STAR TV in TANZANIA - KATIBA MPYA

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
Napenda kuwapongeza star TV kwa ubunifu walionao kwa kupenda kuweka vipindi vizuri na vinavyoleta tija katika taifa letu. Jana kulikuwa na kipindi kizuri sana kuhusu mjadala wa KATIBA MPYA. Me napenda kuwashukuru na muendelee na moyo huo huo, Kwa upande wa MZA kulikuwa na YAHAYA MOHAMED na wanafunzi wawili kutoka SAUT, Upande wa Dar, kulikuwa na Mh Kafulila(NCCR), Mtatiro(Cuf) na Mwita Mwikabe(Chadema). Kweli kilitoa picha wananchi tunahitaji katiba mpya na mimi naomba hili liendelezwa na vituo vingine pia kama ITV na TBC, WASIONE HAYA maana hili swala si la chadema, wala dr slaa wala cuf wala nccr ni la wote. HATA TBC wasione haya.

Kweli STAR TV mmekomaa na mpo tayari kwa hilo na tumshukuru mh Antony Diallo kwa hilo.
 
Wameiuza kwa ccm??hiyo tv-station??mbona wamebadirisha logo imekuwa ya njano na kijani??
 
hakika nami napongeza star tv kwa kipindi hicho cha TUONGEE ASUBUHI huwa nawafatilia saana, wanajitahidi kuwa makini japo hatujafikia viwango vya media transparency.
Binafsi sijaelewa pia imekuwaje wameibadilisha logo yao toka kijani na kuwa njano...LAKINI HUENDA WAMEAMUA KUWEKA UHALISIA WA NYOTA NA NURU YAKE YA NJANO.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom