Star Tv na Redio Free kupunguza wafanyakazi

Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,137
48,808
Kampuni kongwe ya habari nchini, Sahara Media Group itapunguza wafanyakazi wake takriban 100. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyoitoa kwa wafanyakazi, Jumatatu hii.
f28a779a8b88e54abbd6867eac71684e.jpg

sahara-media-group-5
Mwenyekiti Mtendaji wa Sahara Media Group, Dr Anthony Diallo

Imesema inachukua uamuzi huo kutokana na kuhamisha matangazo yake kutoka analojia kwenda dijitali na kwamba nia yake ni kupunguza gharama za uzalishaji. Watakaoathirika ni pamoja na watangazaji, watayarishaji wa vipindi na wafanyakazi wengine.

Itatumia takriban vinane kupunguza wafanyakazi ikiwemo utendaji, elimu, umri, nidhamu na vingine na kutumia kipindi cha miezi mitatu kukamilisha mchakato huo.

Wakati huo huo Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Dr Anthony Diallo, amekanusha tetesi zilizoenea kuwa kampuni hiyo imenunuliwa na kampuni ya Nation Media Group baada ya kushindwa kulipa madeni yake.

Madeni hayo ni pamoja na KCB inayodai shilingi bilioni 28, deni la benki ya Mkombozi, malimbikizo ya mishahara na kodi ya TRA shilingi bilioni 4.

“Tuna asset net value ya zaidi ya bilioni 110. Tuna mkopo kama kampuni na benki ya KCB pekee na hatuna deni kama kampuni huko Mkombozi. Kuuza media company kubwa kama yetu unahitaji kibali cha TCRA,” alijibu Diallo,.

“Tunapunguza wafanyakazi kutokana na uwekezaji mkubwa kwenye automation na kutegemea ununuzi wa vipindi badala ya kuvitengeneza wenyewe, ubora wa vipindi vya kutengenezwa na wengine ni bora zaidi.”

Hadi sasa kampuni hiyo imeajiri wafanyakazi zaidi ya 400.

Source: Bongo5
 
Duu kila siku wigo wa ajira za kuajiriwa unazidi kuwa mdogo, walioko shuleni na vyuoni ni kufikiria kujiajiri wamalizapo masomo yao, vinginevyo matatizo kama stress, ugonjwa wa moyo, depression nk yataongezeka maradufu kwa vijana wadogo.
 
Back
Top Bottom