Star TV Kulikoni? Tuongee asubuhi ya Jumapili si Siasa tena!

hata kile kipindi cha uchambuzi wa magazeti hakieleweki siku nyingine kipo siku nyingine hakipo na hata muda wake wa kuanza kipindi haueleweki!!!
 
Salaam Wakuu,

Binafsi kwa moyo mweupe kabisa uliojaa furaha kwa thamani ya michango ya wadau hapa juu nasukukumwa kuweka mambo fulani sawa nikiwa kama mwajiriwa wa Star TV:

  1. Msemaji wa Vipindi yupo, lakini mabadiliko ya sasa hayana uhusiano wowote na mmiliki wa Chombo kwa masilahi ya kisiasa. Ni feedback nzuri kwa muhusika kuyasoma haya na kurekebisha palipo lege.
  2. Kwa karibu mwezi mzima nimebanwa katika majukumu ya kazi za nje ya kituo na hivyo kukosekana katika mijadala ya siasa kila Jumapili kama ilivyo ada na utamaduni wa kipindi.
  3. Kwa sasa nitakuwa nasikika kutoka DSM kuanzia wiki ijayo panapo majaaliwa yake muumba, ungwe hiyo ya Jumapili itaaimarishwa zaidi.
  4. Ahsante MOHAMED MTOI kwa Tweet yako iliyonitoa usingizini na KAPOTOLO kwa arlert muhimu. nina uda wa zaidi ya wiki mbili nilikuwa sijasign in jamvini.

Tukutane katika kipindi wiki Ijayo, update nyinginezo nitazitoa hapa hapa JF

Ahsanteni sana wakuu
 
Back
Top Bottom