Star TV Kuna maisha baada ya uchaguzi

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,171
3,346
Wana JF.

Leo nikiwa kijiwe fulani napata zangu masanga kulikuwa na TV ambayo walikuwa wameweka station ya Star TV. Kwa takribani masaa kama matano niliyokaa hapo nimeona Star TV wamejitoa akili, yaani imekuwa zaidi ya TBC1. Ni full propaganda! Hii inaweza kuwa na madhara makubwa kwa upande wa biashara baada ya muda.

Nadhani ITV hata kama wanatuhumiwa kuwa ni chombo cha wapinzani lakini wako fair au wana balance. Lakini Star TV imekuwa kama CCM TV, hii ni mbaya TV fulani kueleweka moja kwa moja ni TV yenye mlengo fulani au inaegemea upande fulani.

Endapo uongozi wa Star TV hawatamshauri mmiliki wa Star TV ambaye ni kada wa CCM, athari zake ataziona mara baada ya uchaguzi kwisha. Prevention is better than cure.
 
Hata me wananiboa sana hata taarifa zao siku hizi siziangalii kabisa
Halafu wana ving'amuzi vyao vinaitwa Continental sijui watauzaje?? Wajifunze kutoka kwa AZAM TV, hawataki kuingiliwa na wana siasa wao wanafanya yao kwa kufuata weledi.
 
Wana JF.
Leo nikiwa kijiwe fulani napata zangu masanga kulikuwa na TV ambayo walikuwa wameweka station ya Star TV. Kwa takribani masaa kama matano niliyokaa hapo nimeona Star TV wamejitoa akili, yaani imekuwa zaidi ya TBC1. Ni full propaganda! Hii inaweza kuwa na madhara makubwa kwa upande wa biashara baada ya muda. Nadhani ITV hata kama wanatuhumiwa kuwa ni chombo cha wapinzani lakini wako fair au wana balance. Lakini Star TV imekuwa kama CCM TV, hii ni mbaya TV fulani kueleweka moja kwa moja ni TV yenye mlengo fulani au inaegemea upande fulani.

Endapo uongozi wa Star TV hawatamshauri mmiliki wa Star TV ambaye ni kada wa CCM, athari zake ataziona mara baada ya uchaguzi kwisha. Prevention is better than cure.

Tuseme wewe ndiyo mwenye huruma sana na biashara ya mwenziyo au ujumbe umekuchoma baada ya kutokuwa na mahaba nao
 
Inawezekana wamelipwa goto refu ndo maana wanaseema ya chama hicho mara kwa mara.
Tutaelewana pale wananchi watakapoamua 25/10
Mzee wa Rula
 
Last edited by a moderator:
Star TV ni mali ya DIALO ambaye nafikiri ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa MWANZA.Maamuzi yangu ni kuwa siko tayari kuwafuatilia habari zao na CLOUS.Watumishi waaminifu wa CCM.
 
Star TV ni mali ya DIALO ambaye nafikiri ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa MWANZA.Maamuzi yangu ni kuwa siko tayari kuwafuatilia habari zao na CLOUS.Watumishi waaminifu wa CCM.

Mimi sisikilizi tens Cloud FM waache wenye mapenzi yao waisikilize.

Wangechukulia mfano WA Zecomedy umaatufu wao so kama sasa
 
Tulia dawa iingie vizuri kwenye mishipa ya damu ili uweze kupona ungonjwa unaokusibu.
 
Back
Top Bottom