Stars vs Moroco in JF

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,243
Ninakuwa mnyoofu wa moyo katika kuliongelea gemu la leo maana kinachonisukuma ni uzalendo tu ila si soka!

Timu yetu imekuwa nzuri kiufundi, tatizo lake ni hamasa tu!
Tunahitaji mtu mhamasishaji kama maximo au julio na polsen abaki kuwa mtaalamu wa ufundi tu!

Kuifunga Moroco leo ni maajaliwa ya muumba hata tungefukia binadamu pale Markhesh kipigo bado kitatuaandama tu!

Mwenye ratiba sahihi ya mechi atujuzi tuonyeshe uzalendo wetu!!!
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Hivi bado kuna mtanzania yeyote mwenye matumaini ya kufuzu kuingia kwenye final baada ya leo, ajitokeze sasa tumsikie.

Just imagine, tunatakiwa kushinda kwa zaidi ya goli 4 kwa bila. Na hii tutasonga mbele endapo tu Algeria wataifunga Central Africa leo. Tusisahau hapa nyumbani Morocco walituchapa goli moja. Tusisahau katika line up yetu ya leo,hakuna Nizar, Nsajigwa na Victor costa.

Mpaka hapo mimi sijaona tunatoka vipi hapo. Tusidanganyane wajameni.........
 
Kama nigeria wametolewa na egypt nao nje pamoja utemi wao, lolote laweza kutokea. Vijana wanatakiwa waache uoga, uivivu wa dkk 90! wakomae mwanzo mwisho wataweza kuwabania mbona.
 
Mimi najua tutafungwa zaidi ya goli mbili bila shida halafu huo ndiyo utakuwa mwisho wa ndoto zetu! Kifupi nahisi kocha huyu mpya hajafanya lolote la maana na saizi JK toka nuru yake ya kisiasa ianze kufifia basi ameitupa kabisa michezo.
 
Kama nigeria wametolewa na egypt nao nje pamoja utemi wao, lolote laweza kutokea. Vijana wanatakiwa waache uoga, uivivu wa dkk 90! wakomae mwanzo mwisho wataweza kuwabania mbona.

mwenye ratiba please tujuzeni tutumie kauzalendo kalikobaki.
 
Hii Taifa Stars haitaweza kufika mbali, mwalimu alikuwa ni Maximo siyo huyu wa leo. We hapo hesabu tumetolewa tu!
 
Hivi bado kuna mtanzania yeyote mwenye matumaini ya kufuzu kuingia kwenye final baada ya leo, ajitokeze sasa tumsikie.

Just imagine, tunatakiwa kushinda kwa zaidi ya goli 4 kwa bila. Na hii tutasonga mbele endapo tu Algeria wataifunga Central Africa leo. Tusisahau hapa nyumbani Morocco walituchapa goli moja. Tusisahau katika line up yetu ya leo,hakuna Nizar, Nsajigwa na Victor costa.

Mpaka hapo mimi sijaona tunatoka vipi hapo. Tusidanganyane wajameni.........

Hizo goli 4 bila unafanya hesabu gani ni goli 2 bila kitu ambacho bado mimi naona ni kigumu vilevile.
 
Mechi inaanza saa nne na nusu usiku kwa saa za Afrika mashariki (22hr30). Tujipe moyo tu na kuonyesha uzalendo lakini ukweli ni kwamba hatuendi popote tunakamilisha ratiba tu!
 
Nawatakia kila la kheri vijana wetu wanaotupeperushia bendera yetu huko. Nawaombea wawe mabalozi wema na warudi na ushindi.

kwa jinsi unavyowaabudu waarabu nilidhani ungeweka uzalendo pembeni na kutaka waarabu washinde! big up lady!
 
Kuna kituo kitarusha live mechi hii?Nina hamu kuangalia mechi hii kupima maendeleo yetu.Kiufundi Poulsen yupo safi sana kwani angalau sasa Taifa stars wanamiliki mpira.
 
Mechi inaanza saa nne na nusu usiku kwa saa za Afrika mashariki (22hr30). Tujipe moyo tu na kuonyesha uzalendo lakini ukweli ni kwamba hatuendi popote tunakamilisha ratiba tu!

Msikate tamaa, hapa ni kupigana hadi dk. 90, vigogo wameangushwa jana na hata hao Moroco tunaweza kuwalaza chali, bahati mbaya tunategemea matokeo mengine kule Algiers lakini hata Angola wamepita kihivyo.
 
Hivi bado kuna mtanzania yeyote mwenye matumaini ya kufuzu kuingia kwenye final baada ya leo, ajitokeze sasa tumsikie.

Just imagine, tunatakiwa kushinda kwa zaidi ya goli 4 kwa bila. Na hii tutasonga mbele endapo tu Algeria wataifunga Central Africa leo. Tusisahau hapa nyumbani Morocco walituchapa goli moja. Tusisahau katika line up yetu ya leo,hakuna Nizar, Nsajigwa na Victor costa.

Mpaka hapo mimi sijaona tunatoka vipi hapo. Tusidanganyane wajameni.........
Mkuu nakusahuri ubadili/rekebisha kichwa cha habari hii...

Kukujibu swali, ktk kandanda kuna mambo matatu ya kutegemea, (i) kushinda, (iii) kushindwa, au (iii) kutoka sare/suluhu.
 
kiukweli hakuna jipya la huyu kocha...anaonekana amekuja kupumzika tu Tz na kukusanya hela ya kustaafu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom