Uchaguzi 2020 Ubunge Viti Maalum mkoa wa Dodoma ni vita ya vijana

Environmental Security

Senior Member
May 21, 2020
181
261
Habari wanajamvi

Katika kithibitisha mwitikio wa dhati kwa maono na uongozi wa chama cha mapinduzi CCM chini ya uongozi wa m/kiti Dk. John Magufuli wa kutoa fursa kwa vijana kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama na serikali, tayari hilo limedhihirika kwa vijana hasa wanawake kujitokeza ili kugombea nafasi za kuwawakilisha wananchi kwa kupitia nafasi za ubunge wa viti maalum,

Mathalan katika mkoa wa Dodoma tayari mchuano unaonekana kuwa mkali kati ya wagombea vijana, ambapo hadi sasa tathmini inaonesha mwanamama kijana jasiri na mchapakazi anayefahamika kwa jina la STELLA JASTON MKISI anaonekana kukubalika sana miongoni mwa akinamama wa CCM Dodoma, na hii ni kutokana na jinsi anavyotumia rasilimali zake katika kuihudumia jamii lakini hasa kinachowavutia wengi ndani ya CCM ni aina ya siasa anazofanya, ambapo amejikita katika kufanya siasa za kistaarabu zisizohusisha rushwa, matusi wala kuwagawa wanachama.

Pia, wanawake wengi wanavutiwa naye kutokana na kuchoka uongozi na siasa za mazoea na za kuwagawa wanawake ndani ya chama zinazofanywa na wagombea wakongwe hasa wabunge wa viti maalum waliopita ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiamini katika kutegemea kutoa fedha ili kushawishi wachaguliwe, na kushawishi wanawake wa CCM mkoa wa dodoma wasiwasikilize wagombea wengine.

Naona siasa safi ndani ya CCM ikianza kushika kasi na vijana wakiongoza katika kulithibitisha hilo kitu kinachofanya watu wenye siasa za kistaarabu kama STELLA JASTON MKISI kuwafanya wakongwe wakose usingizi wakihaha huku na kule na wapambe wao.

Viva vijana wa CCM; Viva STELLA JASTON MKISI

CCM imara
 
Ufafanuzi juu ya hiyo barua plz
tapatalk_1594495867679.jpeg
tapatalk_1594493990283.jpeg
 
Kwa anayemfahamu vizuri atujuze kuhusu mwanamama huyu jembe wa CCM anayetikisa wanasiasa wakongwe ndani ya mkoa huu wa makao makuu ya nchi yetu

Katika kuzunguka kwetu kujipitishapitisha ili kujitambulisha kwa wanachama, wajumbe na viongozi wa chama katika wilaya za mkoa wa dodoma, tumekutana na jina hili kwa upande wa viti maalum, linatajwa sana kiasi cha kufanya leo nitamani kumfahamu vizuri mwanamama huu

Naahidi kuwajuza wanajamvi taarifa zaidi kuhusu huyu STELLA JASTON MKISI mara ntakapomfahamu na wanajamvi mnaomfahamu mnijuze nitacompile na kuwajuzeni

Alamsiki

CCM imara
 
Mkuu salama!

Umesema mama ni JEMBE

Kuna aina mbili za majembe,

a) kuna jembe linaloingizwa mpini

b) kuna jembe linaloingia kwenye mpini

Yeye ni aina gani ya jembe kati ya tajwa hapo juu?

Katika maelezo yako umesema anatajwa tajwa

kama kiongozi mzuri na nk.

Mtajwa hapo anatumia aina gani ya uongozi kati

ya hizi:-

a) Bata

b) Kuku

Shukrani sana
 
Kama barua hii ni ya kweli basi kweli CCM ina matatizo katika kusimia demokrasia. Jibu la Magufuli kuhusu watia nia waliohamia CCM lilikuwa ni sahihi, lakini barua hii inaonyesha kupinga hilo.
1594505221973.png
 
Kipindi cha kushobokea watu hiki....
Kuwatafutia watu ulaji hiki.....

Ova
 
Back
Top Bottom