Yahya Mohamed
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 270
- 317
Tumejifunza nini katika Historia ya Majanga na Maafa yake Nchini?
Tanzania imekuwa na historia ya maafa tangu mwaka 1872. Maafa hayo yamesababisha vifo, uharibifu wa mali na mazingiraAina ya majanga nchini Tanzania ambayo yameleta madhara ni magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na mifugo, ukame, moto, ajali za vyombo vya usafiri na za viwandani, mafuriko, wadudu/ndege na wanyama waharibifu wa mimea.
Mengine ni ya wakimbizi, vimbunga na upepo mkali, migogoro ya jamii; tetemeko la ardhi, milipuko na volkano. Wakati mwingine maafa yanaweza kuwa makubwa na yenye madhara makubwa. Makali ya madhara ya maafa katika jamii yanategemea jinsi gani ilivyojiandaa kukabiliana nayo.Kutokana na kuongezeka kwa matukio na madhara ya maafa nchini, Serikali ilipitisha Sheria Namba 9 ya mwaka 1990 ya Uratibu wa Utoaji Misaada ya Maafa. Katika Sheria hiyo, Kamati ya Maafa ya Taifa (Tanzania Disaster Relief Committee - TANDREC) ilianzishwa ili kuratibu misaada yote ya Maafa Nchini.
Kamati za maafa kama hii zilitakiwa kuanzishwa katika ngazi za Mikoa na Wilaya. Sera hii ya Maafa inazingatia masuala muhimu katika mzingo (cycle) wa menejimenti ya maafa yaani kuzuia, kupunguza athari, kujiandaa, kukabiliana nayo yanapotokea na urudishaji wa hali ilivyokuwa kabla ya maafa kutokea au kuiboresha zaidi. Moja ya Kipengele muhimu cha sera hiyo kinasomeka kama ifuatavyo:
2.1.2 Kujiandaa Kukabiliana na Maafa:
(a) Hoja:
Kujiandaa kukabiliana na maafa kunahusisha kuandaa hatua muhimu za kiutawala, kisheria na kiufundi zenye lengo la kupunguza madhara kwa wanaokabiliwa na maafa. Hizi ni pamoja na utoaji wa tahadhari ya awali, mafunzo, mfumo wa mawasiliano, mipango ya uokoaji, na utafutaji wa rasilimali. Zoezi hii linahitaji kurudusiwa mara kwa mara mifumo na mipango, urekebishaji, na kufanya majaribio. Kwa sasa mifumo iliyopo bado haijaendelezwa na mingine muhimu haipo kabisa. Pale inapokuwepo, haifanyiwi majaribio kuona ufanisi au dosari zake ili zirekebishwe.
(b) Madhumuni:
Kuhakikisha asasi zote zenye jukumu la menejimenti ya maafa zinajiandaa, ziratibiwa na zinakuwa na rasilimali na nyenzo za kukabili maafa; mfano hospitali na vikosi vya zima moto.Maswali ya Msingi:Tumekwama wapi?Nini kifanyike?Shiriki Mjadala huu utakaoonyeshwa hapo kesho (Jumapili tarehe 2 Oktoba 2011) kuanzia saa 1:30 asubuhi kwa kutoa maoni na yatasomwa live wakati wa kipindi ambapo update za zoezi la Upigaji kura huko Igunga zitatolewa.
Nawasilisha.