Step 10: Nilivyowekeza laki moja hadi kuanza kutengeneza milioni moja kila siku 3 (step by step)

Jun 8, 2016
83
645
Disclaimer (cha kuzingatia): This is not a get rich quick scheme (hauto tajirika ghafla ndani ya masaa au siku kadhaa), imenichukua mwaka kufikia wakati ambapo naweza pata faida ya millioni moja na kadhaa ndani ya siku 3. Nimejifunza mengi hapo kati, hopefully haitokuchukua mda mwingi kama mimi kwa ku avoid makosa yangu niliyofanya.

Cha kuzingatia kingine ni kwamba sifundishi mtu kutajirika wala kuwa na pesa nyingi hadi mwenyewe hutojua wapi pa kuziweka, nitachokua naelezea ni njia za wewe kujikwamua kutoka kwenye shida, kutohofia tena wapi hela za chakula, hela za kodi wala za mahitaji yako yote mengine ambayo ni ya muhimu zinapatikanaje. Naamini ukiweza ku solve mahitaji kama haya na uwe na milioni kadhaa benki kama savings, mtu anaweza aka focus kufanya mambo makubwa zaidi.

Kuanzia mwezi wa 12 mwaka 2014 nilianza ku experiment na kuagiza vitu kutoka China, nimekutana na malalamiko mengi ya watu kwenye research yangu kabla sijaanza, watu wanalalamika kuwa wanaibiwa mizigo yao haifiki, au wakiagiza mizigo inayofika inakua siyo yenyewe na yenye quality ndogo sana, nikasema ngoja nijaribu na mimi nione expirience yangu itakuaje, nikaweka pembeni laki moja kwa ajili ya kuagiza vitu tofauti, nilikua sijui chochote kuhusu ku import, nini kinahitajika wapi pa kuchukulia mizigo, unasubiri kwa mda gani hadi mzigo uupate, maswali yalikuepo kibao kabla ya kuanza. Ila nikajitosa tu na mtaji wangu huohuo mdogo.

Kwa kutumia laki moja, niliagiza kama vitu 15 hivi tofautitofauti vya bei ndogo, kati ya hivi 15, 13 vilifika.. 7 kati ya hivi 13 ndo vikawa kama nilivyotarajia na vyenye quality nzuri, kati ya hivyo 7 vitu vinne tu ndo nikaona vitaweza kuuzika, kati ya hivyo vinne viwili tu vikauzika. hivyo viwili, vikauzika na kuagiza vitano, vitano nikaagiza kumi, na kufikia sahivi naagiza mzigo wa hadi milioni 3 wa hiyo bidhaa kwa faida yake yenyewe ambayo sijaongezea hela za pembeni hata maramoja. Baada ya hiyo bidhaa moja kufanikiwa nikawa nimejifunza mambo mengi sana kuhusu kuagiza bidhaa na kuziuza kutoka nyumbani kwa kutumia mtandao tu.

Nikarudia hili zoezi kwa kutumia faida ya bidhaa ya kwanza, nikaagiza bidhaa mbili zingine, this time nikawekeza kama laki tano hivi kwa kila bidhaa, kati ya hizo mbili moja ikafeli, mabaki yake bado yame jificha kwenye kona moja nyumbani kwangu, bidhaa ya pili kati ya hizi ikafanikiwa na yenyewe, nikajifunza mengi zaidi kupitia hilo zoezi pia, jinsi ya kutengeneza demand ya bidhaa na kumaliza mzigo haraka zaidi, jinsi ya kujua bidhaa gani inahitajika kabla hata ya kuagiza, so sikuishia hapa nikajaribu bidhaa nyingine tena, kwa kutumia mambo yote niliyojifunza, this time i was right, mzigo wa piece mia ukaondoka ndani ya siku 3.

Kwa kutumia njia zote nilizojifunza nikafanikiwa kuanzisha biashara mbalimbali za mtandaoni, bidhaa mbalimbali tofauti na kuweza kuziendesha kwa muda wa mwaka na zaidi bila hasara yoyote, bidhaa zote ninazo agiza zinapata wateja kwa wakati muafaka, nikafikia kipindi nikaanza kuwa nauza hadi nchi za jirani kwenda kenya na Uganda, nikajifunza mengi pia kuhusu kusafirisha bidhaa nje ya nchi na kupokea malipo na mengine mengi. Sitoweza waonyesha biashara zangu zote kwa kuwa wengi wataiga and do the same, lakini ntajaribu kuwaonyesha moja wapo tu wa biashara ninazoendesha.

Turudi nyuma kidogo
Kwanini nmeamua kushare nnachokijua na wengine badala ya kuendelea kutengeneza hela tu na kuishi maisha yangu, well I enjoy writing sometimes nikiwa inspired, also moyo wangu unaniuma ninapoingia mtandoni na kuona watu wanalalamika kuwa maisha magumu, kuna mtu alipost JamiiForums kuwa ana mke na watoto mshahara wa laki tano then mimi bachelor nina uwezo wa kutengeneza laki tano ndani ya siku moja, kuna kitu moyoni mwangu haki kai sawa. Wengi wanalamika maisha magumu, hawawezi pangilia mshahara wao mdogo, wana hela ndogo hawajui wawekeze wapi na malalamiko mengi kibao nayapitia mtandaoni humuhumu kutoka kwa watu wanaotumia mtandao kulalamika badala ya kutafuta opportunities. Huku kuna baadhi ya watu wanatengeneza hala ya kumudu maisha huku wamekaa tu kwenye computer zao siku nzima.

Tuchukue mfano hapa chini
Hii smartwatch inayouzwa na mtu kutoka Jumia kwenye picha ya juu kwa tzs 120,000/= , ambayo ni the same smartwatch utayoweza kununua kutoka alibaba (cheki picha ya chini yake), site inayouza bidhaa kutoka china kwa bei nafuu ya 13.5$ ambayo ni sawa na karibia 30,000… at best case scenario huyu mtu ananunua kwa 30,000 na kuuza kwa 120,000 ambayo ni faida ya 90,000 kwa saa moja.. worst case analipia kodi mzigo ambayo takribani atakua ananunua kwa 50,000 ambayo faida itakua 70,000.

So kwa product kama hii inayopata faida ya 70,000, au tusiende kote huko, tuseme umeingia kwenye soko la kuuza smartwatch hizi na ukauza kwa bei ya elfu 80,000 ambapo wewe utapata faida ya 40,000 tuseme, unahitaji wateja 25 tu kwa mwezi kuweza fikisha faida ya milioni moja. Na uzuri wake hauto hitaji kuanza hata na smartwatch zote 25, unaweza ukaanza na moja tu, ikauzika then ukanunua mbili zikauzika, then tano, then 10, then 25. Ukifika 25 unaweza baki hapo maana umefikia target yako, na kuendelea kula faida ya milioni moja kila mwezi.

Tutachofanya hapa ni ku make sure hizo 25 (au kiasi chochote ulichonachi) zinaondoka ndani ya mda unaoupangilia na unaagiza mzigo mwingine kwa muda muafaka, kwa njia ntazokuja ziongelea target yetu ni kumaliza mzigo ndani ya siku 3 tu, 3 days, then siku zinazobakia unaagiza na kusubiri mzigo, huku unaendelea na kazi zako zingine. Kwa mtu wa kawaida, hautohitaji any other source of income ukiweza fikisha hii target kila mwezi.

So kwa kifupi bila kupoteza muda zifuatazo ndo step 10 unazoweza kuzifuata ili kufikia;

  1. Tafuta product ambayo itahitajika na watu kadhaa- huhitaji hata wateja wengi, kama product ina faida ya 20,000.. ukiwauzia watu 50 tu kwa mwezi una milioni moja. (Ambayo ni rahisi sana kupata watu 50 nitakuja kuongelea jinsi ya kupata wateja.)
  2. Testing phase, jaribu soko kama bidhaa utayoileta itahitajika na wateja
  3. Agiza kutoka China au nchi ambayo vitu vipo kwa bei rahisi (bila kupotea wala kuibiwa).
  4. Tafuta brand / jina la bishara yako (tengeneza logo/header photo n.k)
  5. Tengeneza outlet zako (social media accounts, facebook, twitter, instagram, website (siyo lazima lakini ni muhimu) pamoja na number ya simu na whatsapp itayokuwa hewani mda wote.
  6. Tafuta outlet zingine za kusambaza product (Jumia, kupatana,olx n.k) pamoja na groups za facebook.
  7. Jua msimu wa bidhaa zako/ jua mda na siku gani ambayo ni nzuri kutangaza bidhaa zako.
  8. Tangaza kwa bei rahisi kama utahitaji kufikia wateja wengi zaidi na haraka zaidi ( kwa kutumia matangazo ya facebook/instagram/google ads).
  9. Wapatie wateja bidhaa zao.
  10. Save contact za wateja ukipata bidhaa mpya unawatumia kwa whatsapp/message
Rudia hili zoezi kila mwezi

As simple as that. Hizo ndo step 10 unazohitaji ili kuweza kutengeneza an extra millioni moja kila mwezi, kwa mimi inachukua kama siku 3 (mara mojamoja hadi 4-5) kumaliza mzigo na faida ina vary from 800,000 – 1,500,000 ndani ya hizo siku kadhaa kwa bishara moja, ukiweza ku master process nzima unaweza ukarudia mara mbili au tatu na kutengeneza bishara zingine ambazo unazifanya kutoka nyumbani. So unaweza kuishia hapo na chukua hizi steps na uzifanye kazi.

Hii hapa moja wapo ya biashara inayotumia formula ya hapo juu
Nimejifunza mengi sana ndani ya mda wa miaka miwili ambayo siwezi kuaandika yote kwa wakati mmoja, nataka niifanye iwe course kwa ataehitaji, so kwa atae taka kujua undani wa kila step na mengine kama yafuatayo;

-Maelezo ya bidhaa za aina gani za kuagiza na misimu yake,

-Jinsi ya kutangaza kwa hela ndogo sana na kupata wateja wengi,

-Jinsi ya kujua suppliers wa uhakika ambao hawato kuibia na utapata mzigo sahihi kila unapoagiza

-Jinsi ya kupata atleast wateja 50 kila mwezi,

-Jinsi ya mtu yoyote kutengeneza website yake ya biashara na watu waweze kuweka orders mwenyewe kirahisi.
 
Kwanza hongera sana kuwa na moyo wa kushea nasi, unalofanya ni jambo jema ambalo hata katika vitabu vya dini unapata thawabu.

Nadhani wengi tunafahamu kuwa bidha uchina ni bei ndogo na wafanyabiashara wengi hupata super profit, tatizo la wengi ni ile namna ya kuagiza zikakufikia bila tatizo. Ungefunguka hapo utakuwa umetusaidia sana....cheers!
 
161 Reactions
Reply
Back
Top Bottom