Startimes media, huu ni utapeli

Mkazamoyo

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
1,256
2,061
Jamani hawa wachina na kampuni yao wanachofanya ni utapeli na uwizi wa mchana kweupe.

Ishu iko hivi mm nilikuwa natumia king'amuzi cha antena vile vya mwanzo lkn ni zaidi ya wiki sasa havioneshi(no signal) nilipowapigia wakasema hvyo vya antena kwa sasa havifanyi kazi kinachotakiwa tupeleke kwa wakala hivyo ving'amuzi then watatupa vya dish na dish lenyewe but tuchangie kiasi 'kidogo' cha sh77,000/-.

Je hii si ni sawa na kununua upya tena? yaan king'amuzi kimoja unanua mara mbili hasa ikizingatiwa kuwa bei halisi ya kile cha dish ni 86,000/-

Kweli nimekubali cha bure gharama nimetangaza rasmi kuhamia azamtv utapeli huu hauvumiliki.
 
Huna lolote, unafanya promotion ya decorder za Azam tu... Kwani ilikuwa ni lazima ututajie Azam TV?...
 
Kwanini haya malalamiko yako hukuyatoa startimes, mbona mm nakitumia cha antena na kinafanya kazi. Wabongo bwana.
 
Jaman nani wataonyesha AFCON?.startimes au AZAM?,au TBC?.hawa TBC Si huwa wamapewa punguzo na CUF Kama station ya Taifa?,maana sioni matangazo na aina zozote za kuonyesha Mubashara.
 
Kwanini haya malalamiko yako hukuyatoa startimes, mbona mm nakitumia cha antena na kinafanya kazi. Wabongo bwana.
Inategemea na eneo au mkoa ulipo lkn kwa sehemu nilipo ving'amuzi vya antena havifanyi kazi. Lkn km umesoma vzr hyo post utaona kuwa hayo malalamiko hayo nimeyaripoti huko star times na majibu ndo hayo kuwa nilipie tena 77,000/-.
Huna lolote, unafanya promotion ya decorder za Azam tu... Kwani ilikuwa ni lazima ututajie Azam TV?...
 
Mwenyewe startim wananiboa sana nalipia hela inaenda bure nimewapigia hadi nimechoka...dawa ni kuwahama wanakera kweli...
 
Mimi nna mwezi wa 5 sasa,,,no signal,, nimewapigia wanasema niwapelekee wakakibadirishe,,ila niende na pesa za kupewa dish.,77elf
 
Jamani hawa wachina na kampuni yao wanachofanya ni utapeli na uwizi wa mchana kweupe.

Ishu iko hivi mm nilikuwa natumia king'amuzi cha antena vile vya mwanzo lkn ni zaidi ya wiki sasa havioneshi(no signal) nilipowapigia wakasema hvyo vya antena kwa sasa havifanyi kazi kinachotakiwa tupeleke kwa wakala hivyo ving'amuzi then watatupa vya dish na dish lenyewe but tuchangie kiasi 'kidogo' cha sh77,000/-.

Je hii si ni sawa na kununua upya tena? yaan king'amuzi kimoja unanua mara mbili hasa ikizingatiwa kuwa bei halisi ya kile cha dish ni 86,000/-

Kweli nimekubali cha bure gharama nimetangaza rasmi kuhamia azamtv utapeli huu hauvumiliki.
na bado hata baada ya kununua hicho cha dish hutopata channel zote
 
Azam utakimbia mwenyewe hamna kifurushi cha elfu 6 ni 15 kwendelea na channel ya bure ni tbc1
 
Azam ndo kila Kitu. Hao jamaa walinidanganya nikanunua decoder yao wakaniambia nitapata free channels kwa mwezi mmoja cha ajabu hata wiki haikwisha wakakata matangazo .ishu ikaja kwenye kulipa sasa aisee sitaki hata kukumbuka. Nimeamua kuacha na nao bora niangalie Azam
 
Cha antena cha zamani nilikuwa napata local chanel zote bure,kuanzia juzi wamekata zote nimebaki na tbc1 na tv1 tu! Mmh!
 
Back
Top Bottom