Stanlaus Nyongo, ameipongeza Wizara Ya Elimu, Sayansi na Teknoloji , kwa usimamizi na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Ufanisi

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
TAARIFA KWA UMMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na maendeleo Ya Jamii, Mh. Stanlaus Nyongo, ameipongeza Wizara Ya Elimu, Sayansi na Teknoloji , kwa usimamizi na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Ufanisi.

Akizungumza katika kikao cha pamoja, kati ya uongozi wa Wizara, Taasisi zilizo chini ya wizara na kamati hiyo, kilichofanyika jijini Dodoma, Mh. Nyongo amesema kufanyika kwa kikao hicho, chenye lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Majukumu ya wizara na Utekelezaji wa Miradi ya Elimu. Kumewezesha kuifahamu vizuri wizara na shughuli zinazotekelezwa na wizara.

Akizungumza kwa niaba ya wizara Mh. Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi Na Teknolojia, Profesa Jemes Mdoe, ameiahidi kamati hiyo kufanyia kazi maoni, mapendekezo na ushauri walioutoa ikiwemo kuiweka katika mikakati ya wizara.

Aidha ameishukuru kamati hiyo kwa kuipongeza wizara kwa kazi nzuri ambayo wanekua wakifanya katika kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata Elimu bora.

Kuipongeza wizara ya elimu kwa kutekeleza miradi ni kichekesho!

Angeipongeza kuandaa mtaala wa kufundisha Historia ya Tanzania angalao.Angeipongeza kiajiri walimu wa kutosha,angeiponge kuboresha maslahi ya waalimu,angeipongeza kuboresha mitaala n.k
 
Viongozi wetu maigizo mengi sana
 
Kuipongeza wizara ya elimu kwa kutekeleza miradi ni kichekesho!
Angeipongeza kuandaa mtaala wa kufundisha Historia ya Tanzania angalao.Angeipongeza kiajiri walimu wa kutosha,angeiponge kuboresha maslahi ya waalimu,angeipongeza kuboresha mitaala n.k
Viongozi wetu maigizo mengi
 
Hii nchi ni kisiwa cha kufikirika kha
Ni maigizo mwanzo mwisho
Shida ni ujinga
Wajinga ndio wamepewa dhamana ya kuiongoza nchi
 
Back
Top Bottom