Startimes nyenzo muhimu katika kuendeleza na kuimarisha ushawishi wa taifa la China barani Afrika

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,041
10,463
Tunaotumia kingamuzi cha startimes sasa tunajifunza lugha ya Kichina kupitia channel ya starswahili hongera kwa Wachina kutumia kampuni yao ya startimes kama jukwaa la kutangaza tamaduni zao pamoja na mafanikio yao.

Mataifa shindani kama USA yameendelea kushangazwa na kuongeza kwa ushawishi wa China Barani Afrika ukweli ni kuwa sababu zipo nyingi ila mojawapo ya sababu ni kingamuzi chao cha startimes kupitia channel zao kama CGTN na channel zao za kikanda kama StarSwahili na nyingine nyingi wanazoshirikiana nazo kama Channel Ten yenye vinasaba vya CCM.

Kupitia hizo channel tajwa hapo juu maudhui yake mengi yamekua ya kuisifu nchi ya China kupitia miradi yake iliyopo nchini China na Barani Afrika kama vile madaraja, viwanda, barabara na siasa za China huku wakituaminisha kuwa wao ndio marafiki wa kweli wanaojua shida zetu A to Z na wenyewe pekee ndio wanaoweza kuzitatua kwa kutuletea bidhaa Affordable kulinganisha na uchumi weru.

Pia wamekuwa wakitumia chombo chao kuwasuta wale wote wanaowashutumu vibaya juu ya siasa zake za ndani kukandamiza haki za raia wake mfano kama utotoni ushawahi kuishi na mlezi anayekutesa siku wakija wageni atakuvalisha nguo nzuri na atapika chakula kizuri na mwisho wa siku atakuita mbele ya wageni na kukuuliza namna gani unaishi naye kwa sababu ya hofu unakuta unamsifia na kuwaambia wageni kuwa una furahia kuishi naye ili hali si kweli.

Mwisho China wanastahili pongezi licha ya mapungufu yao ila wamedhihirishia dunia kuwa wameamua na wanaweza enzi za kutishiwa zilishapita.

From northern part of Tanzania.
 
Sioni matokeo ya kweli kwa AU vision2063 kwa Afrika yetu.

Sioni utashi wa kweli nini tunataka na wapi tunataka kuwa.

Vijana % kubwa hawana matumani na Afrika yao zaidi ya dreaming in America etc.

Zamani tulikua na BBC, VOA na DW now tuna Radio China/ Japan Kiswahili yote ni kusambaza ushawishi

SABC, KBC, UBC etc zingefaa ziwe free ila za ubeberuni ni rahisi kuzipata kuliko hizo affiliations za waafrika wenzetu
😅😅😅
 
China kama inaipenda afrika ijaze waafrika wengi huko kwao china tena waloe na wazae na wachina kama marekani ampo kuna waafrika wengi tu raia wao. China inajipendekeza kwa afrika ili ipate rasilimali za afrika kwa faida yake. Bora mzungu alikuja na dini na elimu kwa waafrika. Sasa mchina anakuja na nini kama si ujanjaujanja wa kutaka kueneza ukoloni wake mpya wa kichina barani afrika?
 
Back
Top Bottom