Stay Home Challenge, ni ujinga uliopandisha bei ‘Toilet Papers’

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,378
26,700
Salamu ndugu zangu.

Kwanza niwape pole kwa janga hili la kidunia, ila niwatie moyo ya kuwa litapita na hali itarejea kama kawaida, tuendelee kujilinda na kuwaombea walionaswa watoke salama.

Wakati tunaendelea kuhangaika na nyenzo za kujikinga na maambukizi, ghafla kumetokea ‘shortage’ ya baadhi ya vifaa kinga.

Hii ni pamoja na bidhaa kama vitakasa mikono [hand sanitizer] na barakoa au vinyago [mask] ambazo ghafla vimekuwa mchongo, yaani ukivipata unajiona kabisa umeyapatia maisha, mara nyingine bila koneksheni hupati.

Sasa limeibuka suala la makaratasi ya chooni [toilet papers], japo wengi wetu tunajua kabisa maisha yetu nyumbani, chooni kwa mjini tunatumia maji zaidi kuliko karatasi.

Kwa mkumbo na kupanic ile kusikia maduka-masoko yanafungwa, basi watu badala ya kustock chakula wamevamia na kununua makaratasi na kuficha majumbani.

Matokeo yake yamekuwa ya kuchezea kama mpira sebleni na kutamba mitandaoni, huku wenye uhitaji wakiteseka kupata bidhaa hiyo kwa bei juu.

Niwakumbushe tu ya kuwa huyu kirusi sio mjinga kiasi cha kujificha maeneo hayo, na hata kama akiwa huko hawezi kuuawa kwa kutumia hizo karatasi, acheni mkumbo na kukimbilia kila mnachoona na kusikia.

Nawasihi mzingatie maelekezo sahihi kutoka mamlaka husika kuhusu namna ya kujilinda, nyie wenye challenge zenu msilete mizaha mnapotosha na kugharimu wengine.

Tulinde afya zetu, na tuwalinde wenzetu, Corona is real.
 
Back
Top Bottom