Star TV ni kitengo cha propaganda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Star TV ni kitengo cha propaganda?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chromium, Apr 9, 2011.

 1. Chromium

  Chromium JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 598
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hivi punde Star TV wamemaliza kipindi cha moja kwa moja kinachoitwa Jicho letu ndani ya habari. Leo walikuwa wanazungumzia jinsi vyombo vya habari vya ndani vilivyoshiriki katika mijadala ya katiba mpya wiki hii.

  Mgeni mmoja wapo ni Dr. Kiwangana yule mbunge aliyemwondoa Selelii Nzega. Huyu jamaa anashangaza kuwaponda CHADEMA akidai inakuwaje leo hawataki katiba ijadiliwe kwa haraka kama serikali inavyotaka, wakati ilani yao ilikuwa ni kuwaletea wananchi katiba mpya ndani ya siku 100!

  Inasikitisha kwamba watangazaji wa Star Tv wamemwangalia tu, mpaka kipindi kimemalizika na hakuna aliyerekebisha kauli hiyo ya kupotosha.

  Mpaka kipindi kinaisha, nimebaki kujiuliza nini nafasi ya mwandishi wa habari anayehost vipindi kama hivi? Kumtizama tu mtu adanganye anavyopenda bila kumsahisha pale anapokosea? Au ndo kama tunavyosikia kwmaba Star TV ni tawi la kurugenzi ya Tambwe Hizza?
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  huyu siyo Dr.(Phd) ni Dk Kigangwala ... aende akatibu kwashakoo kwenye vituo vya afya ..
   
 3. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mdhihaki kigangwala na sio profession yake!
   
 4. Chromium

  Chromium JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 598
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ameonyesha kiwango cha chini sana asubuhi hii. Nadhani hata kutibu kwashakoo umemependelea. Ajianze yeye na kwashakoo ya uelewa.
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,140
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  kama mtangazaz alikuwa paul mabuga huyu ndo huwa bogas wa kufa........huwa anaguna guna tu......
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0


  mkuu ... hebu nisaidie ... mbona sijaona insult ya aina yeyote kwenye bandiko langu
   
 7. Edson Zephania

  Edson Zephania Verified User

  #7
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama msomi mwenye Phd, na mwanasiasa nadhan cfa ya hawa wa2 ni kusoma kila wanachodhan kina manufaa. KAMA aliisoma na NAJUA alisoma ilan ya uchaguz ya CDM na hakuilewa au anazuga tu, ni dhahiri kua hata huo muswada anaosema ameusoma ndan ya 1hr bas ndo hajauelewa KABISA. So mi nadhan arud akasome tena af arud pale star tv akafute kauli yake.
   
 8. Chromium

  Chromium JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 598
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Star Tv wana wanatangazaji vilaza sana. Huyu Paulo Mabuga uliyemtaja hanaga kabisa skills za kupata maarifa kwa mgeni anayekuwa amempotezea muda wa kumleta studio. Inakuwa kama anaita mtu ili yeye aje amwonyeshe mgeni huyo jinsi anavyojua mambo. Hulka hiyo hubadilika ghafla inapotekea amemleta mwana CCM. Yeye hubaki anaguna guna tu in agreement na kinachosemwa hata kama ni upupu. Paulo Mabuga ni mfano sahihi kabisa wa watangazaji weupe kabisa kichwani lakini wakijidhania wako njema.
   
 9. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,821
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kuna tatizo kubwa mno la waandishi/watangazaji wetu wa habari katika kudadisi taarifa..,kwa maneno machache wako weupe kichwani hawafanyi 'homework' ya ishu watakayojadili kabla ya kuja studio..
   
 10. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,117
  Likes Received: 2,089
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa Star tv presenters ni vilaza ile mbaya..sijui wana vi cartificate gani.
   
 11. Mlume

  Mlume Member

  #11
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kilichotokea Star TV asubuhi kilinistua kidogo. Kwanza lilikuwa kosa kubwa kuwaleta watu wa itikadi moja pale studio. Hii inaonyesha upungufu mkubwa katika suala zima la ku-balance story! Pili hawakutakiwa kuwaacha wageni wao kuwashambulia watu wengine wasiokuwepo studio wakati wakijua kuwa watu hao hawana nafasi ya kujibu hoja zinazotolewa kuwahusu! Huu ni ukilaza Mkubwa sana wa waandishi wa Star TV pamoja na wageni wao! Hata hivyo mtangazaji wa zamani wa kipindi hicho Dotto Bulendu alikuwa akikiendesha kwa weledi mkubwa kuliko hawa wa sasa hivi!
   
 12. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,032
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mwategema nini kwa watangazaji wetu walioshia form 4,division 4 na kusoma cheti cha uandishi wa habari watakuwa na weledi gani wa kuhoji?? Ukiangalia wenzetu kama CNN,BBC au ALjAZEERA wanaajiri watangzi waliosoma na wenye uelewa mkubwa wa habari na matukio sasa kwetu wanaajiri vilaza ili wawape mshahara kidogo hakuna la maana hapa,wizi mtupu
   
 13. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 693
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Hebu acha dharau huyo ni medicine doctor (MD) muda wa kusoma hiyo course ni miaka sita. Kama angesoma degree uchwara kwa muda huo ni pamoja na master degree. Tumia akili
   
 14. Chromium

  Chromium JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 598
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mlume, ndio maana ni wazi Star tv wanalipwa na CCM kuendesha mavipindi yasiyo na kichwa wala miguu. Main stream media za bongo (zikiongozwa na Star Tv) zinaongozwa na njaa. CCM wanalitambua hilo vizuri sana
   
 15. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Kwa ujumla star tv,ni mali ya x-mbunge ccm.na wanabase upande mmoja,hata ukipiga cm na hoja yako ikawa tough kwa ccm!,mafundi mitambo wana i-nterupt sauti hadi umalize sehemu wasiotaka.na huyu presenter Damu mbaya anawakatiza mada wale waalikwa wakosoa ccm na wasema kwèli huku akiwaacha wa ccm kuongea watakavyo.
   
Loading...