GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Unaweza sema Mamlaka ya Rais Samia imetekwa( State Capture) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Ni katiba mpya tena vyombo vya habari vya Kimataifa vinamtaja Rais Samia kama kinara wa kukandamiza haki na Demokrasia Tanzania kwa kuwakamata viongozi wa Chadema mjini Mwanza Tanzania
Mtu mmoja na ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza anaamua kujichukulia mamlaka ambayo hayapo kisheria kuzuia uhuru wa watu kutoa maoni juu ya Taifa Lao wanataka liwe na muundo upi (Katiba Mpya)
Propaganda kama zilizofanyika wakati wa hayati Magufuli, Matokeo yake yameonekana sasa na hili Rais Samia amekiri wawekezaji walikimbia na Uchumi wa nchi umeporomoka kutoka asilimia 7% mpaka asilimia 4%
Katikati ya Taifa lililogawanyika kutokana na watu wake kugawanywa kikabila na Kichama na mtangulizi wa Mama Samia, Sasa Rasmi jina la Rais Samia limeanza kuchafuliwa Kimataifa kwa kosa la mtu mmoja na ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliyewakamata viongozi wa Chadema usiku wa manane akiwemo Mwenyekiti wa chama Taifa Mh. Freeman Mbowe
Matokeo ya sera hizi za kuminya haki na uhuru yanaenda kugusa Uchumi ulioporomoka moja kwa moja na kuathiri Sekta ya uma na binafsi
Mosi, Sera za Mama hazitabiriki tena kwa wawekezaji wa Kimataifa ambao wanahitaji taarifa za uwazi na ukweli, Uchumi utaenda kuporomoka zaidi na hivyo mwakani hakuna tena ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi
Pili, Kuendelea na wafuasi wa Rais aliyemtangulia kama mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambao wamezoea kujitwalia sheria na Mamlaka ya Rais mkononi, Hakuna mwekezaji atakaye wekeza kwenye mikoa ya namna hiyo na hili Rais Samia alipaswa kuliona kwa jinsi Ole Sabaya alipoharibu Mali za wawekezaji, Tutegemee anguko kubwa la bei za mazao ya wakulima
Tatu, Chuki juu ya Chuki imeanza kutamalaki tena, Funzo la mtangulizi wa Mama Samia kwa yaliyotokea kila mtu anamtazama Rais Samia kwa macho matatu, Jicho la tatu limeshaamini Tozo za miamala ya simu na Ukamataji wa wanasiasa, Rais Samia ndie anawatuma kuyafanya haya, Bila kuunganisha Taifa lolote utakalofanya ni sawa na kazi bure
Ushauri
Taifa kwa sasa linahitaji kupumua kutokana na Funzo kubwa toka kwa Rais aliyemtangulia Mama Samia, Kupumua kwa Taifa ni watu kutoa maoni yao juu ya Taifa Lao, Watu kuponya majeraha yaliyoachwa na utawala kabla ya Rais Samia, Kuzuia maoni ya wananchi ni kutengeneza chuki isiyotibika ambayo baadhi ya watu walishangilia kifo cha mtangulizi wa Mama Samia
Madhara yaliyofanyika Kimataifa ya nahitaji kuponywa na walioyaongea Kimataifa, Ni muda wa kuwaunganisha watu wenye exposure Kimataifa ambao tayari wanaaminiwa na vyombo vya habari Kimataifa kwa taarifa kama za Leo kukamatwa Kwa wafuasi wa chadema tayari vyombo vya Kimataifa vimewahoji watu hao kuhusu aina ya sera na utawala wa Rais Samia
Nguvu ya watu waliopo mtandaoni Twitter na hapa Jamii Forum wanasukuma agenda kimkakati sana Kimataifa, Rais mtangulizi kabla ya Mama Samia alijaribu kuzuia hii mitandao lakini ndio iliyomuonyesha Kuwa hajali sera za Kimataifa na utengamano na ilipelekea anguko kubwa kama Taifa