- Source #1
- View Source #1
JamiiCheck imefuatilia hotuba iliyotolewa na Stephen Wasira akiwa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa mkoani Mwanza tarehe 26-11-2024 ambapo mbali na mambo mengine alisema kuwa Rais Samia ameongoza kwa kipindi cha miaka minne, na pia serikali yake imejenga madarasa 986
- Tunachokijua
- Stephen Masato Wasira amekuwa mbunge wa jimbo la Bunda, lakini pia amewahi kuwa waziri wa wizara mbalimbali katika vipindi tofauti tofauti. Akiwa katika mkutano wa kampeni ya wagombea wa serikali za mitaa mwaka 2024 mkoani Mwanza, Wasira alipata nafasi ya kuhutubia wananchi waliokuwepo katika eneo hilo.
Mkutano huo ulikuwa ni wa kufungia kampeni ambao ulifanyika tarehe 26-11-2022 siku moja kabla ya uchaguzi wenyewe uliokuwa umepangwa kufanyika 27-11-2024. Wasira alizungumza na wananchi kwa ajili ya kuwaombea kura wagombea ambapo alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo takwimu ya vitu vilivyofanywa na Serikali.
Madai ya Rais kuwa na miaka minne kwenye uongozi wake
Wasira alidai kuwa hadi hivi sasa Rais Samia amefikisha miaka minne ya uongozi wake ambapo alisema “Kwa mfano katika miaka minne (4) sasa ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan”. Madai haya yanapotosha.
Rais Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na alishika kijiti kutoka kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano ambaye alifariki 17-03-2021. Rais Samia aliapishwa tarehe 19-03-2021 kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwaka huu 2024, March 19 Rais Samia alifikisha miaka mitatu kamili ya uongozi wake na hadi kufikia Wasira alipotoa madai hayo tarehe 26-11-2024 alikuwa ametimiza miaka 3 na miezi 8 ya uongozi wake na si miaka minne.
Madai ya shule mpya 986
Wasira alidai kuwa Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia shule mpya 986 zimejengwa ambapo kati ya hizo 467 ni shule za msingi na 579 ni shule za Sekondari.
Madai haya siyo sahihi kwani idadi ya jumla aliyotaja ni tofauti na mgawanyo alioutaja yaani idadi ya jumla amesema ni 986 ampapo za msingi ni 467 na 579 ni za sekondari ambapo ukijumlisha jumla inakua 1, 046 na si 986 kama ilivyodai. Lakini pia takwimu zake zinapishana na zile zilizopo kwenye ripoti yatakwimu za msingi ya mwaka 2023 kilichotolewa june 2024. Ripoti hiyo inabainisha onezeko la shule kuanzia mwkaa 2019 hadi 2023.
Kwa mujibu wa takwimu, kati ya mwaka 2021 na 2022 kwa upande wa shule za msingi, kumekuwa na ongezeko la shule za msingi za serikali 525, na kwa kati ya mwaka 2022 hadi 2023 kumekuwa na ongezeko la shule 282 ambapo jumla kati ya mwaka 20221-2023 kumekuwa na ongezeko la shule 807.
Kwa upande wa shule za sekondari kati ya mwaka 2021-2022 kumekuwa na ongezeko la shule za sekondari za serikali 209, na kwa kati ya 2022-2023 kumekuwa na ongezeko la shule 367 ambapo jumla ni shule 576.
Jumla ya shule zote zilizoongezeka kwa muda huo za msingi na sekondari ni 1,383
CHADEMA kusimamisha wagombea wachache tofauti na Malengo yao
Kwenye mkutano huu, Wasira alinukuu takwimu zilizotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Novemba 19, 2024 kuwa walipanga kusimamisha wagombea kwa 85% mijini lakini wakaishia 63% pekee, Vijijini kwa 60% lakini wakaishia 34% na Vitongoji kwa 60% lakini wakaishia kusimamisha wagombea kwa 31% tu.
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini madai haya yamepotoshwa. Mbowe alisema walisimamisha wagombea kama malengo yao yalivyokuwa lakini wengi walienguliwa na wasimamizi wa Uchaguzi hivyo kubakiza wagombea wachache ikiwa ni 63% pekee ya wagombea wote waliowasimamisha mijini, 34% ya wagombea waliosimamisha kwenye vijiji na 31% kwenye Vitongoji
Ushahidi wa alichosema mbowe upo hapa kuanzia dakika ya 42.