Star tv uchakachuaji/upotoshaji huu unawavunjia heshima

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Katika hali ya kushangaza Kituo cha Television cha Star TV kimerusha hewani habari ya siku tano zilizopita kuhusu Mgomo wa madaktari. Katika taarifa hiyo walimuhoji Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Mbeya Dr Chomboko ambae kwa wakati huo alisema hakuna mgomo hapo. Na kwa kupotosha zaidi wakaonyesha picha ya Dr Chomboka lakini jina la Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dr Samky.

Sijaelewa Star TV wanakusudia nini kwa upotoshaji wa aina hii, kama walitaka kuonyesha madaktari hawajagoma si wangeenda hata kwenye hospitali za wilaya kwenda kuhoji AMOs ambao wanaendelea na kazi kuliko kutuletea taarifa ya zamani na kuudanganya uma kwamba ni ya leo.

Yahya Mohamed ni member humu, tunaomba star TV iwaombe radhi watanzania kwa uchakachuaji huu na kwa kweli vyombo vya habari kama star tv mkianza hivi ile imani tuliokuwa nayo kwenu itapotea.
 
Jenerali Ulimwengu baada ya kuona Rai linachakachuliwa na Rostam alijiondoa na kuanzisha Raia Mwema gazeti linaloheshimika zaidi nchini. Wahariri Startv Msiaibishe weledi na taaluma yenu, Kataeni kutumiwa kwa propaganda za kizembe
 
Mchana wa leo nilikuwa Muh2 na kwa bahati nzuri waandishi walinikuta pale na walipelekwa na manesi hadi mawodini ambapo walionyeshwa maiti nyingi humo mawadini. Hakuna chombo hata kimoja kilichoeleleza hasa kinachoendelea. sijajua ni kwa7bu ya kumlinda nani.
 
Yahaya mwenyrewe gamba baya kabisa hata weledi hana njaa tu hamuoni bias zake; vipindi vyaker vya mijadala naangalia tu vile ambavyo najua nani atakuwa muongeaji anatia aibu sana ndio washauri wakuu wa dialo pumba kabisa
 
serikali inajaribu kutumia vyombo vya habari tiifu kwake kupotosha wananchi, mwisho wa siku cjui itakuwa nn
 
Cha kushangaza naona habari za mgomo tuu lakini sioni habari juu ya madhara ya huo mgomo kwa wagonjwa. Waandishi wa habari wanaogopa kuonyesha yalioyoko sasa huko mahosipitalini? Au wanasubiri bahasha?
 
Back
Top Bottom