Star Times hawana uzalendo kabisa

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,663
20,418
Matangazo ya moja kwa moja (LIVE) kutoka uwanja wa Uhuru yakionyesha sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika yamekatwa ghafla. Najua watu wengine watakuwa walidhani ni TBC ndio waliokata matangazo hayo. Lakini wenye matatizo ni Star Times ambapo channel zao zote za king'amuzi chao zimekata matangazo. Nimejaribu kuwapigia kupitia namba yao ya Customer Care 0764-700800, jamaa wameamua kuizima kabisa. Huo ni uhuni mwingine. Nimejaribu kupiga simu kwa agent wao mkubwa akaniambia eti 'wanaongeza channel kwenye mnara wa Makongo'. Nina mashaka na jibu hilo, kwani channel haziongezwi kwenye mnara. Pia inajulikana kwamba hata kabla ya kuweka mnara wa Makongo, watu wa Dar tulikuwa tunapata mawasiliano kutoka Kisarawe. Sasa najiuliza maswali mawili: Hata kama kuna sababu za matengenezo ya kiufundi yaliyoratibiwa, kwa nini wasifanye muda mwingine ili watu waliopumzika kwa kutokwenda kazini wafuatilie maadhimisho ya kitaifa? Pili, kwa nini hawatoi taarifa hata ya sms au kupitia bulletin ili mtu ujipange kwa ratiba nyingine mapema? Kwa nini wazime simu ya Customer Care?
I present.
 
wanaboa sana....chaneli zote hazionekani kasoro chaneli 022 ndio TBC1 LIVE INAONEKANA
 
Asante mkuu kwa taarifa....hata mimi nilijua kwangu tu, kidogo nipande juu! dah hawa jamaa feki kweli
 
Ndiyo wamerudi hewani sasa hivi 1:04 pm, TCRA inabidi wawatoze FAINI kubwa hii haivumilik hata kidogo.
 
Back
Top Bottom