Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Toeni fact zenu zote lakini msisahau kuna kiumbe anaye iongoza hii dunia,
Jichunguzee kwanza ulivyo,haki utaamini uwepo wa huyo kiumbe
Hoja ni kuwa hicho kiumbe ndie mungu huyu wetu sote au nn?na kama ni kiumbe je chanzo chake ni nini huyo kiumbe?
 
Unavyoquote barua za biblia kama moral highground inaonyesha tayari huwezi fikiri nje yake.
Heshima ya utawala bora haitoki kwa mungu bali hutokana na serikali kuwa na maslahi sawa na majority ya raia.

Kuheshimu utawala kisa hadithi za biblia ni namna yakucontroll watu wasitetee haki na maslahi yao binafsi. pia ndio sababu ya kukwama kwa maendeleo ya kisayansi ulaya during the DARK AGE 1000AD-1400AD.
Hii kwasababu utawala wa MAPAPA uliona sayansi kama tishio kwa muelezo wa dunia waliotoa kwa watu. mfano kuzimu ,mbinguni ni wapi ? dunia inaumri gani? je kweli dunia ndio ipo katikati ya solar system? n.k

kama huyawahi kujiuliza vitu vya karatasi ya kwanza ya biblia. mimea iliumbwa kabla ya jua, je iliishije? hiyo NURU hapo mwanzo ulitokea wapi kama jua na nyota ziliumbwa siku ya nne? mungu hakujua JUA pia ni nyota? giza na mchana vilitokeaje bila JUA ? kama mungu aliumba mwezi kama mwanga mdogo jee inamaana mwezi una mwanga wake ? mbona kuna kupatwa kwa mwezi?
nashangaa watu wengi bado hawajajiuliza maswali niliojiuliza sekondari,

Vyombo vya dini vinapokea TAX REDUCTION mfano shule niliyosoma ST..,pia makanisa na misikiti hayalipi INCOME TAX huku yana uza elimu yakujirudia rudia kila mwaka na kuingiza kipato (sadaka) ndo maana vinapromote the status quo..

Matatizo ya ulaya ya 1300 AD ndo tunayo sasa Tanzania . Wengi humu ni part or symptom of the problem.

Tukiendelea kutumia vitabu vya karne 2000 zilizopita , hatuta weza kufanya reseach zakutransform maisha yetu in food , medicine , climate change ,judiciary n.k
Every scientific discovery is a nail in the religious COFFIN.
Hata marekani wavumbuzi ni atheists wengine wanakula matunda yao.
Kuna reseach evidence inayoonyesha jamii zenye dini ndizo maskini.

40% ya badget yetu ipo funded na donor countries ambapo kodi inayokusanywa kwenye prostitution ,night clubs na pornsites ulaya na marekani, INDIRECTLY inalipa mishahara ya WATANZANIA n.k sababu pesa ni pesa hakuna ya dhambi na safi..

HAHAH UKISEMA 1000 AD TAYARI UNAKUBALIANA NA BIBLIA TAYAR UNAKUBALI YESU YUPO ..TAYAR MUNGU UNAKUBALI YUPO.. BIBLIA IKO FIXED SANA ASEE
 
God Almighty is everything, he has power of controlling everything. His power has no limit

Kwa akili za kibinadamu hautoweza kumwelewa kamwe
Akiweza, atakuwa hawezi kubeba jiwe, asipoweza, atakuwa hawezi kutengeneza jiwe.

Vyovyote vile, Mungu muweza yote ni kamba tupu.
 
Akiweza, atakuwa hawezi kubeba jiwe, asipoweza, atakuwa hawezi kutengeneza jiwe.

Vyovyote vile, Mungu muweza yote ni kamba tupu.
Unataka kumjua Mungu asie na mwili wa hisia kwa kutumia akili za mwili wenye hisia.

It's very difficult my friend.

Hautopata validity kamwe.

Ikiwa tu mfumo wa jua wanasayansi wanakwambia upo kwenye Milk way ambao kiujumla kunako mifumo mingi sana ya sayari (galaxies) zisizo hesabika... hao ni wana sayansi wametumia vifaa vya hali ya juu na bado wanashindwa kutegua vitendawili vya mwanzilishi wa hayo yote, itakuwaje kwa ww usietumia vifaa.

Jaribu kutafakari jambo moja.... the tiniest particle iliyohusika kukuumba ww ilianzaanzaje....
 
God Almighty is everything, he has power of controlling everything. His power has no limit

Kwa akili za kibinadamu hautoweza kumwelewa kamwe
Thibitisha ulichoandika ni kweli na si hadithi za kutungwa na watu tu.
 
Unataka kumjua Mungu asie na mwili wa hisia kwa kutumia akili za mwili wenye hisia.

It's very difficult my friend.

Hautopata validity kamwe.

Ikiwa tu mfumo wa jua wanasayansi wanakwambia upo kwenye Milk way ambao kiujumla kunako mifumo mingi sana ya sayari (galaxies) zisizo hesabika... hao ni wana sayansi wametumia vifaa vya hali ya juu na bado wanashindwa kutegua vitendawili vya mwanzilishi wa hayo yote, itakuwaje kwa ww usietumia vifaa.

Jaribu kutafakari jambo moja.... the tiniest particle iliyohusika kukuumba ww ilianzaanzaje....
Thibitisha Mungu yupo awali ya yote.

Tiniest particle iliyohusika kuniumba mimi ilianzaje?

Unaelewa habari nzima ya mwanzo na mwisho ni mazingaombwe?

Unaelewa kwa subatomic particles zinazosafiri kwa spidi ya mwanga hakuna wakati uliopita, wa sasa na ujao na mambo yote yanatokea kwa pamoja na hivyo suala zima la muda halipo?

Unaelewa muda si kitu fundamental, kuna level ya ulimwengu ambayo muda haupo?

Unaelewa kwamba ukiondoa muda, habari ya causality na hiki kilianzaje inakufa?

Unaelewa kwamba hata nikiruhusu kila kitu kilicho complex kihitaji muumbaji, hilo litaonesha Mungu hayupo, si kwamba Mungu yupo?

Unaelewa niliyoandika hapo juu?
 
Unataka kumjua Mungu asie na mwili wa hisia kwa kutumia akili za mwili wenye hisia.

It's very difficult my friend.

Hautopata validity kamwe.

Ikiwa tu mfumo wa jua wanasayansi wanakwambia upo kwenye Milk way ambao kiujumla kunako mifumo mingi sana ya sayari (galaxies) zisizo hesabika... hao ni wana sayansi wametumia vifaa vya hali ya juu na bado wanashindwa kutegua vitendawili vya mwanzilishi wa hayo yote, itakuwaje kwa ww usietumia vifaa.

Jaribu kutafakari jambo moja.... the tiniest particle iliyohusika kukuumba ww ilianzaanzaje....
Nikikwambia Kipepe wa SANI ni Mungu asiye wa mwili wala hisia, na wewe huwezi kumuelewa kwa kutumia akili zako, ila ni Mungu.

Utakubali Kipepe wa SANI ni Mungu?
 
Kuna rais mmoja wa Marekani wa mwanzo kabisa, nafikiri alikuwa John Aadams yule, alisema wao wanayafanyia kazi masuala ya msingi kabisa yasiyokwepeka katika maisha ya kila siku (kula, pahala pa kuishi, afya, mambo ya kimsingi ya kiuchumi kama ajira etc) ili watoto wao wawe na luxury ya kuweza kuchambua masuala mengine (kama haya ya uwepo wa Mungu).

Tatizo kwetu huko wengi hawajatatua matatizo ya msingi, sasa kujadiliana na mtu ambaye hajapata muda wa kumsoma Anselm, Augustine, Russell, Dawkins, Hitchens, kwa sababu hata bajeti ya vitabu hana, au Kiingereza hajui kwa sababu hakufanikiwa kupata nafasi ya kujifunza, ni tabu sana.

Ndiyo maana nafikia nafasi hata kuonesha areguments za kutokuwepo kwa Mungu zinazotolewa na watu wanaosema Mungu yupo.

Hawana uwezo wa kufikiri kwa kina, muda wao mwingi unatumiwa kufukuza riziki ya siku.

Mtu anakwambia complexity ya dunia na viumbe ni lazima iwe imeumbwa, haiwezi kuwa imetokea yenyewe tu.

Hajui kwamba, kwa kusema hilo, anachosema kiukweli kabisa, ni kwamba Mungu muumba vyote hawezi kuwepo.

Kwa sababu, kama complexity ni lazima iumbwe, haiwezi kutokea tu, hata Mungu naye ni complex, naye atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, ad infinitum, ad nauseam.

Kwa hiyo, hapo hakuna Mungu muumba yote, kuna an infinity of viumbe.

Kwa hiyo Mungu hayupo.

Yani mtu anafikiri ananipinga mimi, kumbe anajipinga mwenyewe.

Kwa nini? Kwa sababu hajapata nafasi ya kuchunguza hoja yake kwa umakini kabla ya kuitoa, amejikita kwenye kufukuza riziki.
 
Kwann mnatumia AD?? Na BC?


Kama hutoweza kuprove vitu vyote vimetokea wapi..

Bas jibu ni rahisi sana ni Mungu...

Usijibizane na mm kama hutotoa maelezo kwamba vitu vyote vimetokea wapi...mana hoja zako zote zimemezwa hapo...

Mungu akubariki
tunatumia AD na BC sababu ni mfumo wa calendar ulioanzishwa na WARUMI na kusambazwa katika utawala wao ambapo ni modern Britain , Germany ,France, Italy ...nk..
hivyo huo mfumo unatumika sababu ya ukoloni. mataifa yaliyoweza kuunda calendar zao mf. CHINA , ETHIOPIA , hata wanamfumo tofauti ila ilikuelewana na majority ya dunia wanatumia both calendars.

kama unge google tu ungejua hili.

na wewe uliye chembe aliyeishi duniani miaka 50,000 kati ya miaka billion 4.51 ya dunia iliyokaribu na nyota moja kati ya billion 100 ndani ya milky way galaxy iliyo miongoni mwa galaxies zaidi ya billion 100. kwamba unaomba kiumbe flani kinacho elewa lugha yako , ufaulu mtihani,upate gari:):)

Basi endelea kuomba uwe maskini ili iwe rahisi kuingia ufalme wa mbinguni.
wengine hatupendi kuabudu acha tutafute maendeleo duniani.
 
Ni change hii Mada kidogo tu ! ni kwamba hakuna Hasi pasipokuwepo na Chanya , uchawi /Satan upo tangu kale ndivyo MUNGU yupo kabla ya Satan uchawi , Bin Adam tuna pande 2 tu kama humwabudu MUNGU unaabudu Shetani
 
Kuna kitu sikielewi..sawa yawezekana MUNGU hayupo ila kuna kitu nataka kuelewesha kama sio kufundishwa

Tunaenda kanisani ghafla katika maombi anatokea dada/kaka anapaza sauti anaruka juu anaongea maneno ya ajabu ajabu saingine analala chini na kuanza kutambaa kama nyoka..

Ghafla mchungaji/shekh akapofika hufanya maombi na kumtaja MUNGU na kila neno MUNGU likitamkwa inakua kama moto unachochewa lakini hadi mwisho muhusika huinuka na kuwa mzima.

Kama si MUNGU ni nani anaefanya mauponyaji ya namna hiyo? Kiranga
 
Kuna kitu sikielewi..sawa yawezekana MUNGU hayupo ila kuna kitu nataka kuelewesha kama sio kufundishwa

Tunaenda kanisani ghafla katika maombi anatokea dada/kaka anapaza sauti anaruka juu anaongea maneno ya ajabu ajabu saingine analala chini na kuanza kutambaa kama nyoka..

Ghafla mchungaji/shekh akapofika hufanya maombi na kumtaja MUNGU na kila neno MUNGU likitamkwa inakua kama moto unachochewa lakini hadi mwisho muhusika huinuka na kuwa mzima.

Kama si MUNGU ni nani anaefanya mauponyaji ya namna hiyo? Kiranga
Ushasoma kuhusu kitu kinaitwa "hypnotism"? Kama hujasoma, tafuta habari hizi zaidi.


Kimsingi, bado hatuelewi vizuri ubongo wa mtu unavyofanya kazi. Kwenye hypnotism, mtu mmoja anaweza kuwa controlled na mtu mwingine, bila hata kutumia habari za Mungu. Ni saikolojia tu.

Saikolojia ya watu wanavyofanya mambo katika crowd inaonesha kwamba ku control watu katika crowd ni rahisi, watu wana conform.

Nilikuwa naangalia comedy moja, comedian katunga habari ya uongo, anahadithia kama imetokea, akamuuliza mtu mmoja kwenye hadhara, uliisoma ile habari? Jamaa akakubali kaisoma. Akamuuliza uliisoma Washington Post au New York Times, jamaa akajibu Washington Post. Yani jamaa hakutaka kuonekana mshamba hajui habari mpya zinazoendelea. Hapo hapo yule comedian akamzodoa, akamwambia hiyo habari hujaisoma, acha uongo. Hujaisoma kwa sababu nimeitunga mwenyewe hapahapa sasa hivi. Mob psychology inamfanya mtu afanye mambo ya kijinga, ya uongo, akubali asichojua.

Pia kuna watu wanataka kuwa sehemu ya kitu kikubwa zaidi yao, wanajiaminisha kabisa kwamba wana mapepo (kwa kweli hatujui vizuri magonjwa ya akili, huenda pia wana magonjwa ya akili wasiyoyaelewa wanayaita mapepo). Kuna watu wametokea kuongea kwa lahaja tofauti kabisa (mfano Mmarekani aanze kuongea Kingereza kwa accent ya Uingereza). Hii hali inaitwa "Foreign Accent Syndrome". Soma zaidi hapa https://en.wikipedia.org/wiki/Foreign_accent_syndrome

Kwenye sayansi kuna watu wanapona kwa kile kinachoitwa "placebo effect". Yani unaweza kugundua dawa ya ugonjwa leo, ukawa na group la watu 300, ukawapa dawa watu 150 kila siku (namba si za kitaalamu, angalia dhana na hoja tu) halafu watu wengine 150 ukawapa vidonge vinaonekana kama dawa, lakini ni vidonge vya geresha tu, havina dawa. Wwanasayansi wameona mara nyingi kati ya wale waliopewa vidonge visivyo na dawa, wakiamini ni dawa, kuna wanaopona nao. Kwa sababu ya imani tu.

Huwa natania kwa kusema Yesu aliposema "imani yako itakuponya" alikuwa anasema kweli, alikuwa anazungumzia "placebo effect"

pla·ce·bo ef·fect
/pləˈsēbō əˈfekt,ēˈfekt/
noun

  1. a beneficial effect produced by a placebo drug or treatment, which cannot be attributed to the properties of the placebo itself, and must therefore be due to the patient's belief in that treatment.
    "orthodox doctors dismiss the positive results as a result of the placebo effect"

1.Kwa kweli, hatuelewi ubongo unavyofanya kazi.
2. Mimi sijawahi kukataa kwamba inawezekana Mungu yupo na ndiye chanzo cha haya
3. Mimi ninataka ushahidi wa kuonesha haya yanatokana na Mungu
4. Ushahidi huu haujatolewa
5. Watu wakiona kitu wasichokielewa, wanakimbilia kusema Mungu ndiye sababu, hata kabla uchunguzi wa kina
6. Kukimbilia huku kusema jibu ni Mungu, bila uchunguzi wa kina, ndiyo ninakukataa
7. Ulimwengu wenye magonjwa ya akili, mapepo, watu wanaopagawa etc una contradict dhana ya kuwepo Mungu mjuzi wa yote mwenye uwezo wote na upendo wote
8. Tutafute maelezo na uthibitisho kuhusu vitu tusivyovielewa bila kuhusisha uchawi, mujiza, Mungu kwanza.
9. Si lazima ujue jibu sahihi ili ujue jibu fulani si sahihi. Ukijua square root ya mbili ni ndogo kuliko mbili, huhitaji kujua square root ya mbili ni nini ili kujua kwamba kumi si square root ya mbili.
10.Tusome zaidi historia, saikolojia, baiolojia, kemia, jiografia, fizikia na hisabati kutafuta majibu ya maswali magumu yanayotukabili.
 
NAOANA UNAANDIKA KAMA UNATAKA KUSHUKA KITUONI KWENYE DALADALA..

HUJASEMA MAANA BC NA AC NI NA KWANN DUNIA NZIMA WANAKUBALI IVO..

KAMA MIAKA ILIANZA BILION HUKO KWANN WALIANZA UPYA NA BC NA AC..

HATA KAMA NI WARUMI ..KWANN WARUMI WAANZE KUTUMIA BC AC MDA HUO...

WEWE UMESEMA HUTAKI KUABUDU NDIO MANA UNAPINGA ..

MBONA HOJA YAKO NI NDOGO SANA ...KWAMBA KISA HUTAKI KUABUDU NA KUA CHINI YA SHERIA NA KANUNI ZA KIUNGU BAS UNAPINGA UWEPO....

..SABABU YAKO NIMEIELEWA..

AHSANTE SANA..
OK
 
Huyo Ngoswe unayetaka hawe na simu! Ni Ngoswe mpya au yule ambaye hakuwahi kutumia simu katika uhai wake?.Maana hata baba yangu aliyeishi miaka ya 1920 hadi 1985,hakuwa na simu.
Sijaomba namba za simu,nimeomba namba za mawasiliano.

Hata anwani ya sanduku la posta nayo ni namba ya mawasiliano pia.

Na historia inatuambia kuwa posta hapa nchini zimeanza kutumika miaka mingi tu kabla hata ya ujio wa kina Ngoswe.

Kwa hiyo acha kunilisha maneno ya kitu ambacho sijakisema.

Weka anwani ya mawasiliano ya Ngoswe hapa!.
 
Wapi nimesimama kwa kutumia mgongo wa Kiranga???! ,mimi nimetumia biblia yenu inayosema kuwa Mungu ni perfect(Mathayo5:48) halafu nashangaa kwa nini ashindwe kuumba dunia ambayo ni perfect, yaani isiyo na magonjwa, ubakaji, ajali, vimbunga, tsunami e. t. c!!


Na unapojinadi kuwa nisitumie verse moja kufikia conclusion ina maana hiyo biblia yenu inajikana yenyewe?.... yaani ina maana kuwa kama verse fulani inasema kuwa mungu ni perfect halafu kuna verse nyingine inakuja kukana??!
What is Perfect? Unawezaje kupima perfection?

Kungekua hamna ajali, magonjwa, mateso, n.k ungegunduaje kua ndo maximum level ya perfection kwnye maisha?

Negative things are there to prove the positive things, that's why there's Good and Bad, where we can measure the perfection.

Ukitaka kumtafuta Mungu wa kweli inakubidi uachane na Bad things first, ukishampata utapongezwa na tutasema ur a winner.
 
Back
Top Bottom