STEALTH (LOW OBSERVABLE) TECHNOLOGY | Teknolojia ya ndege kutoonekana/kutotambulika na rada (RADAR)

Uzi umeshiba sana safi Bila shaka wewe ni Telecom anyway mimi nataka kukuchalenge kidogo Technically Kwanza Radar inatumia Wave gani katika EM Spectrum?
Pili unasema Radar inaweza kudetect vitu kama mtu? Je radar mpaka ifanye detection Si lazima iyo kitu inayokuwa detected iwe ni Metallic? Au reflection inaweza hata kutokea katika Non metallic case na kama ni Yes nini maana ya kuwa na Ultrasonic sensors?
 
Uzi umeshiba sana safi Bila shaka wewe ni Telecom anyway mimi nataka kukuchalenge kidogo Technically Kwanza Radar inatumia Wave gani katika EM Spectrum?
Pili unasema Radar inaweza kudetect vitu kama mtu? Je radar mpaka ifanye detection Si lazima iyo kitu inayokuwa detected iwe ni Metallic? Au reflection inaweza hata kutokea katika Non metallic case na kama ni Yes nini maana ya kuwa na Ultrasonic sensors?
Karibu!

Nakushukuru kwa maswali yako mazuri lakini nitayajibu kwa kifupi ili tuweze kurejea katika muendelezo wa STEALTH ama LOW OBSERVABLE TECHNOLOGY.

Rada hutumia radio waves ili kuweza kubaini uwepo, umbali, kasi pia uelekeo wa vitu mbalimbali. Awali niliweka kirefu cha RADAR katika maelezo yangu na kwa kupitia hilo unaweza kugundua pia mawimbi yanayotumika.

Kuna aina nyingi za rada kuendana na mahitaji na matumizi. Sikuzitaja hapo awali kwa sababu nililenga zaidi kile nilichotaka kukielezea.

Si kila rada ina uwezo wa ku-detect ama kutambua chochota kile. Inategemea rada hiyo inafanya kazi gani na katika frequency zipi. Pia, si kwamba ni lazima kitu kiwe metallic ili kiweze kuwa detected na rada, la hasha, bali ni kile kiwango cha nishati kinachoweza kuakisiwa na kitu hicho ndicho kinachoamua uwezekano wa hicho kitu kuwa detected ama kutambulika na rada.

Kama kiasi cha nishati kilichoakisiwa ni kikubwa kiasi cha kuweza kurudi katika mifumo ya rada, kitu hicho kitaonekana kwenye rada lakini, kama kiwango cha nishati kilichoakisiwa ni kidogo sana kiasi cha kushindwa kurejea katika mifumo ya rada, ni vigumu kwa kitu hicho kuonekana ama kutambulika na rada.

Zipo rada ambazo hutumika hasa katika masuala ya ulinzi wa kawaida maeneo mbalimbali zenye uwezo wa ku-detect uwepo wa wavamizi na hata wapita njia katika kiwango fulani kifupi cha umbali na si zaidi ya hapo.
 
STEALTH (LOW OBSERVABLE) TECHNOLOGY | Teknolojia ya ndege kutoonekana/kutotambulika na rada (RADAR)

MUENDELEZO:

Hapo awali nilieleza kuhusu aina ama mbinu mojawapo ya kupunguza kitu kinachofahamika kitaalamu kama RADAR CROSS SECTION ama RCS. Tuliona ni jinsi gani maumbo (shapes) ya nje ya chombo yanavyoweza kutumika katika kukabiliana na mawimbi ya rada kwa kuyatawanya kuelekea katika upande ambapo hayawezi kunaswa na receiver ya rada. Wakati huu tuelekee katika mbinu nyingine ambayo hutumika katika kupunguza kiwango cha RCS.


2. Ufyonzaji wa mawimbi ya rada (RADAR ABSORPTION).

Hili hufanyika kupitia nyenzo maalumu zijulikanazo kitaalamu kama;

a) RADAR ABSORBENT/ABSORBING MATERIAL (RAM)
b) RADAR ABSORBENT/ABSORBING STRUCTURE (RAS)

Radar Absorbent Material ama kwa kifupi RAM pamoja na Radar Absorbent Structure ama RAS ni nyenzo ambazo hutumika katika kufyonza mawimbi ama signals zitokazo katika rada ili kuzuia ama kupunguza kuakisiwa kwa mawimbi hayo na kuyafanya yasirejee katika mifumo ya rada.

Kwa maneno mengine,

Radar absorbent materials and structures are designed to absorb radar waves and minimize or eliminate reflection.

Mbinu hii si mpya kwa maana ya kwamba imekuwepo muda mrefu sana na mpaka sasa yamekuwepo maboresho kadha wa kadha. Tafiti mbalimbali kuhusiana na mbinu hii zilianza mara baada ya uvumbuzi wa rada. Tafiti hizo zililenga kubaini tabia za mawimbi ya rada pindi yanapogonga katika vitu tofauti tofauti.

Wakati wa kipindi cha Vita Kuu ya Pili ya Dunia (WWII) mwaka 1939-1945, Ujerumani ilikuwa ikitumia mbinu mbalimbali za kuzifunika zana zake za kivita kwa kuzipakaa ama kubandika rangi maalumu ili zisitambulike ama zisionekane kirahisi na rada za upande hasimu.

Rangi hizo zilizokuwa zikifahamika kama Sumpf pamoja na Schornsteinfeger zenye kuweza kufyonza mawimbi ya rada, zilipakwa hasa katika nyambizi (submarines) ili kuzificha dhidi ya mifumo ya rada iliyokuwa ikitumika na ndege maalumu za kukabiliana na nyambizi (anti-submarine aircrafts). Toka kipindi hicho mpaka kufikia hivi sasa kumekuwa na maboresho makubwa ya nyenzo hizi hasa kwa kuzingatia ubora na viwango vya malighafi zinazotumika.

Nimeeleza hayo kwa ufupi ili uweze kufahamu kuwa mbinu hii imekuwepo miaka mingi na imekuwa ikitumika kwa kipindi kirefu kabla ya uboreshaji wake hadi kufikia hii leo.

Kabla hatujaendelea mbele zaidi, naomba niseme jambo moja.
Katika masuala yahusuyo mifumo ya kompyuta, kuna kitu hufahamika kama RAM yaani Random Access Memory. Lakini, katika masuala ya Aerodynamics pia kuna RAM ila, RAM ya upande huu ni kifupi cha Radar Absorbent Material ama Radar Absorbing Material. Nimelisema hili kama angalizo maana wakati nitapokuwa nikiendelea na maelezo kwa kutumia kifupisho RAM kusiwe na mkanganyiko kwa wasomaji katika kulitafsiri neno hili.

Sasa tusonge mbele.

Katika teknolojia ya kisasa, ndege huundwa kwa kupandikizwa mchanganyiko mbalimbali wa mifumo na vifaa vyenye nyenzo zenye sifa na tabia tofauti tofauti kimuonekano, kikemikali na kielektromagnetiki kwa lugha nyingine tunasema, different physical, chemical and electromagnetic properties. Mchanganyiko huo wa vifaa mbalimbali huhusisha nyenzo zisizo za chuma (metallic) ambazo uwezo wake wa kuakisi miale ni mdogo sana.

Kutokana na hilo, mawimbi ya rada huweza kupenya ndani ya vifaa hivi na kusababisha kuakisiwa kwa mawimbi hayo kutokea ndani badala ya nje hivyo kupelekea chombo kizima kugundulika kupitia vifaa vilivyomo ndani. Ili kukabiliana na hili, rangi maalumu zenye RAM hupakwa katika sehemu mbalimbali za nje ama kwa lugha nyepezi 'bodi' ili kuzuia signals au mawimbi ya rada kupenya ndani ya vifaa vinavyounda mifumo mbalimbali ya ndege.

04082_cockpit_1.jpg


RAM hufanya kazi ya kufyonza signals za rada na kuzidhoofisha kwa kubadili kiwango kikubwa cha nishati yake kuelekea katika joto (heat) ambalo hupozwa huku kiasi kingine cha nishati kilichobaki kikipoteza ubora ama nguvu yake hivyo kupelekea kushindwa kurejea katika mifumo ya rada.

Kwa maelezo mengine,

RAM technology is based on the idea of establishing desirable impedance which poses good and absorbing qualities, so that the RAM can accept and then attenuate the incident wave.

Miongoni mwa malighafi zitumikazo katika hizi rangi maalumu zenye uwezo wa kufyonza mawimbi ya rada ni Reinforced Carbon-Carbon (RCC) pamoja na kampaundi (compounds) nyinginezo kama vile Epoxy Resins, Urethane, Polyetherimide pamoja na Ferrite.

Kampaundi kama vile Ferrite pamoja na Carbonyl Iron zimekuwa zikitumika kutengeneza RAM maarufu sana inayojulikana kama Iron Ball Paint yenye chembe ndogondogo kama majivu, chembe zijulikanazo kama 'iron balls' ambazo hutumika katika kupakaa sehemu za nje za ndege na vyombo vingine ili kuvipatia uwezo wa stealth. Iron Ball Paint imekuwa ikitumika kwa muda mrefu sasa ikitumika pia hata katika ndege maarufu za zamani kama vile F-117A Nighthawk.

54085f3ac2b58cd452809ccf2860e74f.jpg

CIP-N1.jpg

PICHA No.1: Carbonyl Iron inayotumika katika rangi maalumu ya RAM inayojulikana kama Iron Ball Paint.
PICHA No.2: Chembe ndogondogo 'iron balls' katika muonekano wa karibu zaidi kupitia hadubini.

Katika mchoro ufuatao, tazama hapo jinsi signals za rada (INCOMING RADAR BEAM) zinavyoweza kufyonzwa na RAM kwa kugongana na chembe ndogondogo za Carbon au Ferrite (CARBON OR FERRITE PARTICLES) kisha kuakisiwa ndani kwa ndani na hatimaye kupoteza nishati yake na kushindwa kurudi katika rada.

fggfgfgfgf.png


Nimekwisha kuzungumza zaidi kuhusiana na RAM yaani Radar Absorbent Material lakini kuna kitu kingine nilidokeza hapo awali kinaitwa RAS ama Radar Absorbent Structure.

RAS hufanya kazi ile ile ya kufyonza rada lakini nyenzo hii tofauti kidogo na kule tulipoona awali kuhusiana na rangi maalumu zitokanazo na RAM. Kwa upande wa RAS ama Radar Absorbent Structure, zenyewe ni RAM pia ambazo hutengenezwa katika shapes ama miundo mbalimbali ili kuweza kupunguza nguvu za signals za rada pale zitakapokuwa zikigonga katika hiyo miundo ama structures.

Laird-ABS-IMG-RFFOAM- Flexible-and-Structural-Radar-Absorbing-Foam-1-102814.jpg


Aina mojawapo ya RAS ambayo ni maarufu sana hufaamika kama Foam Absorber. Nyenzo hii hutengenezwa kwa mchanganyiko wa kampaundi mbalimbali kama vile Urethane pamoja na Carbonyl Iron au pia Graphite kisha kukatwa katwa katika shapes zenye vipimo maalumu kuendana na mahitaji. Moja ya RAS zitumikazo hasa katika kufyonza mawimbi ya rada kama foam absorber ni hii hapa inayofahamika kama Pyramidal RAM kama inavyoonekana katika picha mbili zifuatazo;

960px-Anechoic_chamber_wall.jpg

3640-PU-Foam-based-pyramid-absorber-main-image.png


Kama unavyopata kuona hapo, ni aina fulani ya muundo ufananao na piramidi kama zile zilizojengwa zamani sana nchini Misri lakini hizi za hapa ni ndogondogo zenye ncha kali na vipimo maalumu ambazo zote kwa pamoja huunda kitu kinachoitwa Pyramidal RAM kama nilivyodokeza hapo awali.

Pyramidal RAM hufanya kazi ya kuziakisi signals za rada zaidi ya mara moja kwa kuzitawanya kinyume na uelekeo wake katikati ya piramidi moja na nyingine katika mtindo unaofahamika Kifizikia kama scattering. Signal ya rada inapogonga katika piramidi moja huakisiwa kuelekea katika piramidi nyingine ya karibu kisha huakisiwa kwa mara nyingine kurudi katika piramidi ya awali na kuendelea na mtindo huo mara kwa mara ambapo kila mara signal inapoakisiwa hupoteza kiasi fulani cha nishati yake.

Scattering hutokea pale ambapo kiwango chochote cha mwanga, sauti ama chembe (particles) zilizo katika msafara zinapolazimishwa kubadili uelekeo wake kutoka kule zilipokuwa zikielekea awali kutokana na kugonga vikwazo mbalimbali katika nyenzo zinapopita ama kusafiria.

Kwa maelezo mengine,

Scattering, in physics is a change in the direction of motion of a particle because of a collision with another particle. Or is the process in which a wave or beam of particles is diffused or deflected by collisions with particles of the medium that it traverses.

Kama nilivyosema hapo awali, mtindo huu wa utawanyaji unaofahamika Kifizikia kama scattering huzifanya signals kupoteza nishati pale zinapobadilisha uelekeo mara kwa mara wakati zinapokuwa zikigonga katika piramidi. Kivipimo, urefu kati ya base na ncha ya piramidi pia upana wa bases za piramidi huzingatiwa kuendana na mahitaji ya wavelength. Piramidi huwa nyembamba zenye ncha zaidi na kutokana na hilo, huzifanya signals za rada kuweza kuakisiwa mara nyingi zaidi katikati ya piramidi kuelekea katika bases ama chini ya piramidi.

Katika mchoro ufuatao unapata kuona jinsi muundo huu wa piramidi ufanyavyo kazi ya kuziakisi signals za rada mara kwa mara na kuzitawanya ndani kwa ndani.

hgrrffd.png


Miundo hii hubandikwa sehemu mbalimbali za chombo mathalani ndege ili kukipatia uwezo wa stealth, katika pembe mbalimbali, sehemu za mabawa, fuselage na pia zaidi ndani ya bodi tofauti na rangi za RAM ambazo zaidi hupakwa sehemu za nje. Katika uwekaji ama ubandikaji wake, upande wenye ncha huelekezwa upande signals zinapotokea.

Maelezo ni marefu kidogo lakini bila shaka yanaeleweka vyema.

Wakati tukielekea ukingoni,
Wataalamu mbalimbali wamekuwa wakija na maboresho katika mbinu hizi za ufyonzaji wa rada kadri miaka inavyozidi kwenda, ili kuweza kuendana na mahitaji ya muda. Pia, suala la maintenance ama marekebisho ya hapa na pale limekuwa ni jambo linalozingatiwa sana hasa katika vyombo vilivyopo na vinavyoendelea kutumika huku pia kukiwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vyombo hivyo vinabaki kuwa katika ubora wake wa stealth.

Baadhi tu ya maboresho hayo ni kama ifuatavyo;

Kampuni maarufu ya teknolojia za kijeshi na masuala ya anga Northrop Grumman ya nchini Marekani, imekuwa ikitekeleza miradi mikubwa inayohusu teknolojia hii ya stealth kwa muda mrefu sasa. Kutokana na changamoto mbalimbali hasa katika masuala ya maintenance ya zana na vyombo vya kijeshi vinavyotumia teknolojia hii ya stealth hasa ndege za kivita, kampuni hiyo imekuwa ikija na mbinu ama nyenzo za kukabiliana na changamoto hizo.

Mnamo mwaka 2004, kampuni hiyo (Northrop Grumman) ilikuja na nyenzo mpya baada ya kuwepo kwa ugumu ama changamoto kubwa katika mchakato wa kuirejesha RAM iliyokuwepo katika sehemu mbalimbali za ndege za stealth mara baada ya marekebisho kadha wa kadha (maintenance) kwa sababu kabla ya maintenance, RAM huondolewa katika baadhi ya sehemu zenye uhitaji wa maintenance kisha hurudishiwa baadaye baada ya kumalizika kwa maintenance.

Kutokana na changamoto hiyo, kampuni ilibuni nyenzo inayofahamika kama Alternate High-Frequency Material ama kwa kifupi AHFM. Hii ni rangi maalumu ambayo ilileta maboresho makubwa sana katika teknolojia ya stealth na ilitumika kwa mara ya kwanza katika ndege maarufu za mashambulizi mazito aina ya B-2 Spirit.

B-2 spirit stealth bomber.jpg

maxresdefault (1).jpg

PICHA: Ndege ya kijeshi aina ya B-2 Spirit mahususi kwa ajili ya mashambulizi mazito (bomber).

Hapo kabla marekebisho ya RAM katika ndege hizi yalikuwa yakichukua muda mrefu sana huku yakifanyika hasa kwa mikono lakini kwa ujio wa AHFM, kuliweza kupunguza muda wa maintenance kwa kiasi kikubwa ambapo nyenzo hii iliweza kuwekwa kwa ufanisi zaidi kwa kutumia mitambo maalumu ama 'robots'.

Maboresho katika teknolojia ya stealth kama tulivyokwisha kutazama toka mwanzo, yamekuwa yakijumuisha mbinu mbalimbali ambazo hutumika kwa pamoja kuendana na mahitaji ili kuweza kukipatia chombo uwezo wa stealth. Ili kutekeleza haya, kumekuwa na juhudi kubwa ikiwemo matumizi ya rasilimali nyingi katika uwekezaji wa teknolojia hii katika wakati huu wa sasa na hapo baadaye.

Mpaka kufikia hapa, natumai mtakuwa mmepata kufahamu kuhusiana na teknolojia hii kwa kiasi fulani jinsi ilivyo na ufanyaji kazi wake. Nawashukuru nyote kwa ufuatiliaji ama pia usomaji wenu tangu mwanzo hadi kufikia hapa. Kwa maoni au maswali, karibuni sana.


FRANC THE GREAT,
Semper magnas.
 
Unazungumzia ndege iliyotunguliwa lakini, hicho si kile kinachozungumziwa hapa kwa sasa.

Kama nilivyokuambia, kinachozungumziwa hapa ni kuhusiana na STEALTH ama LOW OBSERVABLE TECHNOLOGY kwa ujumla wake na si kuhusiana na chombo fulani cha anga in particular.

Maelezo haya yatapata muendelezo wake hapo baadaye na tutakapopata wakati wa kuchambua kwa undani kuhusu vyombo mbalimbali vya anga, tutapafikia hapo unapopasema.
Ahsante kwa majibu mazuri alitaka kubadili maudhui ya uzi
 
Asante mkuu, nimeisoma yote na kujijibu maswali ambayo nilikuwa najiulizaga sana kuhusuana na hii technology.
Swali langu inakuwaje kuna muda hizi Stealth zinakuwa detected kwenye radar?
 
Ubarikiwe sana kwa elimu hii uliyotupa kuhusiana na haya mambo

Naomba kufahamishwa kuhusu jambo hili: kuna tv show ya kimarekani inaitwa The Last Ship.. katika series ile kuna episodes zinaonesha uwezo wa marekani katika medani za vita ikiwemo vita ya majini.. sasa katika meli ile ya jeshi la marekani walikuwa wanazima baadhi ya mitambo,wanapunguza mwendokasi wa meli pamoja na kuzuia movements za wanajeshi ndani ya meli kwa lengo la kutoonwa na maadui kupitia rada.. na sekunde chache baada ya kufanya zoezi lile chombo cha maadui kupitia rada walishuhudia meli ile ikitoweka katika screen ya rada..

Je hii ni kweli kufanya vile kunasaidia rada ishindwe kutambua chombo kile? Au ni kutia chumvi tu katika teknolojia??..Nawasilisha swali.
 
PICHA: Muundo wa stealth wenye maumbo kama 'msumeno' kwa ajili ya kuyatawanya mawimbi ya rada, kwenye mlango wa 'landing gear' katika ndege ya stealth ya F-35.

2-stealth-design.jpg

fgfgdgersrsdfdx.png
 
Mkuu umefanya vema kasoro kosa la kwanza uliloonesha B1B Lancer ni stealth, hiyo si stealth hata kidogo. Long range bombers ambazo ni stealth ni kama B-2 na hiyo B-21 zote kutoka kwa Northrop Grumman.
 
Asante mkuu, nimeisoma yote na kujijibu maswali ambayo nilikuwa najiulizaga sana kuhusuana na hii technology.
Swali langu inakuwaje kuna muda hizi Stealth zinakuwa detected kwenye radar?
Nakushukuru kwa kusoma pia kwa kuuliza swali zuri na la muhimu.

Dhumuni kubwa la stealth technology ni kupunguza kiwango cha radar cross section. Maana yake ni kwamba, stealth inaweka ugumu wa chombo kuwa detected na rada kwa kuzuia mawimbi ya rada yasiweze kuakisiwa kurudi katika rada. Lakini pamoja na hilo, kuna baadhi ya visababishi vinavyoweza kupelekea mawimbi ya rada kuakisiwa na kurudi kwenye rada pamoja na kuwa chombo kilichoakisi mawimbi hayo ni chombo stealth.

Kuna factors ama sababu mbalimbali ambazo zinaweza kupelekea stealth kuwa detected kwenye rada.

1) Sababu ya kwanza ni chombo chenyewe.
Kuna vyombo ambavyo vimewezeshwa kuwa na mchanganyiko wa mbinu mbalimbali ama kadha wa kadha za kuvipatia uwezo wa stealth. Pia, kuna baadhi ya vyombo kutokana na mahitaji na masuala mengine mbalimbali, vimepatiwa uwezo kidogo.

Baadhi ya vyombo hupatiwa uwezo kidogo wa stealth kutokana na mambo mbalimbali:

Kwanza ni gharama. Teknolojia ya stealth ni teknolojia yenye gharama kubwa na huhitaji rasilimali nyingi sana katika kuifanyia kazi ipasavyo. Hivyo katika baadhi ya vyombo, mbinu ya stealth mojawapo au baadhi ya mbinu chache hutumika. Kwa maana hiyo, katika viwango fulani vya kiutambuzi kupitia rada, kuna uwezekano wa chombo hicho kutambulika.

Pili ni katika masuala ya kiufundi. Katika suala la ku-design maumbo mbalimbali ya ndege ili yaendane na teknolojia ya stealth, kuna vitu mbalimbali lazima vizingatiwe. Umbo la nje la ndege ama chombo chochote cha anga lina mchango mkubwa sana katika upaaji na mwenendo wa chombo husika kwa ujumla pale kinapokuwa angani.

Hivyo, katika ku-design umbo litakaloweza kuendana na teknolojia ya stealth yaani, kuhakikisha kuwa umbo hilo linayatawanya mawimbi na si kuyaakisi kuelekea katika mifumo ya rada, ni lazima pia umbo hilo lizingatie masuala mengine ya anga ili chombo kiweze kuwa na mwenendo unaopaswa pale kiwapo angani. Kwa maana hiyo kuna zoezi la ku-balance hapo kati ya stealth na aerodynamics.

Kwa maana hiyo, wataalamu wanalazimika ku-limit baadhi ya vitu katika baadhi ya vyombo vya anga (si vyote) ili kuweka uwiano kati ya mambo hayo mawili. Kuhakikisha kuwa kwa kiasi chombo kiwe stealth na pia kiweze kusafiri katika viwango na mwenendo unaotakiwa kuendana na aina ya chombo husika. Kutokana na ku-limit ama kupunguza baadhi ya vitu hasa katika upande wa stealth, kunaweza kusababisha udhaifu fulani na kusababisha sasa chombo husika kutambulika kupitia viwango fulani vya kiutambuzi katika rada.

2) Sababu ya pili ni aina za rada zinazotumika.
Kuna baadhi ya rada zina uwezo wa ku-detect stealth lakini katika viwango fulani tena hasa umbali. Hapo awali nilisema kuwa stealth hukifanya chombo kuwa na radar cross section ndogo, kisiweze kuonekana kirahisi ama kutambulika na mifumo ya rada ama kwa maneno mengine, LOW OBSERVABLE.

Iko hivi,

Mifumo ya rada hufanya kazi katika viwango tofauti tofauti kuendana pia na kazi ama jukumu maalumu lililokusudiwa.

Katika viwango fulani vya rada, tunaweza ku-detect hata vitu vidogo zaidi vilivyopo angani kama vile njiwa. Lakini, mifumo hii ya rada hasa za ku-detect ndege za kivita na za kawaida hufanya kazi ya kuchuja (filtering) baadhi ya vitu hasa vile vidogo sana na kuvifanya visionekane katika mifumo hiyo kupitia software maalumu ili kusiwe na mkanganyiko katika utambuzi. Hilo lisipofanyika vizuri, kunaweza kupelekea utambuzi wa vitu vingine lukuki ama vingi sana kwa wakati mmoja katika eneo lengwa hatimaye kushindwa kubaini kile kilichokusudiwa.

Sasa hapo ndipo teknolojia ya stealth inapofaidika napo.

Kupitia teknolojia ya stealth, ndege kubwa kabisa iliyopo umbali fulani inaweza kupunguzwa radar cross section yake na kuwa na radar cross section kama ya njiwa ama chini ya hapo. Maana yake ni kwamba kiwango hicho kidogo cha radar cross section automatically kitachujwa na mifumo ya rada hatimaye kupelekea ndege hiyo kutotambulika kirahisi. Hivyo, katika viwango fulani vya rada, ndege yenye uwezo wa stealth inaweza kuonekana ama kujitokeza (appear) kwenye rada lakini isitambulike kutokana na mkanganyiko huo wa radar cross section.

Kingine kinachoambatana na hilo, mifumo ya rada inaweza kufanya kazi katika umbali fulani na si zaidi ya hapo. Kupitia viwango fulani vya stealth kuna uwezekano wa kupunguza hiyo range kwa kiasi kikubwa. Maana yake ni kwamba, mfumo wa rada unaweza kuwa na uwezo wa ku-detect vyombo vya anga katika umbali mathalani wa hadi kilometa 400 lakini kupitia teknolojia ya stealth, chombo kikaonekana ndani ya kilometa chache tu ya hizo kilometa 400. Hicho tayari ni kikwazo kwa rada, maana kama chombo kilichopo angani ni chombo cha adui, kinaweza kufanya tukio lolote lenye athari katika umbali mfupi tu na wa karibu ama 'within range' kabla ya kuonekana na rada. Hiyo ndio maana ya 'low observable'.

Asante!
 
Ubarikiwe sana kwa elimu hii uliyotupa kuhusiana na haya mambo

Naomba kufahamishwa kuhusu jambo hili: kuna tv show ya kimarekani inaitwa The Last Ship.. katika series ile kuna episodes zinaonesha uwezo wa marekani katika medani za vita ikiwemo vita ya majini.. sasa katika meli ile ya jeshi la marekani walikuwa wanazima baadhi ya mitambo,wanapunguza mwendokasi wa meli pamoja na kuzuia movements za wanajeshi ndani ya meli kwa lengo la kutoonwa na maadui kupitia rada.. na sekunde chache baada ya kufanya zoezi lile chombo cha maadui kupitia rada walishuhudia meli ile ikitoweka katika screen ya rada..

Je hii ni kweli kufanya vile kunasaidia rada ishindwe kutambua chombo kile? Au ni kutia chumvi tu katika teknolojia??..Nawasilisha swali.
Awali ya yote, nikushukuru sana kwa uwepo wako mahali hapa.

Umeeleza kidogo kuhusu TV show hiyo lakini sijapata kuitazama ila nitajibu swali lako kuendana na kile ninachokifahamu.

Vyombo mbalimbali vikiwemo ndege, meli n.k. huweza kuzalisha vitu vingi sana ambavyo vinaweza kutumika katika utambuzi wa kubaini uwepo wa vyombo na mahali vyombo hivyo vilipo. Vitu kama vile sauti, mwanga, miale, mtikisiko (vibration), joto n.k. hutumika kama nyenzo muhimu katika masuala ya utambuzi.

Kupitia mifumo mbalimbali ya utambuzi, tunaweza kugundua uwepo wa chombo mathalani meli kupitia tu sauti ama kelele katika mifumo yake ya uendeshaji, pia hata joto (heat) linalotolewa kutoka katika mifumo hiyo na hatimaye tukabaini mahali na umbali chombo kilipo na ikibidi hata kukishambulia chombo hicho kwa makombora (heat-seeking missiles).

Hivyo, katika kupunguza ama kuthibiti vitu hivi vinavyozalishwa kupitia utendajikazi wa chombo husika, kunaweza kabisa kupunguza kama si kuondoa kabisa uwezekano wa chombo kutambulika. Hicho unachokisema kupitia hiyo TV show kipo kama njia mojawapo ya kujikinga na mifumo mbalimbali ya utambuzi na si rada tu.
 
Awali ya yote, nikushukuru sana kwa uwepo wako mahali hapa.

Umeeleza kidogo kuhusu TV show hiyo lakini sijapata kuitazama ila nitajibu swali lako kuendana na kile ninachokifahamu.

Vyombo mbalimbali vikiwemo ndege, meli n.k. huweza kuzalisha vitu vingi sana ambavyo vinaweza kutumika katika utambuzi wa kubaini uwepo wa vyombo na mahali vyombo hivyo vilipo. Vitu kama vile sauti, mwanga, miale, mtikisiko (vibration), joto n.k. hutumika kama nyenzo muhimu katika masuala ya utambuzi.

Kupitia mifumo mbalimbali ya utambuzi, tunaweza kugundua uwepo wa chombo mathalani meli kupitia tu sauti ama kelele katika mifumo yake ya uendeshaji, pia hata joto (heat) linalotolewa kutoka katika mifumo hiyo na hatimaye tukabaini mahali na umbali chombo kilipo na ikibidi hata kukishambulia chombo hicho kwa makombora (heat-seeking missiles).

Hivyo, katika kupunguza ama kuthibiti vitu hivi vinavyozalishwa kupitia utendajikazi wa chombo husika, kunaweza kabisa kupunguza kama si kuondoa kabisa uwezekano wa chombo kutambulika. Hicho unachokisema kupitia hiyo TV show kipo kama njia mojawapo ya kujikinga na mifumo mbalimbali ya utambuzi na si rada tu.
Sifa yako moja kubwa ni kwamba hata ngumbaru lazima aelewe
 
Mkuu umefanya vema kasoro kosa la kwanza uliloonesha B1B Lancer ni stealth, hiyo si stealth hata kidogo. Long range bombers ambazo ni stealth ni kama B-2 na hiyo B-12 zote kutoka kwa Northrop Grumman.
B1B Lancer ni toleo la B1 lenye stealth technology zikiwemo radar absorbent materials katika parts mbalimbali.
 
Back
Top Bottom