Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Kitu kimoja umetaja hapo cha "government sucks". Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuamini amini mambo kama ya kuwepo kwa Mungu na kupata uongozi mbovu.

Watu wanaoamini kuwapo kwa Mungu ni rahisi sana kuwa manipulate kisiasa na kuwashikia akili.

Ukisoma historia ya falme kubwa zilivyoweza kushika watu wengi, utaona katikati ya utawala wowote mkubwa, ni lazima kuwe na imani ya Mungu.

Wafalme wa Mesopotamia walitambua hili, Waisraeli walitambua hili, Wamisri walitambua hili, Wachina walitambua hili, Wagiriki walitambua hili, Warumi walitambua hili mpaka Constantine akaukumbatia Ukristo na kuhariri Biblia ya leo kwa sababu za kisiasa.

Mpaka ukija kwa watawala wa enzi hizi wakina George W Bush,Obama na Donald Trump wote wametumia dini kupata urahisi kutawala.

Na watawala wanajua kwamba watu wengi hawana muda wa kuchunguza vitu kwa kina, hivyo wanawanasa kwenye mtego wa "For God and Country".

Ndiyo hapo unapoambiwa habari za "fulani chaguo la Mungu". Wakitutajia Mungu tu, wanajua wengi wetu tunapeleka akili likizo!

Na hapo ndipo wanapopata nafasi za kupiga bila mjadala.

ndo serikali yetu ya sasa . wanamquote mungu kila sekunde wapatayo while wana abuse human rights and their constitutional powers , at the same time wamewaconvince a large group of people that they are doing it for the good of the country.
And they are succeeding because of people's prayers.. ! ! ! ! ! ! ! last time i believed in this was when i was 15 ,

its sad that there are adults who would rather you keep quiet than prove to them that their whole life philosophy is a lie.

Moreover they have been used and abused.
 
Nashukuru sana na nafurahi sana ninapoona kuna watu wengi wamefunguka macho kuona uovu na ujinga huu.
 
Hivi unamfahamu Kiranga kwenye hii mijadala ama unamsikia tu?

Wewe ndiye wakujipanga na ujipange kweli uwezavyo, japo bado najua utapelea parefu sana.

Wasiwasi wangu ni kwamba utatokomea mazima kama alivyotokomea Yesu wenu na akaahidi kurudi na hajarudi hadi leo.

Hakuna kazi ngumu kama ku defend haya maandiko uchwara mnayoambiwa ya Mungu.

Karibu udhalilike!!

First of all, sina sababu ya kumjua KIRANGA but I wanna make him avoid complacencies.
The man is too complacent kwa sababu ameridhika na mambo anayoyajua yeye na hayupo tayari kufundishwa wala kuelekezwa kitu ambacho hakijui.

Siwezi kutokomea kwa hoja nyepesi kama hizi Mkuu.

I'm ready to proceed defending Sir God against your claim.
 
When you have to shoot, shoot.

Don't talk.

Una point ya muhimu sana. Mtu mwenye njaa hana muda mwingi wa kuhoji uwepo wa Mungu.

Atasaka tonge kwanza, tena kwa kuomba Mungu.

Na ukimwambia Mungu hayupo, afanye kazi apate hela, anaweza kuona unamuwekea kijiba cha uchuro.

Ndiyo maana wengi wanapingana nami bila point.

Mtu katoka kusali kanisani apate kazi ili imsaidie kulisha familia yake, halafu unamwambia Mungu hayupo.

Unafikiri atafurahi?

Inabidi nicheke tu_kwaiyo mkuu si kwamba ukisemacho hakieleweki ila watu wanaogopa uchuro

Ila lina ukweli ndani yake
 
Kuna rais mmoja wa Marekani wa mwanzo kabisa, nafikiri alikuwa John Aadams yule, alisema wao wanayafanyia kazi masuala ya msingi kabisa yasiyokwepeka katika maisha ya kila siku (kula, pahala pa kuishi, afya, mambo ya kimsingi ya kiuchumi kama ajira etc) ili watoto wao wawe na luxury ya kuweza kuchambua masuala mengine (kama haya ya uwepo wa Mungu).

Tatizo kwetu huko wengi hawajatatua matatizo ya msingi, sasa kujadiliana na mtu ambaye hajapata muda wa kumsoma Anselm, Augustine, Russell, Dawkins, Hitchens, kwa sababu hata bajeti ya vitabu hana, au Kiingereza hajui kwa sababu hakufanikiwa kupata nafasi ya kujifunza, ni tabu sana.

Ndiyo maana nafikia nafasi hata kuonesha areguments za kutokuwepo kwa Mungu zinazotolewa na watu wanaosema Mungu yupo.

Hawana uwezo wa kufikiri kwa kina, muda wao mwingi unatumiwa kufukuza riziki ya siku.

Mtu anakwambia complexity ya dunia na viumbe ni lazima iwe imeumbwa, haiwezi kuwa imetokea yenyewe tu.

Hajui kwamba, kwa kusema hilo, anachosema kiukweli kabisa, ni kwamba Mungu muumba vyote hawezi kuwepo.

Kwa sababu, kama complexity ni lazima iumbwe, haiwezi kutokea tu, hata Mungu naye ni complex, naye atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, ad infinitum, ad nauseam.

Kwa hiyo, hapo hakuna Mungu muumba yote, kuna an infinity of viumbe.

Kwa hiyo Mungu hayupo.

Yani mtu anafikiri ananipinga mimi, kumbe anajipinga mwenyewe.

Kwa nini? Kwa sababu hajapata nafasi ya kuchunguza hoja yake kwa umakini kabla ya kuitoa, amejikita kwenye kufukuza riziki.

Hizi zarau sasa kwaiyo sie wengine utapiamlo unatusumbua ..
 
Jeff Bezos wa Amazon anamtaliki mkewe, katika talaka yao, Jeff anamuachia mkewe utajiri wa dola za Marekani takriban bilioni 35.

Na bado Jeff Bezos anabaki na utajiri wa dola za Kimarekani zaidi ya bilioni 100.

GDP ya Tanzania ya mwaka 2017 ni dola za Kimarekani Bilioni 52.

Utajiri wa mtu mmoja tu Jeff Bezos, baada ya kumtaliki mkewe na kumuachia utajiri wa dola za Kimarekani bilioni 35, ni takriban GDP ya miaka miwili ya nchi nzima ya Tanzania.

Yani uchanganye uchimbaji madini, utalii, kilimo na kila shughuli ya uzalishaji inayofanyika Tanzania, kwa miaka kama miwili mfululizo, ndiyo unafikia utajiri wa mtu huyu mmoja, tena baada ya yeye kupunguza utajiri wake kwa dola bilioni 35 kutokana na talaka.

Huyo mtu mmoja tu.

Halafu kuna watoto wanakufa vijijini Tanzania kwa sababu hawana chakula, hawana neti za kujikinga na mbu.

Halafu unaambiwa kuna Mungu anayetupenda wote sawasawa, ana uwezo wote na ujuzi wote.

Huyo Mungu yupo kweli au ni hadithi tu?
Mtu akifuatisha wewe anaweza kuacha kuamini mungu kiroho safi
 
Izi zarau sasa kwaiyo sie wengine utapiamlo unatusumbua ..
Kama dharau au si dharau ni jambo la kujadiliwa, inawezekana ufukara unasababisha "inferiority complex" mpaka mtu akikwambia ukweli unaona hii dharau.

Kwa hiyo unaweza kuambiwa ukweli, ukaona dharau.

Cha msingi ni, huo ni ukweli au si ukweli?

Inawezekana pia ikawa dharau unayostahili kwa haki na ukweli.
 
Mtu akifuatisha wewe anaweza kuacha kuamini mungu kiroho safi
"anaweza kuacha kuamini mungu kiroho safi" ni tungo tata.

Maana yako ni ipi?

Anaweza kuacha kuamini imani ya roho safi ambayo ni ya kuamini Mungu?

Au anaweza kuacha kuamini Imani ya kuwepo Mungu kwa namna ya roho safi tu?
 
Hakuna utata ni kwamba ataungana na wewe kimtazamo

Ila pia kuna shida ya kuwa na mtazamo kama huu wa kwako
 
Hakuna utata ni kwamba ataungana na wewe kimtazamo

Ila pia kuna shida ya kuwa na mtazamo kama huu wa kwako
Shida ipi?

Mbaraka Mwinshehe Kila kitu shida shida, shida haiishi mpaka siku ya mwisho.
 
Sasa hadi Hilo la watoto kufa njaa vijijini. Unataka umlaumu mungu? Si uwapelekee chakula
Jeff Bezos wa Amazon anamtaliki mkewe, katika talaka yao, Jeff anamuachia mkewe utajiri wa dola za Marekani takriban bilioni 35.

Na bado Jeff Bezos anabaki na utajiri wa dola za Kimarekani zaidi ya bilioni 100.

GDP ya Tanzania ya mwaka 2017 ni dola za Kimarekani Bilioni 52.

Utajiri wa mtu mmoja tu Jeff Bezos, baada ya kumtaliki mkewe na kumuachia utajiri wa dola za Kimarekani bilioni 35, ni takriban GDP ya miaka miwili ya nchi nzima ya Tanzania.

Yani uchanganye uchimbaji madini, utalii, kilimo na kila shughuli ya uzalishaji inayofanyika Tanzania, kwa miaka kama miwili mfululizo, ndiyo unafikia utajiri wa mtu huyu mmoja, tena baada ya yeye kupunguza utajiri wake kwa dola bilioni 35 kutokana na talaka.

Huyo mtu mmoja tu.

Halafu kuna watoto wanakufa vijijini Tanzania kwa sababu hawana chakula, hawana neti za kujikinga na mbu.

Halafu unaambiwa kuna Mungu anayetupenda wote sawasawa, ana uwezo wote na ujuzi wote.

Huyo Mungu yupo kweli au ni hadithi tu?
 
Sasa hadi Hilo la watoto kufa njaa vijijini. Unataka umlaumu mungu? Si uwapelekee chakula
Kama Mungu yupo kweli, yeye ni muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote.

Alishindwa kuumba ulimwengu ambao watoto hawawezi kufa na njaa?

Kama alitaka kuumba ulimwengu huo, ila hakuweza tu, je, ni kweli ana uwezo wote?

Kama aliweza kuumba ulimwengu huo, hakutaka tu, je, ni kweli ana upendo wote?

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, yupo kweli?

Au ni hadithi ya kutengenezwa na watu tu, isiyo na uhalisia?
 
Shida ipi?

Mbaraka Mwinshehe Kila kitu shida shida, shida haiishi mpaka siku ya mwisho.
Wewe huoni ulafi unaotengenezeka kwa jamii zisizo amini habari za Mungu unavotamalaki

Mtu anamiliki $100 million na bado anajiona masikini kila siku anatafuta

Wakat hata 1% ya pesa hiyo mtumishi wa kitanzania mwenye kuamini mungu anaweza akaacha kufanya kazi na kuimba haleluya mpaka anajifea kiroho safi_pasipo kuendelea kuinyonya jamii na kuipeleka puta
 
Kama aliweza kukugeuza wewe. Kutoka kwenye manii ya mzazi wako wa kiume. Yakaingia katika tumbo la Mama yako. Ukageuka ukawa kiumbe.
Kwanini ashindwe kuumba hivyo unavyodhani?
Hakushindwa Bali HAKUTAKA
Kama Mungu yupo kweli, yeye ni muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote.

Alishindwa kuumba ulimwengu ambao watoto hawawezi kufa na njaa?

Kama alitaka kuumba ulimwengu huo, ila hakuweza tu, je, ni kweli ana uwezo wote?

Kama aliweza kuumba ulimwengu huo, hakutaka tu, je, ni kweli ana upendo wote?

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, yupo kweli?

Au ni hadithi ya kutengenezwa na watu tu, isiyo na uhalisia?
 
Wewe huoni ulafi unaotengenezeka kwa jamii zisizo amini habari za Mungu unavotamalaki

Mtu anamiliki $100 million na bado anajiona masikini kila siku anatafuta

Wakat hata 1% ya pesa hiyo mtumishi wa kitanzania mwenye kuamini mungu anaweza akaacha kufanya kazi na kuimba haleluya mpaka anajifea kiroho safi_pasipo kuendelea kuinyonya jamii na kuipeleka puta
Naweza kujenga hoja kwamba, katika jamii zilizoendelea na kuwa na viwanda, Marekani ina watu wenye kuamini Mungu wengi zaidi kama asilimia ya watu wote kuliko nchi za Ulaya ya kaskazini.

Hii link inatupa figures za 2017 zikionesha Marekani wasioamini dini ni 39%, wakati Finland ni 55%.

https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_countries_by_irreligion

Na uwiano wa kipato kati ya masikini na tajiri uko vizuri zaidi katika nchi za Scandinavia kuliko Marekani.

US 18.5 Finland 5.6
https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_countries_by_income_equality

Ukiangalia hizo nchi zilizo most committed, ni nchi zilizoendelea ambazo Imani ya mungu ni ndogo zaidi ya nchi zilizo least committed ambazo zina Imani kubwa ya mungu.

Nchi ambayo inaendesha sovereign wealth fund vizuri kabisa ni Norway, wanatumia vizuri sana hela za mafuta yao. Hii ni huko Scandinavia ambako hawaamini Mungu sana, wanaamini watu kutumia rasilimali vizuri.

Huko wanakoamini Mungu sana Venezuela kwa mfano, nchi imebarikiwa mafuta lakini inaelekea ku collapse sasa. Kwa nini? Kila mtu anayepata nafasi anajilia yeye na Rafiki zake, wengine hawahurumii. Mkizidiwa ni mtaomba Mungu?

http://www.inequalityindex.com/

Most committed

1 Denmark (Global Rank #1)
2 Germany (Global Rank #2)
3 Finland (Global Rank #3)
4 Austria (Global Rank #4)
5 Norway (Global Rank #5)
6 Belgium (Global Rank #6)
7 Sweden (Global Rank #7)
8 France (Global Rank #8)
9 Iceland (Global Rank #9)
10 Luxembourg (Global Rank #10)

Least committed

1 Nigeria (Global Rank #157)
2 Uzbekistan (Global Rank #156)
3 Haiti (Global Rank #155)
4 Chad (Global Rank #154)
5 Sierra Leone (Global Rank #153)
6 Bhutan (Global Rank #152)
7 Madagascar (Global Rank #151)
8 Lao People's Democratic Republic (Global Rank #150)
9 Singapore (Global Rank #149)
10 Bangladesh (Global Rank #148)

Halafu, ni bora nchi ikawa an inequality ya masikini wengi wenye kuwa na basic needs zote, na matajiri wachache wenye utajiri wa kufuru, kuliko nchi kuwa na equality ya wananchi wote wako sawa lakini wote wana umasikini wa kutupwa wanagawana umasikini sawasawa.
 
Kama aliweza kukugeuza wewe. Kutoka kwenye manii ya mzazi wako wa kiume. Yakaingia katika tumbo la Mama yako. Ukageuka ukawa kiumbe.
Kwanini ashindwe kuumba hivyo unavyodhani?
Hakushindwa Bali HAKUTAKA
Unaweza kuthibitisha yupo, achilia mbali kwamba alinigeuza unavyosema?
 
Soma Aya ya 49
Unaweza kuthibitisha yupo, achilia mbali kwamba alinigeuza unavyosema?
Screenshot_2019-07-05-21-15-05.jpeg
 
kwa hyo unataka mungu aje mwenyewe akwambie kwamba yeye ndo mungu?
Hujathibitisha, unahubiri.

Sijaomba mahubiri, nimetaka uthibitisho.

Hata mimi naweza kuhubiri kwamba Comrade Kipepe, yule kibonzo wa gazeti la Sani, ndiye Mungu aliyeumba mbingu na dunia, na kaumba alivyotaka yeye.

Utakubali?
 
Back
Top Bottom