Stanslaus Nyongo: Pamba imegeuzwa kuwa zao la kisiasa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,167
2,000
Mbunge Stanslaus Nyongo amesema licha ya zao la Pamba kulimwa katika mikoa kadhaa Nchini ikiwemo Simiyu na Shinyanga, Uzalishaji wake umekuwa na kelele kwasababu ya kukosa soko la kudumu

Akiwa Bungeni amesema, "Mkulima wa Pamba ananyanyasika miaka yote. Sisi kwetu Pamba imebadilika, limekuwa sio tena zao la Biashara bali la Kisiasa"

Amesema wanaapoomba Kura, Madiwani na Wabunge huongelea maslahi ya zao hilo ili kupata kura akiongeza, "Sisi Wabunge wa Mikoa inayozalisha Pamba tukirudi hivi hivi hatutarudi Bungeni kwasababu Wakulima wengi wanaona kama hatuwatetei"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom