Stephen Wassira: Nimezipata habari kutoka Vatican na sio Tz

siasa zina vionjo vingi.


Wassira kaleta muziki unaokubalika kwenye siasa kama tunavyoweka vionjo vya Jk kuwa ni Vasco Da Gama wakati si kweli.
 
Inawezekana wassira ni usalama wa taifa wa VATICAN ndo maana kazipata habari hizo mapema kabla ya kardinali Rugabwa wa wakati ule.
 
how comes pesa zichangwe na waumini wa tanzania, au hata kama zimetolewa kutoka Vatcani zikaratibiwa tanzania, ufisadi ukafanyika tanzania halafu VATICAN wapate taarifa hizo mapema kabla ya tanzania. WASSIRA anazeeka vibaya.
 
Nazifahamu dawa wanazotumia wagonjwa wa akili,huwa zinasababisha baadhi ya watumiaji kusinzia ovyo ovyo. Mashaka yangu huenda Wassira ni mmoja wao.
 
Rais wa tuhuma Dk. Slaa ni mwalimu wa wassira kama hatakuwa profesa wake wa tuhuma.


Nani anaongoza kutuhumu wenzake kati ya wassira na Dk. Slaa?


Angalau Christopher Mtikila anajaribu kuwapeleka mahakamani anaowatuhumu.
 
Hii nchi ina vivutio vingi sana......
Nyerere aliamua kuanza kuweka vivutio vya Utalii pale ikulu,
Aliweka Tausi, ndege wazuri sana wale, akaweka hata ndege Mbuni...

Naona marais waliomfuata wameiga nyayo zake!! Kudos!!!

2011_rise_of_the_planet_of_the_apes_001.jpg
 
Rais wa tuhuma Dk. Slaa ni mwalimu wa wassira kama hatakuwa profesa wake wa tuhuma.


Nani anaongoza kutuhumu wenzake kati ya wassira na Dk. Slaa?


Angalau Christopher Mtikila anajaribu kuwapeleka mahakamani anaowatuhumu.
hivi tatizo ni nini hasa??
Mbona anasinzia hovyohovyo sana huyu kivutio wetu wa Gombe?

01-300x225.jpg
 
hii nchi ina vivutio vingi sana......
Nyerere aliamua kuanza kuweka vivutio vya utalii pale ikulu,
aliweka tausi, ndege wazuri sana wale, akaweka hata ndege mbuni...

Naona marais waliomfuata wameiga nyayo zake!! Kudos!!!

2011_rise_of_the_planet_of_the_apes_001.jpg

wanafanana!!!!!!!!!!!!
 
Wassira amewambia watu wa karibu yake kuwa amepokea waraka kutoka Vatican unaohusiana na Dr Slaa na kama wakatoliki hawalielewi hilo wafuatilie Vatican.
Hizi siasa za Wasira, sasa hazitofautiani na wanafunzi sekondari za O level ambao wanachafuana kutokana na teenager age zao wakati wakuchagua Kaka Mkuu na au Dada Mkuu..Nadhani pia anataarifa finyu sana na kuingiza maisuala ya kikanisa kwne siasa ni sawa na kudharau Kanisa Katiliki na maamuzi yake.
Pia mwenye thread hii ni vyema ungeleta maelezo ya kina kwenye jukwaa la dini,na sio dini na siana
 
hahaha kweli mzee ana akili za mbayuwayu, kaona ameminywa alete ushahidi wa alichokisema kaona aongezee uongo mwingine mkubwa zaidi, WASIRA AMEGEUKA SEKRETARI WA POP BENEDICT WA 11

huyu wasira hakuna kitu kichwani yeye kaona vatican ni mbali? siku hizi dunia ni kijiji pamoja na yote hayo bado kuna balozi wa vatican hapahapa bongo akija kukanusha atakuja kusema taarifa nimeipata tokea kwa mungu mbinguni, huyu kweli hamnazo
 
Huyu mzee ana matatizo sana,anatengeneza vurugu isiyokuwa na sababu.ni confuser tu huyu
 
Naona watu wanaingia kwenye Mtego kuona wa kulaumiwa ni Wassira. Huyu bwana hana cha kumlaumu kwa kauli zake maana yeye anaisemea CCM na kama ingekuwa sio hivyo CCM wangekanusha au kumfukuza kwenye kampeni.
Sasa kama CCM wako pembeni wanachekelea matamko ya Wassira ni wazi hayo ni matamko ya CCM.
Kama kanisa katoliki na waumini wake wanaona wamedharauliwa<basi aliye wadharau sio Wassira bali ni CCM nzima.
 
Kwa kweli Wasira na Mkapa hawakuwa na sababu za kuwatuhumu Dr Silaa na V. Nyerere kwa sababu wao si wagombea wa ubunge Arumeru mashariki hata kama tuhuma hizo zingekuwa za kweli. Walitakiwa kukituhumu chama na sera zake au dosari za mgombea wao. Hata Chadema nao wanatakiwa kujiepusha na kuongelea watu badala yake waongelee ubovu wa sera za CCM na uzuri wa Sera za CHADEMA na pia watawafanyia nini watu hata kwa kuwadanganya.
Wasira alihama CCM kuingia upinzani. Alishawahi kuituhumu CCM akiwa upinzani sasa leo njaa imemrudisha CCM baada ya kushindwa hata kulipa bili za maji na kupigana na watumishi wa idara ya maji Kinondoni baada ya kukatiwa maji.
Aache kumtuhumu Dr SILAA kwa sababu ubadilifu wake akiwa Serikali ni mkubwa kupindukia na tunaujua.
 
Habari Leo wanasema Wassira ...ameshawaomba radhi maaskofu...naamini katakiwaa afanye hivo,.....as of Vatican kuwahusisha kwenye siasa za ndani....muwakilishi wa papa atapeleka malalamiko rasmi ikulu na nchi itatakiwa kuomba tena radhi ,that is how uropokaji wa mtu mmoja can cost the country...

Hapo bado uingereza nao wAna malalamiko juu ya Mwigulu....Ccm iwapeleke viongozi wake kozi za diplomacy

Yote ya yote, lakini mimi bado na lia na kanisa,kwa akili yangu ndogo ya mtanzania wa kawaida kanisa kupitia matatizo ya wanasiasa haba/wasio na hofu ya Mungu,waongo,wanafiki,wachongeaji,wezi,wazandiki,wehu,wahuni,wasio jua neno ustaarabu ninini,wasio guswa na umaskini wa watanzania wenzao,wasio wanyenyekevu wa wapiga kura wao na majina mengineyo mengi ya kikafiri unaweza kuwapa je kanisa linajifunza nini kuhusu viongozi wetu hawa?

Ebu pata picha kama kweli kasema,manake kwa sasa tukisikia chochote kwa walio soma somo la Quantative Mathematics [QM] wanajua kuna hesabu za logic hivyo uwezekano wa Wasira kusema kauri ya mbaya huko wazi daima itakuwa ni statement yenye symbol ya T [TRUE].

Ila kwa hili Kanisa lishike Bango mpaka kieleweke manke aiwezekana Waziri mwenye dhamana ya mahusiano IKULU aseme amepata taarifa toka VATICAN,basi atakachosema kitakuwa na mantiki hata kama ALILOPOKA,kwa kuwa hatutegemei Mtendaji yoyote wa serikali au kichama mwenye dhamana hata ya kama ni ya mtendaji wa kata kulopoka yasiyo ya kweli kwenye jamii tutachukua kauri aliyotamka kama ndio kauri sahihi ya Serikali au Chama kwa kuwa maana ya dhamana ni madaraka yaliyokasimiwa mikononi mwake kwa mujibu wa sheria na ndio maana kuna viapo.

Sasa kama alikuwa analopoka akawataja VATICAN akifikilia iko Mbinguni hakika Kanisa muonyesheni kuwa KANISA ni zaidi ya SIASA ili liwe fundisho kwa wengine.Manake haiwezekani VATICAN wakatoa taarifa IKULU kwa Wasira pasipo kutuma nakara kwa mjumbe wa PAPA Tanzania na nakara nyingine kwa CAR-PENGO.Hata kama iliombwa kwa njia za kawaida ni lazima kungekuwa na kopi na vinginevyo wakati anatamka hayo ya DK-SLAA basi angesema kwa mujibu wa taarifa za kiintelejisia ili kupoteza mwelekeo kama ulikuwa ni mchezo wa siasa.

Tatizo CCM ni kuwa na watu wazima wasio waelevu na smart [Intelligent & Smart] sharp minded kwenye kubuni michezo ya siasa ,tunajua duniani kote kampeni nyingi zinaendeshwa kwa kulushiana vijembe ambavyo vingine ni vya kweli,ili kumvunja nguvu adui wake kisiasa,mfano mgombea mweusi wa Urais wa Republican J. Macain alilazimika kujiondoa kwenye mbio za urais kwa siri nyingi zake baadhi binafsi na nyingine za kutunga based on fact, basi akaonekana kweli jamaa atakuwa na matatizo na kina mama.Hivyo Macain kimya kimya akaona aachie ngazi mwenyewe basi maadui zake ambao waliona yeye ni tishio wakawa wamefanikiwa kumtoa kwenye race ya urais kimtindo dhamira yao ikawa imetia lakini katika njia ambayo ni kolofi kwa muhusika yenye ukweli wa muhusika japo umetiwa chumvi.

Sasa ili la viongozi wa CCM,pasipo kuwa na waataalamu wazuri wa kuengineer mambo yao yanayohusu umma,aimaanishi watalaamu wa darasani bali watu wenye elimu mahususi za kijamii ambao wanaweza kupanga mambo kwa ustaarabu na umakini pasipo kuacha kovu kwa mtu na kuaminisha umma na kampeni kufanikiwa pasipo kumgusa mtu mwingine waziwazi.Watu wa fani ya masoko [Marketers], Mahusinao ya Umma [Public Relation] ,wanasheria [Lawyers], Akili za watu [Psychologist] hakika ukichukua watu hawa ukaweka pamoja kama kikosi kazi [Task Force] ukawaambia kuspin na kuengineer jambo based kweye ukweli [fact] fulani fulani na hakika mtu achomoki na bado wadau wanao muhusu muhusika kwenye tukio wanabaki salama ila mlengwa inakula kwake.

Michezo hiyo inakubalika sana kwenye siasa,kwa kuwa ndio maana wanasiasa wanapaswa daima kuwa ni watu wenye kuishi ndani ya mwendenendo msafi usio tiliwa shaka hata kidogo.Lakini ili la wazee wenye elimu kiduchu, mwaka alobaini na saba kisha uspin mambo yapokelewe positive wakati hata mwenye ujui habari current za dunia jana na juzi zinasemaje.Kama mzee wasira alipata habari za kusikia toka kwa watanzania waliopata kuwa huko vatican, [hear say] kisha yeye kama kiongozi akaamua kuja kuzimwaga kwenye umma [public] tena akiwa kama kiongozi mwenye dhaman ya IKILU basi ni mtihani mkubwa sana kwa Seriali ya Kikwete kwa kuwa nina hakika Mawaziri wake wanajua diplomasia na mienendo yake mizima na kuwa dipolamasia ina protocol zake na hata utamkaji wa mambo yanayohusu mataifa hayo kwa viongozi wa kisiasa na kiserikali wa ngazi zote ni tofauti na unaozingatia unagalifu mkubwa sana.

Wasira asiwaone watoa taarifa JF akataka kujilinganisha nao, HAWA UKU NI genge la raia mitaani hawawakilishi Serikali yoyote,ili ni jukwaa [Forum] ya kijamii na ndio maana likaitwa JAMII FORUM na sio GOVERNMENT FORUM. Hivyo alipaswa kuwa mwelevu na makini [Intelligent and Smart] kuchukua taarifa kwenye jukwaa hili na kuzitumia kwa uangalifu pasipo kumdhuru mtu,kulikoni hii ya kulopoka sasa mpaka TAIFA nalo linakua kama LIMELOPOKA.
 
Back
Top Bottom