Startimes Decoders, TV zenye Hisense za Kichina. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Startimes Decoders, TV zenye Hisense za Kichina.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MPadmire, Dec 3, 2010.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  TBC na Startimes wanauza Decoder pamoja na TV za Kichina.

  Hizo TV zina inbuilt decoder, flat screen, inch 26. Bei yake ni 570,000.

  Naomba ushauri wenu kama hizi TV ni nzuri na kama zina matatizo, matatizo ni yepi.

  Asante
   
 2. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Duuh kama watakuwa hawajazichakachua huenda ikawa habari njema...Ni za kampuni gani maana jina la kampuni nalo ni muhimu ?...Kwa kuwa ndio kwanza zimeingia wewe nunua tu utupe uzoefu wako baada ya kuzitumia.
   
 3. N

  Newvision JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Achana nazo utaja lia bure huu ni ushauri wa bure technically hizo TV za Chaina ni bomu
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  kuna thread inayohusu hili jambo na ina maelezo ya kujitosheleza kabisa.....omba msaada wa kutafutiwa
   
 5. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Asanteni kwa michango yenu na ushauri.

  Nitachanganya ushauri na akili yangu halafu nitapata jibu.

  Hizo TV hazina kampuni, ni za Startimes na zimeandikwa Hisense. Hazihitaji Dishi wala antenna.

  OK then, kati ya Sony na Sanyo ni TV ipi Bomba?

  Kuna sony flat model mpya zimeingia-flat screen, je ni nzuri?

  LG vipi ukilinganisha na SAMSUNG?
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  PM mtu anaitwa 3D, jamaa ni noumaaaa.....au subiri aamke
   
 7. j

  jojig Member

  #7
  Dec 3, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Hisense ni chinese brand ya miaka nenda rudi...Pia watanzania inabidi tuamini kuwa kuna other chinese brands which are international known for many yrs.mfano mdogo mmoja wapo ni hii kampuni ya hisense au haier ni kampuni ambazo zinameet international standards in electronics industry.Pia nadhani kwa hiyo bei waliyokutajia ni fair kabisa kwa hiyo tv(original) Ila pia kumbuka chinese can make anything in the world and put what logo/brand name they want hiyo kwao si shida so cha msingi ni kujua kama ni ya ukweli au fabricated kwa kujaribu kujua hata warranty ikoje!
  ni hayo tu!
   
 8. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Warranty ni mwaka mmoja, yaani garantee ni mwaka
   
 9. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Wachina wanatengeneza vitu vingi tu ambavyo vimewekewa brand names tu. Nimegundua vitu vingi ninavyoumia ni made in China. Mfano ni laptop yangu ya Compaq, navigator etc.
   
 10. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huwezi kukwepa vitu vya kichina siku zote inategemea na aina ya vitu. Karibu kila kitu siku hizi kinatoka China na vingine ni nafuu na bora sana.
   
 11. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu,
  Unajua kuwaponda moja kwa moja wachina si busara hata kidogo! wenyewe wanatengeneza bidhaa ya kukidhi mahitaji na bajeti ya kila mtu...! ndy maana masoko yaliyo quality sensitive wanapeleka bidhaa za maana.
  Asilimia zaidi ya 50 ya bidhaa za kielektroniki ama zimetengenezwa china, au ndani yake kuna komponenti toka china!
  HTC, APPLE wanatengenezewa baadhi ya vifaa vyao china, DELL, HP, SONY.
  Tatizo ni wanunuzi, unaenda dukani kutaka kununua BB STorm una laki 1 unategemea muuzaji afanye nini zaidi ya kutafuta za kutoka hongkong!
   
 12. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #12
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kwa taarifa zenu, hivi sasa katika consumer electronics, achilia mbali textile industry, China inaongoza kwa kuwa manufacturer wa consumer electronics zinazopatikana katika nchi zote duniani.

  Unaposema kwamba TV za China ni "bomu", sidhani kama unaelewa unachokisema. Ukweli wa mambo ni kama ifuatavyo.


  1. Mfanyabiashara anapokwenda kiwandani, katika jimbo lolote lile nchini China, mwenye kiwanda anamwuliza: Uwezo wako wa kifedha ni upi, yaani, unataka mali yenye kiwango gani cha ubora kutokana na uwezo wako?
  2. Mfanyabiashara mwenye uwezo, na kujali soko lake, huchagua kiwango cha ubora wa juu kabisa, ambacho kinaitwa Grade 1. Kimsingi, kuna viwango takriban 6 vya ubora, kuanzia Grade 1. Kila kiwango cha chini ya Grade 1 kina ubora PUNGUFU!
  3. Tatizo la Waafrika, yaani, wafanyabiashara wa Kiafrika, wanapenda sana kununua vitu ambavyo vina kiwango kidogo cha ubora. Kule China, kiwandani, wanalipa pesa ndogo, lakini wakifika Dar, BEI KUBWAAA!
  4. Sisi tunaamini kwamba KILA KITU kinachotoka China ni KIBAYA! Hapana! Si kweli. Kama ni wa kulaumu, walaumuni hao wafanyabiashara wenye TAMAA! Msimlaumu Mchina! Yeye anatengeneza kwa order yao!
  Nadhani nimeeleweka!
   
 13. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mkuu NV, wakati mwingine tujaribu japo kidogo kuepuka kujibu kwa kutumia mazoea! Kuna vitu vingi sana vya China tunavyotumia ambavyo ni Imara. Nina DTop yangu ya DEll made China ambayo ninatumia mwaka wa 4 sasa haijanipa matatizo yoyote mi kazi yangu ku-update program tu! Kuna mwanajamvi ameeleza vizuri hapo juu kuwa tatizo la wabongo wengi ni kutaka vitu vya bei chee matokeo yake ndio hayo! Kama una uhakika wa ubovu wake fafanua vizuri kwa hoja zinazoeleweka ili wote tupate somo badala ya kujibu juu juu tu kuwa "achana nazo, utjalia bure"!
   
 14. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Jibu mbaaaado...

  Naomba ushauri wenu kama hizi TV ni nzuri na kama zina matatizo, matatizo ni yepi.
   
Loading...