Star Tv LIVE: Jicho letu ndani ya habari

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,879
1,125
wadau karibuni tuungane na kina Dotto Bulendu katika udadavuzi wa habari zilizotokea wiki hii hususan ajali ya mv skagit na ze komed za bunge.
karibuni.
 
meli imetengenezwa 1986 iliuzwa kwa bei chhe tz ikapelekwa kenya kuongezewa ukubwa ili ibebe watu wengi na ukumbuke ilishapigwa marufuku marekani na magazeti yao yalitangaza me3li mbovu yauzwa kwa nchi masikini na ilitakiwa kufanya kazi kwa miaka 25 tu.
karibuni.
 
CCM imefika mwisho, ni nani aliye ruhusu kutumika hiyo screpa!? nani aliye ruhusu iyo meli mbovu isafilishe watu??
 
Ringo, hapa mwanza umeme umekatika sikupati,ungetueleza kwanza chanzo cha huu mgao fake.
 
Tumechoswa na tume zisizo na mafanikio kila kukicha na zinazo maliza kodi za watanzani na huku ajali za meli zikiendelea!

Tunataka uwajibikaji wa viongozi wa sumatra, lazima waoneshe uwajibikaji kwa vitendo kama wakishindwa basi serikali hiwawajibishe.
 
Viongozi wetu wamekuwa mahiri wa kutangaza siku za maombolezo, lakini hawafanyi jitihada zozote kuthibiti ajali za majini! Hii Meli ilikuwa Mbovu na Chakavu lakini wameiruhusu ibebe watanzania!
 
wadau karibuni tuungane na kina Dotto Bulendu katika udadavuzi wa habari zilizotokea wiki hii hususan ajali ya mv skagit na ze komed za bunge.
karibuni.

kuhusu Ze Commedy za bunge, sikufurahishwa na kitendo cha viongozi wa Chadema kumtaka spika akubali hoja ya Mh Tundu Lissu kuhusu Meli ya ZANZIBAR wakati chama Hicho hakionyeshi dalili ya Kuwa na uchungu na tukio hilo hasa viongozi na wabunge wake kushiriki katika music, Kunywa, kucheza ngoma jioni yake ktk harusi ya dk Slaa
 
Ndugai alikataa hoja ya lisu ila ajue hii wizara ya uchukuzi bado haijapitisha bajeti yake ambayo ndio inahusika na hiyo kashifa ,ategemee mbanano mkali
 
Dotto,
hata waandishi mna matatizo ya kuchambua mambo. hivi kama hali ya hewa ilikuwa mbaya ni MV Skagit tuu ilikuwa baharini? MV Kilimanjaro iliyokuwa ya kwanza kusaidia MV Skagit yenyewe ni anti-mawimbi!!! Hakuna hata jahazi au mtumbwi mmoja ulikuwa baharirini siku hiyo
 
huu mzaha mzaha wa serikali !kuna siku utasikia magogoni panaungua halafu fire brigade hawana vitendea kazi.
Vitendea kazi vilivyoko ni mabomu ya machozi tu.
 
Wahenga walinena mpenda vya bure vya gharama haviwezi,jamani msanii mrisho aliimba ya kuwa wanafanya usanii na roho za watu hatukumwelewa.Tutegemee maafa zaidi kwa watawala tulonao,ajali zote hizi wao hapo makini kuzizuia labda pengine utawala wao ni wa umwagaji damu.
 
kuhusu Ze Commedy za bunge, sikufurahishwa na kitendo cha viongozi wa Chadema kumtaka spika akubali hoja ya Mh Tundu Lissu kuhusu Meli ya ZANZIBAR wakati chama Hicho hakionyeshi dalili ya Kuwa na uchungu na tukio hilo hasa viongozi na wabunge wake kushiriki katika music, Kunywa, kucheza ngoma jioni yake ktk harusi ya dk Slaa

Kwani wao ndio walioruhusu kutumika Meli chakavu,
Nyie mfanye upuuzi mtegemee huruma za Chadema!Wajibikeni!
Msinge ingiza hii Meli mbovu
 
kuhusu Ze Commedy za bunge, sikufurahishwa na kitendo cha viongozi wa Chadema kumtaka spika akubali hoja ya Mh Tundu Lissu kuhusu Meli ya ZANZIBAR wakati chama Hicho hakionyeshi dalili ya Kuwa na uchungu na tukio hilo hasa viongozi na wabunge wake kushiriki katika music, Kunywa, kucheza ngoma jioni yake ktk harusi ya dk Slaa

Ni mana yake ya kuangalia sherehe ya harusi kwani yaingilianaje na shughuli za bunge?Hoja ilikuwa ni kujadili kwa nini maafa yanatokea kizembe kizembe ? Au wananufaika na damu imwagikayo? Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa.
 
Back
Top Bottom