu na kila kiongozi anayeingia madarakani huja na yake. Wassira akakumbushwa nchi kama Marekani dira ya taifa aje Rais mwingine au chama kingine iwe Republican au Democrats, Dira ya Marekani haiyumbi. Lakini kwa Tanzania kila kiongozi anayechukua mamlaka huja na jambo linaloitoa nchi kutoka ktk Dira mfano Kilimo Kwanza tatizo ni nini?

Watangazaji wanauliza kushirikishwa kwa wananchi ktk maamuzi makubwa na nafasi ya kuwepo hoja kizani ndiyo hujenga dira madhubuti itakayozingatiwa kila awamu na haitaathiriwa na mabadiliko ktk uongozi, je hali ya kisiasa na kijamii Tanzania inazingatia hilo?

Mfano Mradi mkubwa wa reli mpya ya SGR unaogharimu ma-Trilioni ya shilingi za kiTanzania unaonekana haupo ktk Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 iliyozinduliwa miaka 20 iliyopita , na Wassira anakiri haijulikani lini SGR Mpya itakamilika . Mradi huu umeanzishwa na CCM Mpya.

Wassira azungumzia fedha za World Bank za elimu na changamoto za jinsia / gender nini kifanyike mimba zipungue shuleni. Pia nini maana ya uzalendo na utaifa pamoja na misemo iliyozuka awamu hii kulinganisha na awamu zilizopita.

Stephen Wassira mahojiano yake yanajikita ktk taifa kuwa na Dira / Visheni anazungumzia juu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania 2025 toka taifa hili linapata uhuru na awamu zote za uongozi zilivyopambana na changamoto za nyakati zao kuhakikisha nchi inavuka na kuwa nchi ya uchumi wa kati ya viwanda na maisha bora zaidi kwa wananchi.

Source: CLOUDSMEDIA

Wassira amechoka apumuzike!!!!! Eti ameanza kupanga watu ili agombee tena Ubunge jimboni Bunda!!!!!
 
Back
Top Bottom