StarTV wanajitahidi sana kutokuwa waoga. Media nyingine zimeufyata, hawaibui hoja zozote kinzani (in a positive way) kwa Serikali na CCM

Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
17,189
46,227
Nipo sehemu hapa kuna mdajada unaendelea StarTV, wamemualika mpinzani anatema cheche ambazo kwa mtu mwenye akili sawa lazima aone jamaa ana point..sidhani kama kuna Media inaweza kutoa platform kwa hili kutendeka..hongereni StarTV.

Anahoji inakuwaje watendaji wa CCM wanatembea nchi nzima kufanya mikutano huku vyama vingine vinapigwa pini?

Mijadala kama hii ya kuhoji demokrasia yetu ni ya kweli au ni danganya toto haipo kwenye media nyingine..huko ni kufwata tu bendera.
 
Timu ikishinda hamasa ya ununuzi wa jezi unaongezeka watakapo imarisha uchumi uhalali wao kuzunguka nchi nzima utakuwa na Tija kwasasa tunwaona kama wanajikosha tu
 
Nipo sehemu hapa kuna mdajada unaendelea StarTV, wamemualika mpinzani anatema cheche ambazo kwa mtu mwenye akili sawa lazima aone jamaa ana point..sidhani kama kuna Media inaweza kutoa platform kwa hili kutendeka..hongereni StarTV.

Anahoji inakuwaje watendaji wa CCM wanatembea nchi nzima kufanya mikutano huku vyama vingine vinapigwa pini?.

Mijadala kama hii ya kuhoji demokrasia yetu ni ya kweli au ni danganya toto haipo kwenye media nyingine..huko ni kufwata tu bendera.
Wacha ujanja wa kilumumba
 
Kuna huyo kijana anaitwa Mtozi Nyanda ana kipindi hapo star tv kinaitwa The Big Agenda,yuko poa sana. Kumbuka ni kupitia kipindi hicho ndipo Mh.Dialo aliujulisha ulimwengu kuwa tumewahi kuwa na kiongozi mwenye faili Milembe. Kwakweli hicho kipindi huwa sitaki kukikosa.
Mzee wetu Diallo hakutaka utani kabisa..
 
ITV watangazaji wanawinda teuzi lazima waimbe pambio,ndo maana wameanza kutumia lugha za ajabu kumfurahisha mtemi Hangaya... eti 'kichaka Cha Magufuli chageuka maficho ya wezi.'
 
Hata mimi nimenoti star tv wamebadilika safari hii.

» Kipindi cha nyuma walikuwa wanaalika wageni wa upande mmoja tu au mgeni kinzani ni aina ya akina john cheyo

» Kwenye matangazo ya kujiunga na bbc ikitokea habari ya moto wanakata matangazo.

Juzi kati kuna kipindi cha jioni mtangazaji alikuwa anawahoji raia katika maeneo ya kinondoni kuhusu tozo, waliinanga sana serikali. Kipindi hiki ingekuwa nyuma huko kisingeruka kabisa.

Nahisi Dialo alikuwa anamwogopa Magufuli lakini alikuwa hamkubali. Lakini sasa hamwogopi Hangaya, hamkubali na anajua hawezi kumfanya kitu.
 
Star Tv wanajitahidi sana, kuna Big Agenda cha Aloyce Nyanda Mtozi na Medani za siasa cha kijana anaitwa Odemba
Ndio Tv pekee naweza kuisikiliza mijadala yake kwa sasa
TV nyingine hamna issues za maama kabisa..ni kusifia sifia tu watawala.
 
Kuna huyo kijana anaitwa Mtozi Nyanda ana kipindi hapo star tv kinaitwa The Big Agenda,yuko poa sana. Kumbuka ni kupitia kipindi hicho ndipo Mh.Dialo aliujulisha ulimwengu kuwa tumewahi kuwa na kiongozi mwenye faili Milembe. Kwakweli hicho kipindi huwa sitaki kukikosa.
Star TV inajaribu kujifufua baada ya mwendazake kuondoka, mbona hawakufanya hivyo vipindi jamaa akiwepo?
 
Back
Top Bottom