Star TV Tuongee Asubuhi: Tumejifunza nini katika Historia ya Majanga na Maafa yake Nchini?

Majanga hapa Tanzania ni matokeo ya siasa chafu,
Angali wakati wa uchaguzi vifaa vya kutisha watu yanavyoandaliwa mapema kwa gharama kubwa, lakini meli inazama au ajali ya moto inatokea wahusika wanachelewa kufika kwenye eneo la tukio. Hata wakifika utakuta hawana vitendea kazi.

Utatuzi : Tuondoe watawala wasiowajibika na mifumo isiyotenda kazi.
 
Ahsante kwa kushiriki, mchango wako utasomwa punde

nina ving'amuzi viwili:

  • kimoja cha Star Times (hakina channel ya Star TV). Na hata walizonazo wameamua kuzigawa mafungu mawili, moja la Tshs. 9000/month na jengine 18000/month. Nasisitiza: hawajaongeza channel, bali wamezigwa zilezile makundi mawili. huu tuite nini kama si wizi na ubabaishaji katika biashara ya Digitali?
  • kingine cha EasyTV (kinayo channel ya Star TV, lakini haionekani).

Nafikiria kuachana na haya ma digitali yao niendelee na mtindo uwa zamani wa 'geuzia mjini, pandisha kidogo'.

naomba hii iwe mada siku moja jamani tujadili hawa watu wanaofanya biashara ya digitali kwa mtindo wa kitapeli.
 
Mi nakubaliana sana na MARCUS, unaweza ukawa mzalendo lakini mazingira fulani yakakufanya ukawa fisadi. Kwa hapo ni kweli kabisa UFISADI uko juu sana na ni janga kubwa hapa nchini. Pongezi startv kwa mijadala ya kujenga.
 
inasemekana ile meri iliyozama kule zanziber ilitengenezwa mnamo mwaka 1967,ata kwa kuiangalia ile meri ilikua imechoka,swala la kutonunua meri mpya laweza kusababisha majanga zaidi pia meri zote nchini utaratibu wao wa kuingiza abiria ni mbovu,kwa mfano meri ya victoria yenye safari bukoba kwenda mwanza huwa inajaza abiria hadi masikitiko,wafanyakazi wake hawakujifunza kutoka meri ya mv bukoba ilyozama,na pengine selikari inalijua ilo.lakini inasubiri meri izame waunde tume.
 
nina ving'amuzi viwili:
  • kimoja cha Star Times (hakina channel ya Star TV). Na hata walizonazo wameamua kuzigawa mafungu mawili, moja la Tshs. 9000/month na jengine 18000/month. Nasisitiza: hawajaongeza channel, bali wamezigwa zilezile makundi mawili. huu tuite nini kama si wizi na ubabaishaji katika biashara ya Digitali?
  • kingine cha EasyTV (kinayo channel ya Star TV, lakini haionekani).
Nafikiria kuachana na haya ma digitali yao niendelee na mtindo uwa zamani wa 'geuzia mjini, pandisha kidogo'.

naomba hii iwe mada siku moja jamani tujadili hawa watu wanaofanya biashara ya digitali kwa mtindo wa kitapeli.

Tutashughulika na Hili Mkuu ni Kero hasa,
 
Tatizo liko pande zote mbili,kwa wananchi na serikali kwa upande mwingine,mfano mwananchi anapanda meli au gari wakati limejaa au gari linakwenda mwendo wa kasi,hakuna anayemuonya dereva,baada ya ajali mtu akiwa kavunjika ndio utasikia anasema...."Ooh gari lilikuwa linaendeshwa kwa mwendo kasi nk" lakini pia hii inawza ikawa imesababishwa na umaskini wetu,unahitaji kusafiri hakuna usafiri wa kutosha unajikuta unaingia katika tatizo la kupanda meli au gari lililojaa ili kuwahi nk.

Kwa upande wa serikali hakuna mtu wa kusimamia sheria,trafiki wanapiga deal,SUMATRA wamelala,mawaziri na raisi wetu wamekalia kutoa salamu za rambirambi kila siku....kwa msingi salamu za rambirambi imekuwa ni kama wimbo wa taifa kwetu kila siku ni kupeana hizo salamu...cha kushangaza baada ya salamu za rambirambi hakuna hatua zinazochukuliwa kuzuia ajali hizo.
Upande wa hizi tume ni JANGA lingine hili,kila siku tume ambazo mawazo yake hayafanyiwi kazi kabisa.
 
Back
Top Bottom