Star TV Kulikoni? Tuongee asubuhi ya Jumapili si Siasa tena!

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,213
Nilikuwa nategemea Star TV ndio chombo consistent katika vipindi vyake.

Nashangaa haya mabadiliko ya mara kwa mara yanatokana na nini, vipindi vimekuwa havieleweki.
Tulizoea Jumapili tuongee asubuhi ni mada zinazohusiana na siasa lakini siku hizi hata mara hakuna mada yoyote, mara elimu. Star TV mnatuangusha.

Yahya vipi kulikoni?
 
Tangu ndugu yao kaukwaa ukubwa huko kwenye chama basi siasa wameacha. Acheni hizo.
 
Kuna likipindi asubuhi hi limeniaharibia siku kabisaa,eti wanasibitisha hakunaga nchi dunian inayoweza kutoa elimu bure na wamekubaliana hivyo,wanasema wana siasa wanao sema elimu bure niwaongo.awe mwandish wageni wa star tv asubuh wote ni ziro,nataman kupasua tv
 
Nilipoona huo upuuzi nikazima TV
 
Boss wao kaukwaa UNEC basi ndo kabisa kwisha kabisa TV YAO.....Sasa Tz hatuna TV kwa ajili ya watu wote zote ni za CCM Labda CDM wafungue TV yao
 
Aibu startv. Watu tunasubiri uhondo nanyi mnabadirisha mada. Alhamiso si kuna elimu. Boss kawazuia!
 
Waageni hawana taaluma inayohusiana na mada..alimradi kipindi kirushwe hewani tu..wiki hii yote hakukuwa na habari za magazetini....Star Tv imekuwaje sijui
 
kwa hakika pasipo CDM TV ndugu zetu maskini tutaumia sana ..naona uhuru wa habari umekwisha sasa,mwanahalisi nayo ndo hv
 
Kufika kule tunataka itakuwa kaazi kweli kweli

ndio hivyo tena mwenye tv kishaingia mstari wa mbele kikosi cha kutafuta ushindi wa ccm 2015 .atuna star tv tena bali kipeperushi cha chama kama ilivyo tbc .hakuna jinsi ila kuipa kwaheri star tv bye bye .
 
Nilikuwa nategemea Star TV ndio chombo consistent katika vipindi vyake.

Nashangaa haya mabadiliko ya mara kwa mara yanatokana na nini, vipindi vimekuwa havieleweki.
Tulizoea Jumapili tuongee asubuhi ni mada zinazohusiana na siasa lakini siku hizi hata mara hakuna mada yoyote, mara elimu. Star TV mnatuangusha.

Yahya vipi kulikoni?

Kuyumba huku kwa star tv kumeanza baada ya mmilikiwake kurudi madakanikwa nguvu katika chama chake cha ccm.

Kamaumefualilia vizuri hata zile hoja nzitonzito na mijadala inayovuta hisia kwa watanzaniawengi inafukiwafukiwa siku hizi.

Hivyo ni viashiria tu vya Star TV kuanza kupoteza uelekeo.
 
JF pekee ndo chombo makini cha habari..................

Nakubalina na wewe mkuu 100%

Tatizo ni watanzania wangapi wanapata habari kupitia huku kwenye mitando ya kijamii? niwalewale wapo face book, twita na

jamii forum. Watanzania wengi watabaki kupigwa propaganda kwa msaada wa TBC na redio zake pia Star TV na redio zake.

Kwasababu Tv na redio zinawafikia watanzania wengi zaid kwa makundi na mmojammoja, tunahitaji chombo huru kuziba nafasi

ambayo sasa inaachwa wazi na Star tv na redio zake.

Doto Bulendu na Yahaya na yule jamaa wa DSM japo amebadili mpaka chumba cha matangazo back ground kuwa ya Kijan

kibichi walianza vizuri tukawategemea nadhani wamedhitiwa, nasasa tunahitaji mbadala haraka iwezekanavyo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom