Star TV yakinzana na TCRA

Chemwali

JF-Expert Member
Apr 5, 2011
397
178
[h=3]AA! STAR TV YAITUNISHIA TCRA MSULI [/h]
Siku moja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuagiza matangazo ya Star TV yarejeshwe kwenye kisimbuzi cha Star Times ifikapo saa 10 jioni jana, televisheni hiyo imegomea agizo hilo na imetishia kwenda mahakamani ikiwa italazimishwa kurejea humo. Taarifa ya kugoma agizo hilo, ilitolewa jana na Meneja Mipango na Utafiti wa Sahara Media Group Ltd, Kampuni inayomiliki Star TV, Nathan Lwehabura.
Ilieleza kuwa kinachofanywa na TCRA, kuwalazimisha kurejesha matangazo Star Times ni ukiukwaji wa Sheria ya Hatimiliki na Sheria ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.
“Serikali ya Tanzania ni mwanachama wa WTO na pia WIPO (World Intellectual Property Rights Organization) na hivyo kwa kulazimisha uvunjaji wa sheria za hati miliki ina maana inavunja haki zetu zilizopo kikatiba! Tutakwenda mahakamani kupata haki yetu hii muhimu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Pamoja na kutoweka bayana lini watakwenda mahakamani, Lwehabura alisema sheria ya hati miliki inaweka
kinga kwa vipindi vya redio, televisheni, nyimbo na sanaa. Alisema kulazimisha Star Times kupora vipindi vya Star TV, inadhihirisha kilio cha wasanii wa Tanzania, wasivyolindwa na Serikali yake. Taarifa hiyo ilieleza Mei 23 mwaka huu, Star TV kupitia mwanasheria wake iliwataka Star Times kuiondoa kwenye kisumbuzi chao ifikapo saa sita usiku wa Mei 31, mwaka huu kutokana na kurusha na kuuza maudhui na vipindi vyake bila idhini na kukiuka sheria za haki miliki (Copyright laws).
“Katika barua hiyo, Star TV iliwakumbusha Star Times kwamba hawakuwa na mkataba wa kurusha kituo hicho kwa mujibu wa sheria ya EPOCA, pia hawana haki ya kutumia maudhui yake bila idhini chini ya Sheria ya Haki miliki ya Tanzania na kimataifa,” ilieleza taarifa hiyo.
Hata hivyo, Mei 31 Star Times/Star Media walijibu kwamba hawajakiuka sheria yoyote. Walisisitiza wataendelea kuirusha Star TV, kutekeleza matakwa ya sheria ya EPOCA na kanuni zake. Lakini, Star TV iliwaandikia tena na kuwaeleza itachukua hatua zaidi kwa kukiuka ;na kuwataka iwaondoe saa sita usiku wa Juni 8, mwaka huu.
Tarehe 6 Juni mwaka huu, Star TV iliwaandikia tena Star Times ikisisitiza nia yake ya kuchukua hatua zaidi, kutokana na wao kuendelea kukaidi ombi hilo na kuainisha mapungufu kadhaa ya kisheria kwa upande wao, yanayoifanya Star TV ijiondoe kwenye king’amuzi chao ifikapo saa sita usiku wa tarehe 8 Juni, mwaka huu na kufanya hivyo.
Jana, TCRA, kupitia Mkurugenzi Mkuu, Profesa John Nkoma, iliagiza chaneli hiyo irejeshwe mara moja jana ifikapo saa 10 jioni na kuzitaka pande hizo mbili, kukutana na mamlaka Juni 17 mwaka huu kwa majadiliano zaidi.
Hata hivyo, mpaka jana saa 11.20 jioni, Star TV haikuwa inaonekana kwenye Star Times huku TCRA ikidai Star TV inakiuka sheria ya EPOCA na ikikaidi, itachukuliwa hatua kwa kuwa si yenyewe wala Star Times walioko sawa katika maamuzi hayo.
TCRA iliwataka watoa huduma hao kufuata Sheria, inapotokea kutokuafikiana katika jambo fulani badala ya kutoa maamuzi bila kumshirikisha Mdhibiti (TCRA), kwani kufanya hivyo ni kuwakosea haki wananchi.
Hata hivyo, Star TV imesema haipo tayari kuona maudhui yake yakiuzwa nje ya nchi bila makubaliano. Star Times jana hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo. Lakini, awali, Msaidizi wa Meneja wa Star Times, Hellen Elisa alithibitisha kujitoa kwa Star TV. Alisema waliwaandikia barua na kudai wamejitoa kwa matakwa yao.
 
Well done start tv, huu ni ushenzi hao tcra wanataka kutuambia nini kama sio kuwatengenezea wachina ulaji, hivi serikali yetu ina tatizo gani jamani? Hebut watanzania shime tusimame upande wa star tv, wakizuia matangazo tuandamane mpaka kieleweke, kwanza kuna utata tayari juu ya clouds na hawa start tv ambao mpaka leo huyo prof nkoma ameshindwa kuutatua, tuuizeni sisi tuliokaribu na wamiliki wa hivi vyombo, hawa wachina ni kiburi kuliko takataka yoyote, wamezoea kutoa kitu kidogo na kutukanyaga wazawa kam amatope, sasa hapa ndio na vyombo na waandishi tuungane tuwateneneze hawa washenzi
 
Du lakini nitamiss Pika Bomu,na Mbwembwe za BBC za salim Kikeke Na Charles Hillary
 
Ni maajabu kuwa serikali, kupitia TCRA inawalazimisha Star TV kufanya kazi na Star Times pasipo makubalino yoyote ya kimaandishi!
Napata mashaka kidogo kuona taasisi kama TCRA ambayo nilikua naamini inaongozwa na wasomi wenye weledi wa masuala ya mawasiliano wanafanya mambo kienyeji!
Kama maprofesa ambao ni wasomi wajuu zaidi nchini wanafanya mambo kienyeji, ni nani atatusaidia kujenga taifa imara?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Well done §tar Tv ni njia mojawapo nzuri na ya busara... Hakuna kulazimisha ndoa...
 
Hawa Star times wezi sana,kwenye king'amuz cha Continental(star tv) channel20 bure,wakati star times bure ni local tu tena zipo nne tu,hawa TCRA ni wasanii wataka kutuendesha kama punda,tumechokaa na huu usanii
 
Tuone sakata la Chama na Serikali nani ameshika hatamu za uongozi!nasubiri
 
Huwa sinaga imani na huyu Prof Nkomo sijui Nkoma wa TCRA yaani anaonkana seriousness ya usoni kwenye matendo sifuri
Unaanzaje kuwapiga biti watu wazima?
Ata suala la anonimous phone calls mpaka leo limewashinda!
 
Safi sana Star TV tupo pamoja komaeni mpaka kieleweke msikubali kuwaneemesha Star times
 
Ni maajabu kuwa serikali, kupitia TCRA inawalazimisha Star TV kufanya kazi na Star Times pasipo makubalino yoyote ya kimaandishi!
Napata mashaka kidogo kuona taasisi kama TCRA ambayo nilikua naamini inaongozwa na wasomi wenye weledi wa masuala ya mawasiliano wanafanya mambo kienyeji!
Kama maprofesa ambao ni wasomi wajuu zaidi nchini wanafanya mambo kienyeji, ni nani atatusaidia kujenga taifa imara?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Kwenye hela ndugu yangu uprofesa unawekwa chini yaani mtu anaweza akajiita darasa la saba ili mradi tu afanikishe dili.Sasa mimi sijui ntaipateje futui yule jamaa tajiri wa Kigoma du
 
Nimekichoka kisimbuzi cha Startimes,na ITV wakijitoa napata sababu kamili za kwenda kuki2pa...
 
TCRA mambo wanayofanya chini ya mkurugenzi mkuu wao yanatia shaka. Wanawapendelea wageni na kuwakandamiza watanzania. Toka alivyotangaza kuwa mwezi wa tatu bei za simu zitashuka mpaka leo hajatoa tamko lolote. Hivi watanzania tunamhitaji mkurugenzi wa aina hii? Prof. Nkoma ni Bomu. Kwa maslahi ya watanzania na serikali yao mtu huyu aondolewe kwa sababu ataleta madhara makubwa. Maamuzi yake yanaonesha anatumia nafasi yake kwa maslahi binafsi. Kama anatumiwa na baadhi ya viongozi wa serikali kwa hila basi aache, la sivyo hasira za wananchi zitahamia kwa serikali. Suala la ving'amuzi na bei za kupiga simu ni matatizo nyeti kwa kipindi hiki nashangaa viongozi hawalioni.
 
Back
Top Bottom